Kwanini jamii inatudharau tulioacha shule?

Concord

Member
May 11, 2016
34
30
Wakuu,

Kwanza salamu ziwafikie,Mimi ni si mwenyeji humu JF nimekuwa nikitumia kama guest kwa muda kidogo.

Wakuu jambo linalonshangaza nimekuwa gumzo hapa mtaa kwetu baada ya kuamua kuachana na shule (secondary level) kwa kuwa sina mpango wa kuajiriwa na ni kama miaka sita au saba hadi kumaliza elimu yangu ukiangalia umri unaenda na nataka kuwa free na mishe zangu na skuli inabana sana muda.

So huku mtaa kila nikipita lecture hazishi mara oh utajutia, mara elimu haina mwisho n.k

Hivi wakuu kwanini hisia zetu zisiheshimiwe sisi tulioacha shule?
 
Elimu inamchango mkubwa sana hata katika maisha yako ya kila siku na si lazima uje kuajiriwa..Labda ukose hiyo fursa kwa bahati mbaya lakin kama kulikuwa na fursa ya kupiga book ukaacha tena katika ngazi ya Sekondary hata mimi nazidi kukushangaa kwa maamuzi hayo..
 
Wakuu kwanza salamu ziwafikie mimi ni si mwenyeji humu jf nimekuwa nkitumia kama guest kwa muda kidogo.Wakuu jambo linalonshangaza nimekuwa gumzo hapa mtaa kwetu baada ya kuamua kuachana na shule(secondarylevel) kwa kuwa cna mpango wa kuajiriwa na ni kama miaka sita au saba hadi kumaliza elimu yangu ukiangalia umri unaenda na nataka kuwa free na mishe zangu na ckuli inabana sana muda.So huku mtaa kila nnapita lecture hazishi mara oh utajutia,mara elimu haina mwisho nk,hivi wakuu kwa nn hisia zetu zisiheshimiwe sisi tulioacha shule?
Unajishughulisha na nini kwa sasa?
 
Elimu inamchango mkubwa sana hata katika maisha yako ya kila siku na si lazima uje kuajiriwa..Labda ukose hiyo fursa kwa bahati mbaya lakin kama kulikuwa na fursa ya kupiga book ukaacha tena katika ngazi ya Sekondary hata mimi nazidi kukushangaa kwa maamuzi hayo..
Mkuu asante kwa ushauri lakini najua kuna elimu tofauti na shule.
 
Mtu akiacha shule kibongobongo hapa olvl mi siamini mafanikio yyt juu yake hyo anajitaftia shida2 maana hata sklls ya kusoma kitabu na kukielewa atakua hana kwa hyo kijana nakushaur piga2 shule mwanang si wengn imetutoa japo sio sana ila tuna maisha yetu kifupi vijana tupende shule hakuna namna kwa Nchi zetu hz masikini
 
Wakuu,

Kwanza salamu ziwafikie,Mimi ni si mwenyeji humu JF nimekuwa nikitumia kama guest kwa muda kidogo.

Wakuu jambo linalonshangaza nimekuwa gumzo hapa mtaa kwetu baada ya kuamua kuachana na shule (secondary level) kwa kuwa sina mpango wa kuajiriwa na ni kama miaka sita au saba hadi kumaliza elimu yangu ukiangalia umri unaenda na nataka kuwa free na mishe zangu na skuli inabana sana muda.

So huku mtaa kila nikipita lecture hazishi mara oh utajutia, mara elimu haina mwisho n.k

Hivi wakuu kwanini hisia zetu zisiheshimiwe sisi tulioacha shule?
Hama mtaa! Ukienda mtaa mpya hakuna atakaye jua kuwa uliacha shule...
 
Kama mkuu alivyosema hapo juu. Kwa vile umeamua kufanya business, then hakuna shaka kuwa itakubidi utafute mbinu za kubobea katika hiyo kazi yako. Nasema hivyo ili ujipange vizuri uwe na business endelevu. Soma hivyo vitabu vya business, fuatilia watu waliofanikiwa katika biashara na usijaribu kufanya illegal business.
 
Mkuu ukitaka kujua umuhimu wa shule waulize matajiri ambao hawakusoma watakwambia, ila wanajuta sana kutokusoma na ndio wanaongoza kwa kuwa na uchungu juu ya elimu ya watoto wao.
 
Mkuu nlichofata shule nshakipata na nimeshafanya utafiti juu ya hasara na faida ndo nimeamua hivyo.
 
Kama mkuu alivyosema hapo juu. Kwa vile umeamua kufanya business, then hakuna shaka kuwa itakubidi utafute mbinu za kubobea katika hiyo kazi yako. Nasema hivyo ili ujipange vizuri uwe na business endelevu. Soma hivyo vitabu vya business, fuatilia watu waliofanikiwa katika biashara na usijaribu kufanya illegal business.
Mkuu kuhusu hilo ucjali japo nmeacha shule ila sijaacha kutafuta elimu zaidi
 
Back
Top Bottom