Kwanini kesi ya utakatishaji fedha haina dhamana? Utakatishaji unaanzia wapi?

Miongoni mwa sheria tulizopandikiziwa na mabeberu na kusema kweli zipo kwa ajili ya kuumiza na kukomoa watu! Sheria kama hizi zilianzia nchi za Ulaya na Marekani ili kulinda mabenki na Taasisi zao za fedha.

Watawala wa Kiafrika wakaichukua lengo kubwa(sio la wazi) ikawa ni kuitumia sheria hii ili kuwadhibiti watu kisiasa, kwamba kusiwe na pesa nyingi kwenye mzunguko au mikononi mwa watu zikatishia kuanguka kwa tawala zao maana watawala wa Kiafrika wanaamini mtu mwenye uwezo wa kiuchumi na fedha hatawaliki!!!

Kama waendesha mashtaka wakiona hawana ushahidi wa kutosha kukutia hatiani basi watatumia sheria ya utakatishaji pesa ili tu ukae ndani muda wote wa kusikilizwa kwa kesi yako hata kama ni miaka saba and for them, they have nothing to loose weather after all that time you will be convicted or not. Wanafurahi wameshakuadhibu, wameharibu maisha yako na familia yako n.k!

Natamani atokee mtu akai challenge hii sheria mahakamani ifutiliwe mbali kwa sababu inapingana na katiba kwamba mtu yeyote atakua hana hatia mpaka mahakama ithibiishe vinginevyo
Kenya nasikia ina dhamana
 
Mkuu mimi siyo mwanasheria, lakini nitajibu kiasi nachoweza, akitokea mwanasheria hapa basi aje atuweka sawa.
Kutakatisha pesa ni zoezi la kuingiza kwenye mzunguuko pesa ambayo imepatikana kwanjia ambayo huwezi kuitolea maelezo mbele ya ofisa wa kodi.
Mfano hela uliyolipwa ili utekeleze tukio la kigaidi, pesa uliyolipwa baada ya kuuza nyara za serikali, pesa zako ulizochuma baada ya kuuza madawa ya kulevya nk. Hii ni moja kati ya sheria ngumu sana, maana ukiangalia mifumo ya maisha ya watanzania ni rahisi sana kujikuta umetupiwa kwenye jinai hii.
Hata hivyo kuwanyima dhamana watu hawa ni ule uoga dhidi yao hasa hasa ni kujaribu kuwazuia wasivuruge ushahidi, kuwadhuru mashahidi nk.
Kwakuwa inadaiwa wauza unga wa kulevya, magaidi na wauza nyara ni watu wenye uwezo wa kuifanya meri ipae au ndege itue sokoni hasa kwenye nchi za kimasikini kama hizi zetu.
Kwamba wana uwezo kugeuza matokeo kwa kutumia ukwasi wao.
Nadhani huko nyuma tulishawahi kusikia watu waliodai kuwa na uwezo wa kuiweka mfukoni Serikali, sheria hii ndiyo dawa ya watu hao.
Sheria hii ina faida hasa kuwadhibiti matajiri wenye fujo, lakini inaweza kutumika vibaya na maofisa wa Serikali wanaopenda kutumia nafasi zao kuwaumiza wananchi kiasi ambacho hata masikini akajikuta anasukumiwa huko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiwa unauza let say drugs, halafu pesa yk ukaenda kununulia friji au TV palé duka la LG mlimani city ukapewa na risiti halali Ya efd, bas ht kwa ilo dogo tu ushanasa Kwenye money laundaring, ht pesa ambayo umeiba kazini kwako
No thank you... Kutakatisha fedha ni kutumia fedha haramu kuanzaisha biashara halalii.. Kuiba na kununua friji ya nyumbani ni Ufisadi labda kama friju utalitumia kama source ya pesa ili kuficha wizi wa fedha ulizoiba..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani hela yoyote haramu. Iwe ya rushwa, wizi, utapeli nk kuingiza kwenye mfumo ionekane ni hela halali, itakuwa ni money laundering. Tafsiri pana.
Ndiyo maana akina Kaburu, Malinzi, Kitikya inawahusu.
Kiasi fulani inatumika kukomoa watu wakae ndani bila dhamana.
 
