Kwanini kesi ya utakatishaji fedha haina dhamana? Utakatishaji unaanzia wapi?

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
4,855
2,000
Naelewa kuwa utakatishaji fedha ni kitendo cha mtu kuficha chanzo cha fedha alizozipata kiharamu na kuzifanya zionekane zinetoka kwenye vyanzo halali..

Swali la kwanza: ili kitendo kiitwe utakatishaji frdha kinaanzia kiasi gani au operation kubwa kiasi gani.
Mfano nikiwa nafanya biashara ya dawa za kulevya na fedha zangu nikaziingiza kwenye casino zikaonena kama ni fedha za wacheza kamari, hapo bila shaka ni utakatishaji wa fedha

Je, kama ni mfanyakazi wa umma, akawa anadokoa kidogo kidogo kama laki 2 kwa mwezi hivi akawa anapeleka kwenye duka lake ili kufanya kipato chake cha ziada kionekane kinatokana na biashara yake ya duka, badala ya wizi, huyu naye akigundulika atapewa kesi ya utakayishaji fedha?

Swali jingine: Ni sababu gani inayofanya kesi hii watuhumiwa wake wanyimwe dhamana? Maana kesi ambazo hazina dhamana kisheria ni za makosa makubwa ambayo mtu kesi ambazo mtuhumiwa akikutwa na hatia anapewa adhabu kubwa kama vile kunyogwa, ila utakatishaji fedha adhabu yake sio kubwa na mtuhumiwa ananyimwa dhamana?

Mfano kuna kesi ya jamaa anaitwa Ndama mtoto wa ng'ombe inayohusu utakatishaji, adhabu yake ilikuwa ni miaka 5 jela, kesi ya kubaka ni miaka 30 jela na ina dhamana..
Kuna nini?

NDAMA Mtoto wa Ng'ombe ahukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya mil. 200 - MICHUZI BLOG

Wadau wa sheria kams Petro E. Mselewa Stanley Mitchell II Retired na wengine mnaojua sheria
 
Mina cute

JF-Expert Member
Sep 18, 2018
1,144

Ukiwa unauza let say drugs, halafu pesa yk ukaenda kununulia friji au TV palé duka la LG mlimani city ukapewa na risiti halali Ya efd, bas ht kwa ilo dogo tu ushanasa Kwenye money laundaring, ht pesa ambayo umeiba kazini kwako
 
chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
4,855
2,000
Ukiwa unauza let say drugs, halafu pesa yk ukaenda kununulia friji au TV palé duka la LG mlimani city ukapewa na risiti halali Ya efd, bas ht kwa ilo dogo tu ushanasa Kwenye money laundaring, ht pesa ambayo umeiba kazini kwako
Basi mtu akiwa mwizi pia automatically atakuwa na kesi ya kutakatisha fedha pia, maana fedha atazitumia kwa matumizi halali

So, kwa nini haina dhamana?
 
100 Likes

JF-Expert Member
Nov 5, 2018
2,373
2,000
So, kwa nini haina dhamana?
Hujambo?

Kuna mtu anatumia avatar yako humu na anaandika thread za kipuuzi puuzi.

Kuhusu topic yetu, sina uhakika kama kesi zote tunazoziita ni Money Laundering zinakidhi vigezo sahihi vya kimataifa kuita hivyo. Isipokuwa naona ni kama inatumika kisiasa kwa wale tunaotaka kuwasotesha gerezani.

Nitaandika kidogo kwenye post nyingine juu ya jinsi ambavyo case inachukuliwa kuwa sensitive kiasi cha kutokuwa na dhamana, ingawa siyo kwa upande wa kisheria, maana mimi siyo mwanasheria.
 
citymist

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
701
1,000
Ndio Tatizo la kukopi Sheria, na zinawekwa makusudi ili ziwe zinatumika kuwakomoa watu hasa wa mlengo wa kushoto na msio watoto pendwa. Aingii akilini watu wenye akili timamu mnatunga sheria Kama hii haina dhamana!! Sijui ni usalama wa mtuhumiwa!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
4,855
2,000
Ni kwa sababu ya uzito wake mkuu.

Hii inalenga kukomesha kabisa swala hilo liogopwe.ni sawa na fedha bandia tofauti yake hizi ni halisi.
Bado mantiki yake sijaiona, kama ni kokomesha basi wangekua wanatoa adhabu kali kwa wanaokutwa na hatia, ila anayekutwa na hatia anapewa kifungo cha miaka 5 tu, halafu kesi haina dhamana..Yaani mtu unaweza kukaa mahabusu muda mrefu ukiwa mtuhumiwa kuliko muda ambao ungekaa kama ungekutwa na kosa
 
chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
4,855
2,000
Ukiwa unauza let say drugs, halafu pesa yk ukaenda kununulia friji au TV palé duka la LG mlimani city ukapewa na risiti halali Ya efd, bas ht kwa ilo dogo tu ushanasa Kwenye money laundaring, ht pesa ambayo umeiba kazini kwako
Basi mtu yoyote anayeiba hela basi atakuwa ana kosa ls kutakatisha fedha automatically..maana ataenda kuitumia hiyo matumizi ya kawaida
 
