Kwanini kazi nyingi za kijasusi ni za kifamilia (Family-friendly)?

God'sBeliever

JF-Expert Member
Sep 1, 2015
5,790
3,020
Katika maisha ya binadamu ni watu wachache sana tena ambao ni vichaa, matahira au waliologwa ndio wanaoweza kwenda kinyume na wazazi wao au kwa kwa lugha rahisi kuwasaliti wazazi wao au kuwa ignore completely.

Ni jambo gumu sana kwa binadamu kulifanya kwani watoto huwapenda sana wazazi wao na ni kweli ni watu muhimu sana kwao. Wamewalea na kuwafikisha hapo walipo.

Sasa wazee wa kazi (KITENGO) wanachukulia fursa hii adimu kupata credible asset au watu wa kuaminika.

Ni rahisi kuwaamini bila mashaka.

Wazazi wao nao wanakua na details zao ndani ya hizo agency hivyo mambo yanakua mbwito mbwito.

Hii njia imewamaliza watu wengi sana na kwa bahati mbaya hawajitambui. Kwa hiyo wanaliwa kiulaini mno kwa kuwa brainwashed na wazazi wao wenyewe.

Kwa hili nawalaumu sana wazazi na mwisho wa siku malipo ni hapa hapa duniani tuu na motoni utalipa, Nalaumu hili iwapo kijana/mtoto ataingizwa chaka kwa kupitia wazazi wake.

Watoto wengine unakuta walishapangiwa siku nyingi sana na wazazi wao kuuawa kwa malipo fulani/kuuzwa.

Most intelligence agencies zote za huu ulimwengu hufanya hivyo, akina CIA, KGB, Mossad and so on…

Unaweza shangaa taifa kubwa kama marekani/USA lenye maadui kila kuona ya ulimwengu hadi kuzimu kwanini hawaangushwi/hawaadhibiwi? Lina kila aina ya races/jamii zote za ulimwengu so kutengeneza ma agent wa covert operation ni simple sana lakini kwanini hili linakua gumu?

Jibu ni fupi tuu hilo taifa lina watu wanalishikilia. Nafasi nyeti hawapewi watu tuu from no where.

Wapo watu wa kuaminika toka vizazi na vizazi ambao taarifa zao hazipo popote wala hawaongelewi kabisa hawa ndio roho ya hilo taifa.

Hizo nafasi nyingine sio deep na ikitoke shida mhusika anadhibitiwa mara moja.

Mataifa yanaendeshwa kiutaalamu sana. Hata wale wanaolalamika huku kwamba wana vipaji lakini hawapewi hizo nafasi wajue tuu wanajulikana vizuri sana ila hawafai kwani ni threat na pengine background ya wazazi wao ni mbaya pengine ni defector au wapinzani au walidhulumia. Kwa hiyo kupunguza visasi na matatizo yatakayotokea wanakua omitted mapema sana.

NB:Ndugu zangu kwa upendo wangu kwenu nawaombeni sana msimuamini mtu yeyote yule chini ya jua ila ishini na wato wote vizuri hata wabaya wenu. Binadamu ni dhaifu sana na niwaambieni tuu hakuna mtu atakaeweza kutoa uhai wake kwa watu wengine na wanaogopa onyo. Kaeni mbali sana na marafiki zenu wa karibu (damu damu) na ndugu zenu wa kuzaliwa. Kaeni mbali sana na girl/boy friend, wachumba, masela/washkaji, wake na waume zenu. Hao ni target/silaha ya maangamizi na njia ya kufikia target(Mlengwa wao). Watu wengi wameuawa na watu wao wa karibu kama Rais wa Burkina-faso marehemu Thomas Sankara (Aliuawa na rafiki/mlinzi wake mkuuu Blaise Compaore aliekuja kuwa Rais baada ya yeye, alipoulizwa alisema makomandoo wa ufaransa ndio waliohusika), Laurent Kabila uyu alikua rais wa Congo DRC aliuwawa na bodigadi wake, Fidel Castrol mkewe alitumiwa na CIA kumuwekea sumu kwenye kinywaji lakini Fidel alishtukia mchezo hivyo akakishinda kifo na wengineo.

