Kwanini ITV mmetuletea ripota mtoto Richard Steven

Umri siyo tatizo, muajiriwa mmojawapo hapo, japo sijamsikia siku nyingi, kwa jina la Aboubakary Sadick, kama mtakumbuka aliajiriwa akiwa hata hajafikisha miaka 20 hapo Radio One, ila leo kawa mkongwe tayari na anakaribia kufikisha miaka 20 kama bado yupo hapo.

Hivyo, kwa wenye vipaji, wapewe nafasi, na changamoto wanazopewa Tv husika, wazifanyie kazi.

Ahsante!
 
Kama mtu ana kipaji hatakiwi kusoma sana
Kusoma kunalemaza vipaji
Hivi leo Messi angekaa darasani ingekuwaje
 
Richard Steven sio mtoto ni mtu mzima now ana miaka 21 then nimemaliza nae diploma ya uhandishi wa habari mwezi WA 12 mwaka jana chuo cha DsJ yaani Dar es salaam School of Journalism kiko ilala Sharifu Shamba kwenye jengo LA Basata

xomen wachen uvivu xx n hivo vidiploma vyen mtaendelea kubebwa na kupewa ujira mbuzi!
piga kitabu ww!
 
kila mtu ana ndoto katika kufika mbali katika shuguli afanyazi, ukwel ni kua dogo angeenda kusoma tu kwanza akamaliza maana kipaji hakifi. vitu 2 kwa wakti 1 lazima kimoja kiwe chini, ukiwa MWEUSI bbc, cnn, cctv, n.k hawaangalii kipaji ila vyeti sidhan kama akiletwa ofa ya majuu atakataa et kisa ITV
 
Watanzania hatutaki kuwa na standards
Hilo ndio tatizo letu kama taifa, hatutaki kukosolewa wala hatutaki kukubali kuwa uwezo wetu ni mdogo na tunahitaji kujiongeza. Huwezi kuleta mchezo kwenye kitu muhimu kama news, ndio maana siku zote kwenye tv za kimataifa huwezi kukutana na mijadala kama hii, kwa nini ITV haitaki kujifunza ndio maana imeishia kuwa hivyo ilivyo, haina ubora wowote na hizo super brand wanazopeana tunajua kuwa wanalipia dola 5000 ni mradi wa kawaida tu, ITV imeshindwa ku retain watu wenye uzoefu na kuendelea kuwa chombo kichanga kwa ajil ya hicho kiburi, watu tunaenda huko kuangalia news tu dakika 8 hazifiki tumeshahama channel, je wao hawalijui hilo? ni kwa kuwa wanapata matangazo ya kampuni kubwa chache wanajiona wako sawa, ni kweli kuwa tunawapapatikia kwa kuwa hakukuna mwingine lakini sio kwa kuwa ni the best. 'we are in the land of the blind where a one man eyed is a king' wote tunajua kuwa ITV hawatoi mafunzo yoyote si ya academic wala practical kwamba kuna senior wanao mentor vijana, katika TV inayotakiwa kuwa serious kila kituko kinatoka hapo, mahojiano gani ambapo host anageuzwa kuwa interogated, ndio maana mpaka leo hii so many years have passed wameshindwa kuwa na kipindi hata kimoja, kinachoitwa 'popular', tazama kile kipindi cha dakika 45 kilitakiwa kiwe ni kipindi moto kwa mijadala ya policy na good governance, vijana wanaokiendesha hawajajiongeza, wanaishia kuuliza maswali yale yale ya quality ya muandishi mpita njia, hakuna taarifa yoyote wala sera yoyote iliyojadiliwa serious tukaondoka tuki ki quote kipindi chochote cha ITV zaidi ya news.

Watanzania hatutaki kuambiana ukweli
Tuwaambie ukweli tuwasaidie, tazama kwa nini watangazaji wakitoka hapo wanakoenda wana shine? Joyce anajitamba kuwa aliwatengeneza yeye, si kweli kama ndio uliowatengeneza kwa nini hivyo viwango hatukuviona hapo? Kama ni kweli kwa nini wakina Salim Kikyeye, Fauziyat Abou, Charles Hilali etc hata wanapokua likizo hapa hawana hamu ya kutia mguu kwa boss aliyewatengeneza " if it true' kushow off? kina Regina Mwaleko, Millard Ayo, Kitenge, kuna shida sana hapo ITV hata taarifa za uchaguzi tuliona walivyokua vituko, jamani kama walaji hatutajua tunachokitaka tutalishwa mavi tukisifia chakula kitamu. Si malumbano ya hoja wala, kipima joto kinachokidhi haja zetu, vipindi motomoto vyote vinatoka nje na haviendelei kwa sababu ya majungu na wivu wa ITV, wapi "The Tanzania We Want' mbona hakikuwepo wakati wa uchaguzi watu tulikua tunakizunguka kama tunaangalia mpira wa Arsenal,

