Wazungu gani hao'wale walioigawa sudan?nani kakuambia sisi waafrica tunaweza kuungana?
Mbona tanganyika na znz matatizo kibao tangu tulipoungana?je tukiingiza wakenya na watusi itakuwaje?
..Kwahio huo Wimbo ndio unakufanya u-conclude kwamba JK anaogopa EAC kwa sababu Wakristu watawafunika Waislamu, Mkuu hii sababu yako ni dhaifu, hoja iwe Tanzania itafaidikaje kiuchumi ndani ya EAC, umeuliza swali kwanini JK hakubaliki ndani ya EAC, jibu ni kuwa Nchi nyingine zinazounda EAC walidhani Tanzania tutaingia mkenge kirahisi katika kila matakwa ya Integration, sasa wanapoona tumeshtuka ndo wanaanza Unafiki.usiogope kujadili kila kitu kama unataka kufahamu ukweli halisi.............................kumbuka JK aliwakosoa EAC pale ule wimbo wa Kenya ulipochaguliwa kuwa wimbo rasmi wa Shirikisho akidai mbona ni "gospel"......................................wao walimjibu hawa ndiyo waliojitokeza hizo taarabu mbona hazikujitokeza??????????????????
hakuwa na majibu..............................................sasa wafikiri kwa nini aligusa suala la "gospel".........................udini ni urithi wetu na usipojadiliwa na jinsi unavyosukuma maamuzi ya kisera ujue hatutafahamu tupo wapi na kwa sababu zipi achilia mbali twaelekea wapi...................
Kwahili naweza kumtetea JK kwamba hakubaliki na hii ni kutokana na yanayoendela katika shirikisho, ikumbukweTanganyika inaonekana kama lulu miongoni mwa nchi za ukanda huu wa Afrika Mashariki, sasa kwa hayo yaliyojiri juzi kati wakati wa utiaji sign wa mkataba ambapo Tanganyika chini ya Samweli Sita waligoma mpaka baadhi ya vipengele vilipowekwa sawa umewakasirisha hawa jamaa!
walitegemea turuhusu ardhi yetu iwe yao, siasa na hata majeshi kitu ambacho kingetugharimu
Nimshukuru binafsi kwa mara ya kwanza JK kwa kutowapa vilaza hii wizara ya Afrika Mashariki maana naamini wangekuwa ni Malima,Kombani,Ngeleja, Nchimbi,Sofia simba, wamekamata hii wizara wangesign haraka haraka maana ni vihiyo watupu
Nakushauri ufikiri sana hatma ya nchi yako miaka ijayo kabla ya kumlaumu Jk na Sitta katika suala la EAC hasa masula ya ardhi. Kumbuka ni 2015 Jk atamaliza kipind4 chake. Ungependa mrithi wake na wanao na wajukuu wagombee ardhi ya Nchi yao wenyewe na wakenya?
Hapa kuna upungufu mkubwa wa reasoning. Tuliungana na Zanzibar, kutokana na mwungano huo leo Wazanzibari wanaweza kuchukua ardhi yoyote wanayoitaka ya Tanganyika LAKINI Watanganyika hawaruhusiwi kuichukua wala kuitumia ardhi ya Zanzibar. Leo hii tukiungana na nchi za Afrika Mashariki tutapoteza nini ambacho hatupotezi sasa hivi kwa Zanzibar? Si aheri hata huo mwungano wa Afrika Mashariki ambao, kila mwananchi wa Afrika Mashariki atakuwa na haki ya kutumia rasilimali zote za Afrika Mashariki kuliko sasa ambapo Wazanzibari wanaruhusiwa kutumia rasilimali za Tanganyika lakini Watanganyika hawaruhusiwi kutumia rasilimali za Zanzibar? Mpaka sasa Kenya ni mwekezaji wa pili baada ya Afrika Kusini, je, tumepoteza nini kutokana na uwekezaji wa Kenya? Si Wakenya hawa hawa walifunga kiwanda kimojawapo cha Tusker kule Kenya ili kukiimarisha cha Tanzania? Walifanya hivyo kwaajili ya kupata faida zaidi lakini na sisi tunapata ajira zaidi, na serikali inapata kodi zaidi.
Watanzania tusiwe na roho ya korosho. Huwezi kuendelea kwa kujitenga, unaendelea kwa kushindana. Nenda mikoa, wilaya au vijiji ambavyo zaidi hukaliwa na watu wa asili na kabila moja, halafu ulinganishe kiwango cha maendeleo na mikoa, wilaya au vijiji vyenye mchanganyiko mkubwa wa jamii. Waafrika Mashariki tukichanganyika zaidi, ndipo tutakapoweza kushindana, na kila mmoja kujifunza kutoka kwa mwingine. Hii mipaka iliwekwa na wakoloni, tunataka kurudi tulivyokuwa kabla ya wakoloni. Kama wakoloni wasingekuja, tungeanza kuwaambia watu wa maeneo fulani wasitumie ardhi ya maeneo mengine?