Chunguzeni kwa kina tuu hata kwenye /mitaa/vijiji/miji/familia zenu vifo vya kitata/kishirikina/kichawi wahusika wakuu ni watu wa karibu hivyo ni vyema kuokoka mapema kuwa na kinga ya Mungu kwa maana maadui ni wengi na vita mipiganavyo sio vya kimwili bali vya kiroho. Mambo mengi huanzia ulimwengu wa kiroho ila sasa kama huna uelewa na haya mambo ni vyema uanze kuutafuta utukufu wa Mungu mapema sana. Tafuta wachungaji kwenu, mafundisho google, youtube, facebook, instagram hata hapa lipo jukwaa la dini/imani upate kujifunza.

It’s dangerous game to trust anyone even your lovely parents/children. Usiwe na aibu ya kuwatupilia mbali watu wako wa karibu eti kisa watakuona vibaya. That is wrong… ndipo watu wengi wanapoangukia kwa hofu ya kukwepa lawama. Ukiona shida sana ita mtu wako huyo wa karibu mwambie waogopa mabaya yatakayomkumba kwa kuwa karibu na wewe. Hata maandiko yanasema amuaminiye binadamu amelaaniwa.

Bora lawama kuliko fedhea/kifo”

Ni muhimu sana kuisikiliza sauti ya MUNGU kuliko binadamu, Na tatizo la binadamu hawaamini bila kushuhudia ila naama mhusika ukipuuzia sauti moja au mbili halafu ukaona madhara basi utajifunza kitu na utamuamini MUNGU siku zote za maisha yako.

Kua na positive mind. TRUST GOD ONLY!

Trust but verify - Ronald Reagan

Good luck! Mungu awe nanyi, wakuu.

Mika 7:5-6
 
NI KAMA UNAYACHAMBUA MAISHA YANGU NA VILIVYONIKUTA NA VINAENDELEA KUNIKUTA,ILA NINAWANYOOSHA VYEMA SASA BAADA YA KUYANG'AMUA WALIYOYATENDA.
Sio wewe tuu mkuu wapo wengi mno ila shida ni namna ya kuwasadia. Yes wapo wengi sana walioingizwa mkenge kwa kpitia wazazi, walezi na ndugu zao lakini tunawasaidiaje? Lengo ni kuwakomboa makuchani mwa shetani...
Kwa kutumia hizi social networks ni njia sahihi na rahisi ya kuwasaidia walengwa wanaopitia haya mauza uza maana najua taarifa zina flow haraka sana.

Goodbles you ndugu MUNGU ni mwema kwa wale wanaomtumainia, Kamwe Mungu hawasahau wanyonge na wanaaonewa bali waovu watakumbwa na adhabu ya Mungu.
 
Dunia ni ngumu sana na ni pana ajabu.
 
Japo sipo ktk hizo familia za kijasusi ila ulichokiongea kuhusu wanaotuzunguka hujakosea.

Nimepitia changamoto nyingi kumbe chanzo ni baadhi ya marafiki na wengine ni waliokuwa wafanyakazi wenzangu.

Baada ya kutafakari kwa kina na kuchunguza nikashtukia mambo, sasa hivi maisha yana muelekeo mwingine.

Ahsante sana kwa somo MURUA kabisa.
 
taamu,

Mtegemee mungu kila kitu kitakua chepesi sana mkuu. Ila isimame kweli kweli kiimani maana Mungu hukaa karibu na mtu mwaminifu. Iwapo imani yako itayumba kidogo basi yatakukuta yaliyomkuta mose na hatimae hakuiona tena nchi ya ahadi kwa sababu ya mashaka yake.
 