Television kuendeshwa kizamani sana
Noamba niulize swali, hivi hapa Jf kuna mtu yoyote anayeweza kudai kuwa anaangaliaga local TV? yaani unatoka huko unafika nyumbani unachukua remote kuangalia nini kinachoendelea ukitegemea kuvutwa? wote tunafungua kwa kuangali news mostly, wakati mwingine tutabaki kwenye dishes vikiwemo vin'gamuzi. Sitashangaa kama hawa ITV hata baada ya comments hizi hawatafanyia kazi swala la huyo mtangazaji kwa kuwa watakubaliana na comfort waliyopewa na watu wachache, waliokashifu hoja. hakuna research hakuna surveys za kutuhoji kupata maoni yetu kama walaji, survey zao ni zile wanazolipia ili waingizwe kwenye u super brand. watajiongezaje? ahueni yetu leo ni uwepo wa Clouds Tv tena kwenye dishi la DSTV, it is a great opportunity i believe kama watakua waangalifu they will very soon kick out ITV, watabaki na waangalizi wa news ambazo hazihitaji utaalamu wowote bali kuwa na resources za kuwepo zanzibar na mara kwa George Marato.

Ume panic mkuu, ITV itabaki kuwa super brand kwanza kuilinganisha na Clouds TV unakosea sana, Clouds TV waweke na EATV, habari zinazotolewa na ITV ni very reliable siyo kama za Star TV, TBC
 
Mbona ni wa muda mrefu uyo kijana?? Ninamfahamu takribani mwaka wa pili sasa..
Na mara nyingi anakuwa mtaani akifuta habari...
Pia unakumbuka umri alioanza Milard ayo kusoma taharifa ya habari ya ITV?
Na uyo kijana unajua ana umri gani?
 
Sawa mimi mtoto kwa kuwa wewe unanilisha na kunipa malazi.
Ile ni kazi kama kazi nyingine,mbona kuna wachezaji nyota na wana umri mdogo,kwa nini uhoji kwake tu?
Hata kama ameacha shule na kuamua kufanya kazi,hiyo ni juu yake na familia yako,wewe fuata yako na huko unakopata mshahara mkubwa kuliko anayotoa Mengi!!!

We pia kumbe ni mtoto,nimuonee wivu kwa lipi fani yangu na yake vitu vinne tofauti,eti aache niende mimi we akili zako zime expire kwa mishahara gani ya meng?
 
Watanzania hatutaki kuwa na standards
Hilo ndio tatizo letu kama taifa, hatutaki kukosolewa wala hatutaki kukubali kuwa uwezo wetu ni mdogo na tunahitaji kujiongeza. Huwezi kuleta mchezo kwenye kitu muhimu kama news, ndio maana siku zote kwenye tv za kimataifa huwezi kukutana na mijadala kama hii, kwa nini ITV haitaki kujifunza ndio maana imeishia kuwa hivyo ilivyo, haina ubora wowote na hizo super brand wanazopeana tunajua kuwa wanalipia dola 5000 ni mradi wa kawaida tu, ITV imeshindwa ku retain watu wenye uzoefu na kuendelea kuwa chombo kichanga kwa ajil ya hicho kiburi, watu tunaenda huko kuangalia news tu dakika 8 hazifiki tumeshahama channel, je wao hawalijui hilo? ni kwa kuwa wanapata matangazo ya kampuni kubwa chache wanajiona wako sawa, ni kweli kuwa tunawapapatikia kwa kuwa hakukuna mwingine lakini sio kwa kuwa ni the best. 'we are in the land of the blind where a one man eyed is a king' wote tunajua kuwa ITV hawatoi mafunzo yoyote si ya academic wala practical kwamba kuna senior wanao mentor vijana, katika TV inayotakiwa kuwa serious kila kituko kinatoka hapo, mahojiano gani ambapo host anageuzwa kuwa interogated, ndio maana mpaka leo hii so many years have passed wameshindwa kuwa na kipindi hata kimoja, kinachoitwa 'popular', tazama kile kipindi cha dakika 45 kilitakiwa kiwe ni kipindi moto kwa mijadala ya policy na good governance, vijana wanaokiendesha hawajajiongeza, wanaishia kuuliza maswali yale yale ya quality ya muandishi mpita njia, hakuna taarifa yoyote wala sera yoyote iliyojadiliwa serious tukaondoka tuki ki quote kipindi chochote cha ITV zaidi ya news.

Watanzania hatutaki kuambiana ukweli
Tuwaambie ukweli tuwasaidie, tazama kwa nini watangazaji wakitoka hapo wanakoenda wana shine? Joyce anajitamba kuwa aliwatengeneza yeye, si kweli kama ndio uliowatengeneza kwa nini hivyo viwango hatukuviona hapo? Kama ni kweli kwa nini wakina Salim Kikyeye, Fauziyat Abou, Charles Hilali etc hata wanapokua likizo hapa hawana hamu ya kutia mguu kwa boss aliyewatengeneza " if it true' kushow off? kina Regina Mwaleko, Millard Ayo, Kitenge, kuna shida sana hapo ITV hata taarifa za uchaguzi tuliona walivyokua vituko, jamani kama walaji hatutajua tunachokitaka tutalishwa mavi tukisifia chakula kitamu. Si malumbano ya hoja wala, kipima joto kinachokidhi haja zetu, vipindi motomoto vyote vinatoka nje na haviendelei kwa sababu ya majungu na wivu wa ITV, wapi "The Tanzania We Want' mbona hakikuwepo wakati wa uchaguzi watu tulikua tunakizunguka kama tunaangalia mpira wa Arsenal,