Kama JK angekuwa na upeo na nia ya kuwasaidia Watanzania angewaandaa Watanzania kwa kuwamilikisha ardhi ili wageni wakija wajadiliane na wamiliki wa ardhi. Leo mnawakatalia ardhi Wakenya wakati kule Mahenge Mwarabu kamilikishwa ardhi zaidi ya ekari laki moja; kule Kigoma, nadhani ni Wabrazili wamemilikishwa ardhi zaidi ya ekali laki moja, n.k. Au mnataka kusema ni halali wazungu na waarabu kumiliki ardhi ya Tanganyika lakini siyo weusi wa Kenya, Uganda, Rwanda au Burundi? Kosa lao ni nini - labda ni rangi.
Mkuu, Rejea mfano huu:kama hatuamini juu ya malengo ya EAC si tujitoe tu kulikoni kuwakwamisha wale wanaotaka kwenda mwendo mdundo.......
spot on.............

Mtoa mada angeeleza faida za kushirikiana Ardhi, na usalama i.e National security (siyo kusaidiana kwa idara za usalama au polisi).
Zaidi ya hapo ni mipayuko isiyo na maana. Tushirikiane kwenye biashara baina ya nchi zetu, zaidi ya hapo waondoke zao hatuwahitaji.
Mkuu Ruta, huyu hakubaliki ndani ya nchi yake iweje akubalike ndani ya EAC?
Hukuelewa mkuu alimaanisha nini "think globally act locally" kwa nchi ina maana kuwa iwe na uhusiano mzuri na mataifa mengine kwenye nyanja za biashara, technologia, elimu, masoko nk lakini ilinde interest zake kama nchi locally. Mfano ni UK na jumuia ya ulaya wao hawakuingia kwenye safaru ya pamoja (Euro) wakabaki na £ yao lakini wamo kwenye common european market. Wachina wameingizwa kwenye G20 na WTO lakini wamekataa baadhi ya masharti kama kushusha thamani ya pesa yao kwa sababu haina manufaa kwa wananchi wake. Tanzania ingekuwa ni kosa kubwa kuweka rehani adhi yake kwa manufaa ya wakenya, waganda, wanyarwanda nk watu ambao tunajua ni wakabila kupita kiasi. Sidhani kama kuna mtanzania anaweza kwenda kenya, uganda au Rwanda na kumilki ardhi. Mipaka hakikuletwa na wakoloni, babu zetu walikuwa nayo pia, wasukuma walijua mipaka yao, hali kadhalika wanyamwezi, wangoni, wahehe, wazanaki, wachaga, wapare nk wote walijua na kulinda maeneo yao na palikuwepo vita vya makabila vya kugombea ardhi. Mkoloni yeye alichofanya ni kuchora ramani bila kujali mipaka ya mababu zetu, jambo ambalo limechangia migogoro afrika
Re: Kwanini JK hakubaliki ndani ya EAC?Siungi mkono Afrika Mshariki kwa sababu Tanzania tutaishia kuwa losers Kenya wale wanataka ardhi na masoko dhidi ya bidhaa zao Burundi, Rwanda na Uganda wanataka ardhi je sisi tutapata nini? hakuna kitu ila kupoteza kila kitu
Wakati europen Union inaanzishwa na Ufaransa, Ubelgiji, Luxernburg, Ujerumani, na Uholanzi Uingereza ilizuiliwa kuwa iko too developed maana hizi nchi zingine viwanda vyake vilikuwa vimeharibiwa na vita kuu ya pili ya dunia Uingereza imekuja kuwa registerd mwaka 1977 nayo kwa kulipa kisasi ikakataa kudisolve pesa yake pia nchi zingine zimekuja baada ya kutimiza madharti na kuwa tayari.
Kwa muungano ule nchi za magharibi zinauza bidhaa nchi za mashariki kwahiyo zina soko hapo na nchi za mshariki zinatoa cheap labor wafanyakazi kwa lugha nyingine wananchi wa nchi za mashariki wanapata ajira nchi za magharibi kwahiyo mambo ni win win situation lakini kwetu sisi Tanzania kuna mtanzania anaweza pata kazi kenya? Kuna mtanzania anaweza pata ardhi Kenya? Je kuna bidhaa za Tanzania za viwandani zinaweza kuuzwa Kenya? ukiacha mazo ya chakula? kwanini tuwe na muungano ambao ni one way traffic? Hapo sijaongelea kuwa treated kama second citizen maana makenya ni mabaguzi kishenzi