Kwanini hizi mila za kutembea na silaha (wamasai na wakurya) zisiwe halali maporini na sio mijini?

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,596
15,392
Makabila haya mawili licha ya uzuri wao huws yanakitu kinaitwa Mori. Ukiwachokoza nje ya uvumilivu wao wanapanda mori wanakuwa kama wanyama. Akili zinakuwa hazipo anafanya chochote.

Kwa bahati mbaya licha ya kuwa na sifa hii hatarishi ambayo makabira mengine mengi hayana bado ndio wanaoongoza kutembea na mikuki na sime katika maeneo yenye watu wengi. Kwa wakurya ukienda miji midogomidogo Tarime ni kawaida kukuta jamaa anapanga bila sababu yoyote. Na bahati mbaya wanasauti ya upole hivyo huwezi kujua umemkasirisha saa ngapi hasira za kumfanya atumie kisu, panga.

Nashauri, na na ungana na wazanzibari kwa dunia ya sasa mila ya kutembea na visu ikatazwe mijini. Kama wanatumia kwa ulinzi, zifunguliwe Ghala za silaha za jadi mijini. Wanazikabizi, wanauza dawa wakitaka kuingia lindoni wanazichukua.

Ni hayo tu.
Tatizo langu ni ule mori unasababishwa na vichuri na vinywaji mbalimbali vya jadi.
 
Unawazungumziaje wanaotembea na bastola . Au kwa kuwa silaha za wamasai zinaonekana.
Wale wanazo kisheria zinazowaongoza sio kitamaduni au mori.
Labda wawekewe sheria za matumizi ya silaha za jadi mijini.
 
Huwezi amini masai hadi akukande basi uvumilivu umemshinda ila ni watu wenye uvumilivu sana mpaka atoe ile fimbo au sime we umefika nae mbali hata wa kurya pia.
 
Mispalcement tu, hizo zilikuwa kwa ajili ya kujihami porini huko wanakofugia wanyama wao.
Sasa mjini, rungu, sime, na fimbo ni ya nini? Savage!
 
Mkurya kutembea na silaha unakuta ni wale wakorofi tu wapenda ugomvi na ujinga mwingi kichwani mwao, ila wamasai naona wanawaonea kuwakatalia kutembea na silaha zao za jadi maana hazinaga madhara sana na ni jadi yao tu
 
Mispalcement tu, hizo zilikuwa kwa ajili ya kujihami porini huko wanakofugia wanyama wao.
Sasa mjini, rungu, sime, na fimbo ni ya nini? Savage!
Alafu siku hizi watu hawapigani hovyo. Hayo ni mambo ya kizamani.

Watu wengi ni wagonjwa na hawajiamini kiafya sasa ukimpiga fimbo ya kicwa anaweza kuzima moja kwa moja.

Hili suala wakae wazee wa kumila wawashauri hawa wajasiliamali wa kimasai. Kuchokozwa au kudharauliwa kupo tu maana hata hivyo asilimia kubwa wengi wa wabango tunaambiwa tunaupungufu wa afya ya akili.
 
Back
Top Bottom