Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Je tatizo ni nini? Sababu ni ipi hasa ya kumdharau Mwanamke kiasi hiki?? Hili utaliona kila mahali kwa mfano Mwanamke akibakwa hapa TanZania siku zote jamii hugawanyika, Wanaume wengi huona kwamba ni kosa la Mwanamke na huja na misemo kwamba amezidi naye huyo, msichana akipewa mimba jamii yetu hasa Wanaume isipokuwa labda baba wa Msichana husema ni kosa lake na kumlaumu Msichana kana kwamba ile mimba amejipa na huenda mbali zaidi hata kumsafisha kijana aliyempa mimba Msichana!
Kama ndoa ikivunjika jamii isipokuwa labda baba mwenye binti huona kwamba kosa ni la Mwanamke na haijalishi Mwanamke ameteswa na kuteseka vipi na Mume wake.
Mtoto asipoenda Shule wa kuadhibiwa na kulaumiwa ni Mwanamke ingawaje mtoto pia ana baba ambaye hushinda bar lkn yeye hakuna wa kumlaumu tena hapa Mwanamke hulaumiwa kwamba ni kosa lake kwamba mume wake anashinda bar kana kwamba Mwanaume ni mtoto mdogo ambaye anatakiwa kufanyiwa kila kitu!
Lakini kinachonishangaza sasa, Wanaume karibia wote wanapenda sana mama zao, sasa hapa shida iko wapi?? Iweje karibia kila kosa linalohusu jamii alaumiwe Mwanamke lkn mama zetu tunawatetea mpaka mwisho wa Dunia? Tofauti ya mama yako na Mke wa mtu xyz ni nini? Ni kwa nini Mwanamke awe mbaya akiwa Mke wako lkn awe mwema na Malaika akiwa mama yako??!
Ni kwanini Mwanamke analaumiwa karibia kwa kila jambo liendalo vibaya kwenye jamii yetu, hata ukiona Mwanaume kavaa nguo chafu analaumiwa Mke wake, Mwanaume akinuka na asipooga analaumiwa Mke wake kwamba ni kwa nini hamuangalii? Sasa kwani kazi ya Mwanamke na kumlea Mume wake ?
* Hata Mods wa JF hawajaona umuhimu wa hii Mada na wameihamishia kwenye Jukwa la mambo ya mapenzi! Huu ni ushahidi tosha kama kuna aliyekuwa anatafuta ushahidi, tuna safari ndefu sana!