Mkuu mimi siyo mwanasheria, lakini nitajibu kiasi nachoweza, akitokea mwanasheria hapa basi aje atuweka sawa.
Kutakatisha pesa ni zoezi la kuingiza kwenye mzunguuko pesa ambayo imepatikana kwanjia ambayo huwezi kuitolea maelezo mbele ya ofisa wa kodi.
Mfano hela uliyolipwa ili utekeleze tukio la kigaidi, pesa uliyolipwa baada ya kuuza nyara za serikali, pesa zako ulizochuma baada ya kuuza madawa ya kulevya nk. Hii ni moja kati ya sheria ngumu sana, maana ukiangalia mifumo ya maisha ya watanzania ni rahisi sana kujikuta umetupiwa kwenye jinai hii.
Hata hivyo kuwanyima dhamana watu hawa ni ule uoga dhidi yao hasa hasa ni kujaribu kuwazuia wasivuruge ushahidi, kuwadhuru mashahidi nk.
Kwakuwa inadaiwa wauza unga wa kulevya, magaidi na wauza nyara ni watu wenye uwezo wa kuifanya meri ipae au ndege itue sokoni hasa kwenye nchi za kimasikini kama hizi zetu.
Kwamba wana uwezo kugeuza matokeo kwa kutumia ukwasi wao.
Nadhani huko nyuma tulishawahi kusikia watu waliodai kuwa na uwezo wa kuiweka mfukoni Serikali, sheria hii ndiyo dawa ya watu hao.
Sheria hii ina faida hasa kuwadhibiti matajiri wenye fujo, lakini inaweza kutumika vibaya na maofisa wa Serikali wanaopenda kutumia nafasi zao kuwaumiza wananchi kiasi ambacho hata masikini akajikuta anasukumiwa huko

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwani hii utakatishaji fedha inaanzia kiasi gani cha fedha? Maana hata laki 3 mtu anaweza kuitakatisha pia

Najua jamaa ambae ana uwezo wa kawaida tu kapewa hii kesi
 
Hii sheria nadhani ilipitishwa kipindi cha Nyerere enzi za uhujumu uchumi,haiendani na mazingira ya uchumi na Maisha ya sasa.Bahati mbaya kwa sasa inatumika kukomoa watu na kuwaumiza tu wale ambao hawako kwenye good books na viongozi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii AMLA ipo kitambo na 2012 imefanyiwa amendment kuiboresha zaidi ipo vizuri kunyoosha mafisadi
 
Watu wangapi wamewekwa rumande kwa kesi za utakatishaji fedha kisha wakashinda kesi au dpp akaamua kwamba hana nia ya kuendelea na kesi?Dhamana ni haki ya raia na pale mahakama ikimkuta ana hatia basi kifungo kinamhusu.
Hii AMLA ipo kitambo na 2012 imefanyiwa amendment kuiboresha zaidi ipo vizuri kunyoosha mafisadi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kwa mantiki hii basi kesi zote zingekuwa hazina dhamana ili watu wasifanye makosa...mbona uhujumu uchumi, rushwa zina dhamana?
Hoja nzuri Sana , kesi ambazo hazina dhamana ni kukomoana Tu , hakuna logic yoyote, kutompa dhamana mtu maana yake ni kumkuhumu mtu kabla hata kesi haijatolewa uamuzi
 
Ndio Tatizo la kukopi Sheria, na zinawekwa makusudi ili ziwe zinatumika kuwakomoa watu hasa wa mlengo wa kushoto na msio watoto pendwa. Aingii akilini watu wenye akili timamu mnatunga sheria Kama hii haina dhamana!! Sijui ni usalama wa mtuhumiwa!.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo wakiruhusu dhamana itakuwa ndyo km wameruhusu raia kufanya miamala watakavyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii AMLA ipo kitambo na 2012 imefanyiwa amendment kuiboresha zaidi ipo vizuri kunyoosha mafisadi

“ipo kunyoosha mafisadi”

unanyoosha vipi mafisadi wakati adhabu yake ni laini ? ( miaka 5, faini milioni 50, 100)?
 
Hii sheria nadhani ilipitishwa kipindi cha Nyerere enzi za uhujumu uchumi,haiendani na mazingira ya uchumi na Maisha ya sasa.Bahati mbaya kwa sasa inatumika kukomoa watu na kuwaumiza tu wale ambao hawako kwenye good books na viongozi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii AMLA ipo kitambo na 2012 imefanyiwa amendment kuiboresha zaidi ipo vizuri kunyoosha mafisadi
Yes uko sahihi , hivi kwann wanasheria ( watu) hawaipingi hiyo Sheria ? Maana haina tija
Tija uliyokuwa unaitaka Ni ipi mkuu?
 
Hata hivyo kuwanyima dhamana watu hawa ni ule uoga dhidi yao hasa hasa ni kujaribu kuwazuia wasivuruge ushahidi, kuwadhuru mashahidi nk.

...kutumia ukwasi wao.

Sheria hii ina faida hasa kuwadhibiti matajiri wenye fujo

vipi suspect mwenye pesa ambae hakupewa charge ya utakatishaji fedha (kakutwa nazo ndani), na amepewa dhamana, huyu hawezi kuharibi ushahidi na kudhuru mashahidi wa ukwasi wake?

Au “matajiri wenye fujo” ni waliotakatisha fedha tu?
 
Back
Top Bottom