Television kuendeshwa kizamani sana
Noamba niulize swali, hivi hapa Jf kuna mtu yoyote anayeweza kudai kuwa anaangaliaga local TV? yaani unatoka huko unafika nyumbani unachukua remote kuangalia nini kinachoendelea ukitegemea kuvutwa? wote tunafungua kwa kuangali news mostly, wakati mwingine tutabaki kwenye dishes vikiwemo vin'gamuzi. Sitashangaa kama hawa ITV hata baada ya comments hizi hawatafanyia kazi swala la huyo mtangazaji kwa kuwa watakubaliana na comfort waliyopewa na watu wachache, waliokashifu hoja. hakuna research hakuna surveys za kutuhoji kupata maoni yetu kama walaji, survey zao ni zile wanazolipia ili waingizwe kwenye u super brand. watajiongezaje? ahueni yetu leo ni uwepo wa Clouds Tv tena kwenye dishi la DSTV, it is a great opportunity i believe kama watakua waangalifu they will very soon kick out ITV, watabaki na waangalizi wa news ambazo hazihitaji utaalamu wowote bali kuwa na resources za kuwepo zanzibar na mara kwa George Marato.
We kiongozi umemaliza siongezi hata nukta,kuna watu wa hovyo sana kudhani kukosoa ni chuki.
 
Jaman uyo Richard steven nimesoma nae diploma ya uandishi wa habari katika chuo cha Dar esp salaam school of journalism(dsj) kilichopo buguruni malapa kamaliza mwaka jana mwezi wa 12 sahiv nahis atakua kwenye process za kujiunga na university . ila aliwahi kunichukulia demu wangu kwasababu alikua maarufu sana kwa kweli kile chuo kipo vizuri kwa waandishi Wa habari
teh teh teh we unaleta utani kwenye ishu serious
 
Mtoto kaajiriwa ww miaka bdo inasepa bado unasungua benji! Marekani mtoto akisha fikisha miaka 18 anatimuliwa nyumbani kujitengemea! Kipaji cha mtu huanzia akiwa na umri mdogo hapo hamna cha kupoteza
Pitia upya ulicho coment
 
Richard Steven sio mtoto ni mtu mzima now ana miaka 21 then nimemaliza nae diploma ya uhandishi wa habari mwezi WA 12 mwaka jana chuo cha DsJ yaani Dar es salaam School of Journalism kiko ilala Sharifu Shamba kwenye jengo LA Basata
Na wewe umemaliza course gani? Maana kama na wewe ni mwandishi wa habari basi ni shida..UHANDISHI WA HABARI......chuo KIKO ilala..labda kwa sababu chuo chenyewe ndo cha huko SHAMBA..
 
Kwanza sina uhakika kama katimiza kisheria umri wa kuajiriwa(mtanisaidia hapa)lakini nakumbuka huyu mtoto alikua mwanafunzi sielewi ni lini kamaliza shule/chuo na kuanza kazi,nimekua nikikaona kana report mambo ya kipindi cha kipima joto ila siku zinavyozidi kwenda nazidi kumuona anareport vitu vikubwa(mahojiano)

kama mnavyojua mtoto ni mtoto yaani uwezo wa kazi aliyopewa hana
Ushauri-kama mmeamua itv kumuajiri huyu mtoto ni vema akaanza na vipindi vidogovidogo/kawaida hasa vya watoto mpaka akue kifikra na kimwili kwanza.
sasa unataka akacheze pool ama nn si anaendelea kukua atakomaa tu
 
Kwanza sina uhakika kama katimiza kisheria umri wa kuajiriwa(mtanisaidia hapa)lakini nakumbuka huyu mtoto alikua mwanafunzi sielewi ni lini kamaliza shule/chuo na kuanza kazi,nimekua nikikaona kana report mambo ya kipindi cha kipima joto ila siku zinavyozidi kwenda nazidi kumuona anareport vitu vikubwa(mahojiano)

kama mnavyojua mtoto ni mtoto yaani uwezo wa kazi aliyopewa hana
Ushauri-kama mmeamua itv kumuajiri huyu mtoto ni vema akaanza na vipindi vidogovidogo/kawaida hasa vya watoto mpaka akue kifikra na kimwili kwanza.
Sijaona Tatizo lake, labda tueleze mapungufu yake na umegunduaje kuwa ni mtoto? miaka ishirini watu wanagraduate
 
Huwezi kuchukua saidia fundi akawa fundi mkuu halafu unampa majukumu ya fundi mkuu,huko ni kuharibu kazi za watu,labda kama watazamaji tumeanza kuzarauriwa sasa,habari muhimu na nyeti zinaripotiwa na katoto ka miaka 16
 
DUU, kumbe napitwa na vingi, nina kama week tatu sasa sijaangalia taarifa za habari za tv za kibongo.
 
Back
Top Bottom