Kwanini ITV mmetuletea ripota mtoto Richard Steven

Kwanini ITV mmetuletea ripota mtoto Richard Steven

Mtoto? Kwa maana ana umri wa chini ya miaka 18?
 
Watanzania hatutaki kuwa na standards
Hilo ndio tatizo letu kama taifa, hatutaki kukosolewa wala hatutaki kukubali kuwa uwezo wetu ni mdogo na tunahitaji kujiongeza. Huwezi kuleta mchezo kwenye kitu muhimu kama news, ndio maana siku zote kwenye tv za kimataifa huwezi kukutana na mijadala kama hii, kwa nini ITV haitaki kujifunza ndio maana imeishia kuwa hivyo ilivyo, haina ubora wowote na hizo super brand wanazopeana tunajua kuwa wanalipia dola 5000 ni mradi wa kawaida tu, ITV imeshindwa ku retain watu wenye uzoefu na kuendelea kuwa chombo kichanga kwa ajil ya hicho kiburi, watu tunaenda huko kuangalia news tu dakika 8 hazifiki tumeshahama channel, je wao hawalijui hilo? ni kwa kuwa wanapata matangazo ya kampuni kubwa chache wanajiona wako sawa, ni kweli kuwa tunawapapatikia kwa kuwa hakukuna mwingine lakini sio kwa kuwa ni the best. 'we are in the land of the blind where a one man eyed is a king' wote tunajua kuwa ITV hawatoi mafunzo yoyote si ya academic wala practical kwamba kuna senior wanao mentor vijana, katika TV inayotakiwa kuwa serious kila kituko kinatoka hapo, mahojiano gani ambapo host anageuzwa kuwa interogated, ndio maana mpaka leo hii so many years have passed wameshindwa kuwa na kipindi hata kimoja, kinachoitwa 'popular', tazama kile kipindi cha dakika 45 kilitakiwa kiwe ni kipindi moto kwa mijadala ya policy na good governance, vijana wanaokiendesha hawajajiongeza, wanaishia kuuliza maswali yale yale ya quality ya muandishi mpita njia, hakuna taarifa yoyote wala sera yoyote iliyojadiliwa serious tukaondoka tuki ki quote kipindi chochote cha ITV zaidi ya news.

Watanzania hatutaki kuambiana ukweli
Tuwaambie ukweli tuwasaidie, tazama kwa nini watangazaji wakitoka hapo wanakoenda wana shine? Joyce anajitamba kuwa aliwatengeneza yeye, si kweli kama ndio uliowatengeneza kwa nini hivyo viwango hatukuviona hapo? Kama ni kweli kwa nini wakina Salim Kikyeye, Fauziyat Abou, Charles Hilali etc hata wanapokua likizo hapa hawana hamu ya kutia mguu kwa boss aliyewatengeneza " if it true' kushow off? kina Regina Mwaleko, Millard Ayo, Kitenge, kuna shida sana hapo ITV hata taarifa za uchaguzi tuliona walivyokua vituko, jamani kama walaji hatutajua tunachokitaka tutalishwa mavi tukisifia chakula kitamu. Si malumbano ya hoja wala, kipima joto kinachokidhi haja zetu, vipindi motomoto vyote vinatoka nje na haviendelei kwa sababu ya majungu na wivu wa ITV, wapi "The Tanzania We Want' mbona hakikuwepo wakati wa uchaguzi watu tulikua tunakizunguka kama tunaangalia mpira wa Arsenal,

Television kuendeshwa kizamani sana
Noamba niulize swali, hivi hapa Jf kuna mtu yoyote anayeweza kudai kuwa anaangaliaga local TV? yaani unatoka huko unafika nyumbani unachukua remote kuangalia nini kinachoendelea ukitegemea kuvutwa? wote tunafungua kwa kuangali news mostly, wakati mwingine tutabaki kwenye dishes vikiwemo vin'gamuzi. Sitashangaa kama hawa ITV hata baada ya comments hizi hawatafanyia kazi swala la huyo mtangazaji kwa kuwa watakubaliana na comfort waliyopewa na watu wachache, waliokashifu hoja. hakuna research hakuna surveys za kutuhoji kupata maoni yetu kama walaji, survey zao ni zile wanazolipia ili waingizwe kwenye u super brand. watajiongezaje? ahueni yetu leo ni uwepo wa Clouds Tv tena kwenye dishi la DSTV, it is a great opportunity i believe kama watakua waangalifu they will very soon kick out ITV, watabaki na waangalizi wa news ambazo hazihitaji utaalamu wowote bali kuwa na resources za kuwepo zanzibar na mara kwa George Marato.

Umezunguka weeeee mwisho wa siku we ni Ruge wa clouds media
 
Ume panic mkuu, ITV itabaki kuwa super brand kwanza kuilinganisha na Clouds TV unakosea sana, Clouds TV waweke na EATV, habari zinazotolewa na ITV ni very reliable siyo kama za Star TV, TBC

Mwambie huyo Azam wenyewe wamejaza watangazaji wakongwe kama Barcelona lakini habari yao anaangalia Bakhresa na familia yake
 
Mwambie huyo Azam wenyewe wamejaza watangazaji wakongwe kama Barcelona lakini habari yao anaangalia Bakhresa na familia yake
Yaani wewe kua mfuatiliaji wa habari za i.t.v unajiona mjanja,we ndezi kweli yaani i.t.v pamoja na ukongwe wake wa miaka lukuki imebadili picha za mdundo tu pale ambapo habari inataka kuanza,usifananishe na azam japo wanamapungufu but muda utakuja kuongea.
 
Yaani wewe kua mfuatiliaji wa habari za i.t.v unajiona mjanja,we ndezi kweli yaani i.t.v pamoja na ukongwe wake wa miaka lukuki imebadili picha za mdundo tu pale ambapo habari inataka kuanza,usifananishe na azam japo wanamapungufu but muda utakuja kuongea.

ungenifahamisha bila kuniita ndezi nisingekuelewa?
ujumbe wangu hapo ni kwamba ni kweli Azam wamewekeza sana katika studio na rasilimali watu wa habari lakini tatizo linakuja lilelile hawana tofauti na hao ITV unaowaona hawana mabadiliko japo studio za zamani lakini bado watu wanaamini habari ya ITV kuliko vituo vingine kwa nini ? je nini Azam wanamis katika habari zao hadi wasipate watazamaji wengi?
 
Sina fujo BD...
Najua Diploma ya Uhandisi wa..., au Diploma ya Uandishi wa Habari🙂
Hahahah

Sasa ndio ujue kuna diploma ya uhandishi wa habari........

Sasa huyu akiwa ndio mwandishi au mhariri tutegemee "r" badala ya" l " na "h" za kutosha
 
Mtoto kaajiriwa ww miaka bdo inasepa bado unasungua benji! Marekani mtoto akisha fikisha miaka 18 anatimuliwa nyumbani kujitengemea! Kipaji cha mtu huanzia akiwa na umri mdogo hapo hamna cha kupoteza
Marekani ya wapi?
 
Meng kama ni muelewa hiki kitoto akipeleke kwenye vipindi vyake vya shule,hawezi kuhoji mtu wala kuripot jambo kiufasaha,
 
Huyu mtoto juzi juzi tu alikuwa akitangaza vipindi vya watoto na watoto wenzake, but jana nimemwona anasoma habari safi kabisa! Maisha yaenda kasi sana.
 
mijitu mingine sijui ikoje,halafu inalalamika ajira hakuna
 
Back
Top Bottom