100 Likes

JF-Expert Member
Nov 5, 2018
2,373
2,000
Basi mtu yoyote anayeiba hela basi atakuwa ana kosa ls kutakatisha fedha automatically..maana ataenda kuitumia hiyo matumizi ya kawaida
Ukipata muda soma hii article hapa, huyu jamaa ana mawazo kama yako (of course na yangu pia) kwamba kuna unyanyasaji kwenye hizi case na kwamba hazijatatua tatizo ila government officials wanatumia kama karata yao kuwanyanyasa wananchi:-

Why the War on Money Laundering Should be Aborted
 
100 Likes

JF-Expert Member
Nov 5, 2018
2,373
2,000
Ukiwa unauza let say drugs, halafu pesa yk ukaenda kununulia friji au TV palé duka la LG mlimani city ukapewa na risiti halali Ya efd, bas ht kwa ilo dogo tu ushanasa Kwenye money laundaring, ht pesa ambayo umeiba kazini kwako
Principally, hata yule aliyekuuzia anatakiwa ahusishwe kwenye case; awe amekuuzia kwa kufahamu au kutofahamu chanzo cha hela yako ni kwamba kawezesha wewe kutakatisha fedha.

Swali, je kwa hapa kwetu kuna kesi yoyote umesikia imemhusu official yeyote kutoka kwenye financial institutions?
 
bigmind

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
12,246
2,000
Ukiwa unauza let say drugs, halafu pesa yk ukaenda kununulia friji au TV palé duka la LG mlimani city ukapewa na risiti halali Ya efd, bas ht kwa ilo dogo tu ushanasa Kwenye money laundaring, ht pesa ambayo umeiba kazini kwako
Sababu ni kesi za/ya uhujumu uchumi ambayo ni miongoni mwa kesi sizizo na dhamana..!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mina cute

JF-Expert Member
Sep 18, 2018
1,144
2,000
Basi mtu yoyote anayeiba hela basi atakuwa ana kosa ls kutakatisha fedha automatically..maana ataenda kuitumia hiyo matumizi ya kawaida
Ela iliyopatikana Kwa zao la uhalifu, then ukaenda kununulia kitu halali, hapo tayari mtu hawezi jua kama ili Gari lenye kadi halisi limenunuliwa kwa hela Ya wizi au ya drugs, au kuiba serikalini, au Ya kutaperi, etc,

Sheria hii nzuri, ila ubaya Wake ile kukosa kuwa na option ya dhamana
 
Mina cute

JF-Expert Member
Sep 18, 2018
1,144
2,000
Sababu ni kesi za/ya uhujumu uchumi ambayo ni miongoni mwa kesi sizizo na dhamana..!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kesi za uhujumu uchumi zina dhamana, il tatizo mara nyingi dhamana zake zinahusisha ela keshi, au hati ya nyumba yenye thamani sawa ña kesi,,
Kama kesi ina thamani ya millón 400, hapo lazima uache mahakamani milioni mia mbili keshi ndo upate dhamana
 
bigmind

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
12,246
2,000
Kesi za uhujumu uchumi zina dhamana, il tatizo mara nyingi dhamana zake zinahusisha ela keshi, au hati ya nyumba yenye thamani sawa ña kesi,,
Kama kesi ina thamani ya millón 400, hapo lazima uache mahakamani milioni mia mbili keshi ndo upate dhamana
Okay! Ngoja niendelee kusoma zaidi..! So chinchilla is wrong..?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CaprePoint

Member
Dec 30, 2018
46
125
So, kwa nini haina dhamana?
Navyojua sio kwamba hazina dhamana.. issue ni kuwa mahakama za chini (hakimu mkazi na zingine) hazina uwezo wa kutoa dhamana kama kesi inahusisha zaidi ya tsh bilion 1.

Ila kesi hiyo ikifika mahakama kuu mtuhumiwa anaweza pewa dhamana kama atakidhi vigezo.

Tatizo ni hadi ifike mahakama kuu(uchunguzi ukamilike) utakuwa ushasota sana mahabusu.
 
Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
9,451
2,000
So, kwa nini haina dhamana?
Miongoni mwa sheria tulizopandikiziwa na mabeberu na kusema kweli zipo kwa ajili ya kuumiza na kukomoa watu! Sheria kama hizi zilianzia nchi za Ulaya na Marekani ili kulinda mabenki na Taasisi zao za fedha.

Watawala wa Kiafrika wakaichukua lengo kubwa(sio la wazi) ikawa ni kuitumia sheria hii ili kuwadhibiti watu kisiasa, kwamba kusiwe na pesa nyingi kwenye mzunguko au mikononi mwa watu zikatishia kuanguka kwa tawala zao maana watawala wa Kiafrika wanaamini mtu mwenye uwezo wa kiuchumi na fedha hatawaliki!!!

Kama waendesha mashtaka wakiona hawana ushahidi wa kutosha kukutia hatiani basi watatumia sheria ya utakatishaji pesa ili tu ukae ndani muda wote wa kusikilizwa kwa kesi yako hata kama ni miaka saba and for them, they have nothing to loose weather after all that time you will be convicted or not. Wanafurahi wameshakuadhibu, wameharibu maisha yako na familia yako n.k!

Natamani atokee mtu akai challenge hii sheria mahakamani ifutiliwe mbali kwa sababu inapingana na katiba kwamba mtu yeyote atakua hana hatia mpaka mahakama ithibiishe vinginevyo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom