Kwanini huandiki mambo unayofanya?

Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,025
6,593
Umeenda shule ya msingi, umejifunza kusoma, kuandika na hesabu, ukaenda sekondari ukapewa maarifa mengine yawe ya sayansi, sanaa, biashara n.k

Umeingia mtaani unafanya mambo yako mengi tu lakini uloyafanya mwaka jana / mwezi jana / wiki jana / jana huna kumbukumbu nayo kwa sababu huandiki. Ulijifunza ili iweje?
Kwa nini huandiki?

Kama yaliyopita huyakumbuki, unayoyafanya leo hayawezi kueleweka na utakayoyafanya kesho huna mpango nayo!

Mada inaonekana rahisi lakini kiuhalisia ni ngumu kujibu au kuchangia. Ugumu wa kuchangia ni pale inapoonyesha udhaifu wa mchangiaji au watu wake wa karibu mno.Na kama jadi yetu ilivyo hatutaki ya hovyo yanayotuhusu wachangie.Kwa kuwa ina tija kubwa nitajibu inayonihusu.Siandiki kwa sababu nina chembechembe za uzembe.Kutoandika kwa anayejua kuandika ni uzembe.Kutoandika ninayoyafanya kila siku na ninayotarajia kuyafanya baadaye yamenigharimu mno.

Kwa kutoandika ninayoyafanya kila siku nimeshindwa kufuatilai mipango niliyoipanga siku nyingi na kutoikamilisha,kuanzisha vitu vipya kabla ya kumalizia niliyoyaanza,kutotathmini niliyoyatekeleza,kukosesha nafasi kwa walio nyuma yangu kujifunza ninachochafanya,kasoro zangu na nguvu zangu.

Ahsante kwa kunikumbusha nitaanza kuvunja mwiko wa 'huwezi kumfundisha mbwa mzee mbinu mpya.'
 
Hapo kwenye bold nimecheka sana!
Wabongo wengi wapo hapo! Kuna nguvu kubwa na ya ajabu kwenye kuandika .... na yale uloyaandika ndo yamenisukuma kuuliza wana Jf ni kwa nini hawaandiki?

Kinachoendelea hata kwenye taifa letu ni kwa sababu hatuna dira ya kitaifa iliyoko kwenye maandishi.
 
Ndo maana tunafanya mambo/kazi kwa mazoea mkuu hatubadili mbinu maana tulichokifanya jana hatukikiandika na tutakachokifanya kesho hatukijui
 
Sasa tubadilike,
Andika mambo ya kufanya kwa siku ...
Ikifika jioni pitia ni mambo gani umefanikiwa kuyafanya na ni mambo gani yameshindikana kufanyika. Yale yaliyoshindikana andika ni sababu zipi zimekufanya ushindwe.
Utaratibu huu ni mzuri sana, utasaidia kujitathmini kwa vipindi vifupi vifupi.
 
Kila mwaka huwa nanunua diary kwa ajili ya kuandika....hadi December inakuwa blank!
Ngoja nijaribu mwaka huu!
 
kila siku napostpone kua na ki journal changu,hata nikiwa nacho SIANDIKI..hata nikishika kalamu ili niandike siandiki kama navotaka niandike
 
Ebu nikuwekee sample ya karatasi moja toka kwenye kijidaftrari ninachotumia badala ya Diary. ...
 
Sasa tubadilike,
Andika mambo ya kufanya kwa siku ...
Ikifika jioni pitia ni mambo gani umefanikiwa kuyafanya na ni mambo gani yameshindikana kufanyika. Yale yaliyoshindikana andika ni sababu zipi zimekufanya ushindwe.
Utaratibu huu ni mzuri sana, utasaidia kujitathmini kwa vipindi vifupi vifupi.
Kweli kabisa mkuu.....mm nimeandaa na kuandika mpango wa miaka mitano, nikaweka katika mwaka mmoja mmoja, nikaweka katika miezi, nikaweka kwa kila siku natakiwa kufanya nn na ikifika usiku kabla ya kulala naweka nn cha kufanya kesho yake na kuangalia kama nilichokipanga siku husika kimefanikiwa kama hakijanikiwa naandika sababu kwann sijafanikisha
 
kila siku napostpone kua na ki journal changu,hata nikiwa nacho SIANDIKI..hata nikishika kalamu ili niandike siandiki kama navotaka niandike
Kinachokuzuia kuandika nini nini? Itapendeza nikijua sababu ....
Nimejiandalia vijitabu 12, kila mwezi lazima kimoja kiishe ..
upload_2017-2-14_12-6-47.jpeg
 
Kweli kabisa mkuu.....mm nimeandaa na kuandika mpango wa miaka mitano, nikaweka katika mwaka mmoja mmoja, nikaweka katika miezi, nikaweka kwa kila siku natakiwa kufanya nn na ikifika usiku kabla ya kulala naweka nn cha kufanya kesho yake na kuangalia kama nilichokipanga siku husika kimefanikiwa kama hakijanikiwa naandika sababu kwann sijafanikisha
Ongera sana! na nina uhakika utaona matokeo chanya kwenye mipango yako!
 
Ahsante sana mkuu......umekumbushia jambo muhim sana kwa anaetaka kufanikiwa afuate ushauri wako huu.

Ataepukana na mengi hata mambo kununua vitu au kufanya vitu ambavyo viko nje ya bajet au mipango yanaepukika
 
Ahsante kwa kulijua hilo!
 
Back
Top Bottom