Japo sipo ktk hizo familia za kijasusi ila ulichokiongea kuhusu wanaotuzunguka hujakosea.

Nimepitia changamoto nyingi kumbe chanzo ni baadhi ya marafiki na wengine ni waliokuwa wafanyakazi wenzangu.

Baada ya kutafakari kwa kina na kuchunguza nikashtukia mambo, sasa hivi maisha yana muelekeo mwingine.

Ahsante sana kwa somo MURUA kabisa.

Mtangulize Mungu mkuu.
 
1. Huruma huzaa dhambi/maumivu

2. Mazoea yana tabu/kunao watu uliowazoea ambao ndio chanzo cha mateso yako na mahangaiko yako

3. Nasema hivi!, chunga sana ndoto zako asizijue yeyote akujuae.
 
1. Huruma huzaa dhambi/maumivu

2. Mazoea yana tabu/kunao watu uliowazoea ambao ndio chanzo cha mateso yako na mahangaiko yako

3. Nasema hivi!, chunga sana ndoto zako asizijue yeyote akujuae.
Ndio hali halisi mkuu yani maisha ni full kuigiza sasa usipokua na exposure umeliwa.
 
1. Huruma huzaa dhambi/maumivu

2. Mazoea yana tabu/kunao watu uliowazoea ambao ndio chanzo cha mateso yako na mahangaiko yako

3. Nasema hivi!, chunga sana ndoto zako asizijue yeyote akujuae.
ndoto fafanua unamaana mipango.
 
Ninayoyapitia siwezi andika hapa, familia inaweza kuwa mwiba katika maisha ya mtu, shetani anaweza kutumia familia kwaajili ya kumtesa mtu. Mara nyingi tunaamini kuwa familia yako haiwei kuwa against na wewe kumbe si kweli, Ndo maana katika makafara mengi ya damu mhusika anatakiwa kutoa damu ya ndugu wa kuzaliwa au mtoto hata mjukuu ili kuweza kupanda ngazi fulani katika ulimwengu wa nguvu za giza, au kunamikataba ya giza mtu anaingia kwa kujua au pasi kujua kisha baadae anatakiwa kutoa kafara ya mtu wa uzao wake.

Kunawakati mtu inabidi kujitenga kabisa na aina fulani ya watu ili kuweza kuvungu vizuizi fulani, inapobidi hata familia ndugu na wazazi inatakiwa kujitenga nao. Lakini kutokana na maisha ya kiafrika tunaamini kuwa wazazi hawawezi kudhuru mtoto wao wa damu.
 
Hapo kwenye red ndio wengi wanapopotezwa.
Kwa mfano kama famili yenyewe ni mawakala wa shetani wewe unategemea nini? Shetani ni muongo siku zote hivo mkuu nakushauri UOKOKE haraka sana MUNGU ndio kimbilio lako. Plz usipoteze muda...
 
Hivi mkuu unafahamu pepo la utambuzi?
Chamsingi mkuu ni kumweka MUNGU awe mtegemezi wa maisha yako kwa kila jambo.
Ulimwengu wa kiroho ni mgumu sana kwa sababu shetani nae aliwahi kufanya kazi na MUNGU hivyo ana siri nyingi sana za MUNGU ila pamoja na yote hayo MUNGU atabaki kuwa MUNGU tuu.

Kwa nachoona mimi kinachowakwamisha watu ni kutokukomaa kiimani hivyo wanakua mara kwa MUNGU mara kwa shetani na hili ni kosa kubwa sana maanda maandiko yanasema usiabudu miungu bali wapaswa umwabudu MUNGU tuu...
 
Ofcourse familia zina mchango wake lakini ukiwa hodari kwenye eneo fulani mbona easy tu sema "wengi" wetu tunafeli kwenye vetting pale. Na ukute ndio uko mjeuri jeuri "unatupiwa tu' Extendend Vetting Process. Unasaga lami bila kujua..2 yrs imenitesa!
 
Back
Top Bottom