Kwanini ikulu walitumia yahoo - mawazo yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini ikulu walitumia yahoo - mawazo yangu

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Sep 18, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Sep 18, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  KWA NINI IKULU WALIAMUA KUTUMIA YAHOO

  Pamoja na kwamba nilikosoa uamuzi wa ikulu ya tanzania kutumia barua pepe ya yahoo kwa ajili ya kuwasiliana na wananchi , nimekaa tena na kufikia mara nyingi zaidi kuona ni kwanini wao waliamua kufanya hivyo , ikulu ni sehemu nyeti sana lazima iwe na wataalamu waliobobea kwenye mawasiliano yao hawawezi kukurupuka tu na maamuzi ,lazima watakuwa wamejadiliana na kuona kile wanachotaka kufanya kwa muda mfupi .

  Kama mnakumbuka wiki moja kabla ya tangazo la ikulu kulikuwa kuna mambo yanaendelea kwenye ulingo wa siasa nchini haswa uchaguzi wa chadema , chadema walifanikiwa sana kuteka mitandao mbali mbali na majukwaa mbali mbali hata kwenye magazeti kutokana na uchaguzi huo , mambo ya zitto kutaka kupambana na mbowe na mengine mengi sana siwezi kutaja .

  Mwishowe chadema waliamua sasa kuanzisha utaratibu wa kukusanya michango yao kupitia simu za mikono hii ni njia nzuri nawapongeza lakini wajue kwamba nchi yetu kwa sasa hakuna sheria za kudhibiti mambo mengi yanayohusu mitandao pia simu zinasajiliwa kwahiyo huko mbeleni inaweza kuwa mbaya sana kwa wanaharakati wao haswa kipindi cha uchaguzi .

  Inawezekana kabisa kwamba chadema walifanikiwa kuteka anga ya tanzania kwa kiasi kikubwa kila mtu macho yalikuwa huko , ndio ikulu ikaja na mbinu hii , kama wao wanatumia mitandao na majukwaa mengine nasi tunakuja na hii kuwasiliana na wananchi moja kwa moja kuanzia live kwenye tv mpaka kwenye mitandao ya internet .

  Pia kuna kitu kingine walipotumia yahoo labda walimaanisha kokote mtu alipo kama anaweza kutumia ( IM ) instant Messenger kama yahoo , trillian na msn wanaweza kuingiza anuani ile ya yahoo kwenye contact list yao wawe wanaweza kuchat moja kwa moja na raisi kwa wakati huo pamoja na siku nyingine kwa kutumia hiyo hiyo na ni kitu cha kweli ni watu wengi sana wanaweza kutumia hizi messenger kwa ajili ya mawasiliano ya hapo kwa hapo .

  Lingine inawezekana walitumia yahoo kama tanganya toto kumbe barua zote zilizoingia yahoo zilikuwa zinapelekwa katika email nyingine yaani email forwading , hii inaweza kusaidia sana kuhifadhi maswali kwa ajili ya utafiti huko mbeleni na kujua wale wote waliouliza maswali hayo , kwahiyo inawezekana waliona jambo hilo mapema .

  Kuna kitu kinaitwa spam , hizi anuani za yahoo , hotmail na gmail zinaweza kufilter spam vizuri na kwa umakini zaidi kuliko hizi zingine za kawaida kwa kuwa yalikuwa ni maswali ya moja kwa moja inawezekana mpinzani akaamua kutuma spams kwa wingi ili kuvuruga mambo ukiwa na hizi barua pepe za kawaida maofisini kwetu ni hatari sana .

  Mwisho napenda kutoa wito kwa Ikulu kuweka namba ambazo kupiga ni bure ili kila mwananchi aweze kupiga anavyotaka , kuna wengine huko walipo hawana uwezo hata wa kununua vocha za simu kutokana na hali zao kukiwa na huduma za bure basi wengi zaidi watawasiliana na raisi pamoja na kuchangia mawazo yao .

  Bila kusahau kuanzisha sehemu yao katika mtandao wa www.youtube.com kwa ajili ya kuweka video zote zinazomhusu raisi kwa ajili ya ummah wale wanaotaka kudownload na kutumia kwenye shuguli zingine , hata juzi ile wale waliombali wangeweza kumwona raisi kutumia youtube na kuuliza maswali .

  Ingawa kumekuwa na makosa ya hapa na pale naamini sasa ikulu pamoja na wadau wengine watakaa vizuri wajipange kwa ajili ya kuamua kuja na aina nzuri zaidi ya mawasiliano isiyokuwa na usumbufu na iliyobeba uasilia wetu kabisa .

  Haya ni mawazo yangu tu , Karibuni tuendee kujenga nchi www.wanabidii.net , www.naombakazi.com
   
 2. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  This must be MARO of WANABII....you sound like him!
   
 3. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Nayaunga mkono hayo niliyowekea wekundu. Hata hivyo email redirect siyo njia madhubuti ya kujikinga na spam au madudu mengine mtandaoni. Wala siyo njia mbadala ya kuwasiliana na wananchi. Wanafungu la kushughulikia mambo haya, hela hizo sijui zinatumika vipi... (kukwepakwepa maswali, au?)...
  Naona watakuwa wamewasiliana nawe kwa karibu kuwapatia ushauri baada ya kuwa umeyasema yafuatayo:

  Na...hapa ambapo uliwashushua kikwelikweli:

   
 4. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  The Great SHY nadhani with "both the contradicting posts" haukutuma email kuuliza swali kwa Rais?
   
Loading...