Kwanini kukosoana mambo ambayo siyo ya msingi?

Mwiyuzi

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
853
440
Kuna aina ya watu ambao wanaonaga wao wanajua kila kitu, wao ndo wanaowaza na kufanya vitu sahihi, yaani hawakoseagi!

Mfano siku ya leo ni Siku ya Mama duniani, unakuta mtu anatoka mapovu kuponda wanaopost au kusifia mama zao! Mpaka unamshangaa!

Ni kweli kuwa upendo wa mtoto kwa mama hauonekani kwa kupost kwenye mitandao ya kijamii, lakini pia, asiyepost naye siyo kwamba ndo anamjali mama yake sana!

Tuache ku-complicate maisha. Kisichokufurahisha wewe siyo lazima kisimfurahishe na mwingine, kibaya kwako kwa mwingine Lulu!

#FanyaKituRohoInapenda#
 
Back
Top Bottom