Kwanini historia ya Mwafrika kabla ya biashara ya utumwa na ukoloni haipo? Ni makusudi au bahati mbaya

Chachasteven

JF-Expert Member
Jul 4, 2014
1,878
1,849
Wakubwa zangu shikamoni. Wadogo marhaba na nyinyi wenzangu na mimi mambo vipi?

Ni matumaini yangu kuwa wote tu wazima, na kwa kuwa jicho na mkono wa Mungu upo juu yetu hivyo nalazimika kuamini kuwa ukitoa haya matatizo madogo madogo, suala la kuwa hai ni uzima tosha na ni la kushukuru. Lakini kuwa hai pasi na kujua kwanini upo hai ni jambo la kukemea.

Hebu tuwemo sasa,
Nasema hayo hapo juu kwa sababu leo nilipata fursa ya kupitia pitia makabrasha yangu ikiwemo ya shule ya msingi na sekondari... Kwa bahati nzuri au mbaya nikakutana na madaftari mengi ya somo la "history.' Katika kuperuzi peruzi nikagundua jambo moja ambalo limenipa maswali mengi sana.

Swali kubwa zaidi likiwa ni; Kwanini historia ya Mwafrika inaanzia kusimuliwa kipindi ambacho biashara ya utumwa na ukoloni vimeingia.?? Ikigusiwa ya kabla ya ukoloni na utumwa basi ni kiduchu sana. Je Watu wa enzi hizo hawakuwa na mfumo wa kuandika au kusimulia yale yaliyotokea - Ni kwamba Mzungu ndiyo kaleta kila kitu?? Kwa maana utasikia hata ziwa Victoria lilipewa jina la malkia wa wapi wapi sijui... Kuna vitu vingi tunafichwa, Na kwa dunia ya sasa inapoenda watoto wanaijua historia ya Queen Elizabeth kuliko hata ya Mwalimu Nyerere!!

Pia kunayo matukio mengi tu hayaandikwi kwenye historia ya darasani, Kama jaribio la kumuondoa nyerere madarakani... Vurugu za mwembe chai na kadhalika, hazina umuhimu au inakuwaje??..

Hata hivyo katika kujijibu nikahisi;

> Inawezekana hivi tulivyo sasa ni kwa sababu ya kukosa uelewa wa historia YA KWELI ya mwafrika. Hapa nazungumzia dini na tamaduni yake ya kweli.! Zamani wajukuu walikaa na bibi zao kusimuliwa, sikuhizi Televisheni ndizo zinatumika kuua ukweli wa Mwafrika na kusambaza kwa kasi ya moto uunguzao msitu, tamaduni za wenzetu. Ni jambo la kusikitisha.

> Inawezekana historia inayofundishwa darasani imewekwa kwa lengo la kutupotosha na kutusahaulisha, sisi, waafrika chimbuko letu ni nini hasa na njia zetu ni zipi haswa.

> Inawezekana kunazo ajenda nyingi kwa maana kiungo muhimu cha mtu ni historia ya jamii yake. Ili uelewe unaenda wapi ni lazima ujue unatoka wapi. Ajabu ni kuwa sisi historia yetu imeanzia kati kati kwa mujibu wao. Yaani tumetoka kuwa nyani tukawa watumwa, halafu tukatawaliwa then tupo hapa. Gibberish!!

Naamini kuna vitu tunafichwa and they can be traced, kwa kuwa bado ni mapema. Wanahistoria fanyeni kitu... Najua ni dozi chungu, lakini kwa hakika, mgonjwa anaihitaji ili apone.

Labda nirudie tena swali langu, Ni kwanini historia ya Mwafrika kabla ya biashara ya utumwa na ukoloni haipo popote. Inafichwa au haikuandikwa??
 
Katafute topic inaitwa pre colonial African societies. Hapo utajua waafrika tulikua tunafanya nini kabla kuja hao wakoloni.
 
I know that topic. Its the skeptical me that thinks there is more that isn't said publicly!!

Ni kiduchu sana kilichoandikwa na kufundishwa shuleni.
 
Yes alikimbilia misri herode alivyotaka kumuua, eliya alitwaliwa akiwa Ethiopia, falme za lubalunda, ngoni migration, chief milambo na ole tiptip, hima empire,..........
 
Hizi ni zile anazosimuliwa mtoto ila alale. Kuna zaidi ya hizi ndizo nazoulizia!!
 
Wakubwa zangu shikamoni. Wadogo marhaba na nyinyi wenzangu na mimi mambo vipi?

Ni matumaini yangu kuwa wote tu wazima, na kwa kuwa jicho na mkono wa Mungu upo juu yetu hivyo nalazimika kuamini kuwa ukitoa haya matatizo madogo madogo, suala la kuwa hai ni uzima tosha na ni la kushukuru. Lakini kuwa hai pasi na kujua kwanini upo hai ni jambo la kukemea.

Hebu tuwemo sasa,
Nasema hayo hapo juu kwa sababu leo nilipata fursa ya kupitia pitia makabrasha yangu ikiwemo ya shule ya msingi na sekondari... Kwa bahati nzuri au mbaya nikakutana na madaftari mengi ya somo la "history.' Katika kuperuzi peruzi nikagundua jambo moja ambalo limenipa maswali mengi sana.

Swali kubwa zaidi likiwa ni; Kwanini historia ya Mwafrika inaanzia kusimuliwa kipindi ambacho biashara ya utumwa na ukoloni vimeingia.?? Ikigusiwa ya kabla ya ukoloni na utumwa basi ni kiduchu sana. Je Watu wa enzi hizo hawakuwa na mfumo wa kuandika au kusimulia yale yaliyotokea - Ni kwamba Mzungu ndiyo kaleta kila kitu?? Kwa maana utasikia hata ziwa Victoria lilipewa jina la malkia wa wapi wapi sijui... Kuna vitu vingi tunafichwa, Na kwa dunia ya sasa inapoenda watoto wanaijua historia ya Queen Elizabeth kuliko hata ya Mwalimu Nyerere!!

Pia kunayo matukio mengi tu hayaandikwi kwenye historia ya darasani, Kama jaribio la kumuondoa nyerere madarakani... Vurugu za mwembe chai na kadhalika, hazina umuhimu au inakuwaje??..

Hata hivyo katika kujijibu nikahisi;

> Inawezekana hivi tulivyo sasa ni kwa sababu ya kukosa uelewa wa historia YA KWELI ya mwafrika. Hapa nazungumzia dini na tamaduni yake ya kweli.! Zamani wajukuu walikaa na bibi zao kusimuliwa, sikuhizi Televisheni ndizo zinatumika kuua ukweli wa Mwafrika na kusambaza kwa kasi ya moto uunguzao msitu, tamaduni za wenzetu. Ni jambo la kusikitisha.

> Inawezekana historia inayofundishwa darasani imewekwa kwa lengo la kutupotosha na kutusahaulisha, sisi, waafrika chimbuko letu ni nini hasa na njia zetu ni zipi haswa.

> Inawezekana kunazo ajenda nyingi kwa maana kiungo muhimu cha mtu ni historia ya jamii yake. Ili uelewe unaenda wapi ni lazima ujue unatoka wapi. Ajabu ni kuwa sisi historia yetu imeanzia kati kati kwa mujibu wao. Yaani tumetoka kuwa nyani tukawa watumwa, halafu tukatawaliwa then tupo hapa. Gibberish!!

Naamini kuna vitu tunafichwa and they can be traced, kwa kuwa bado ni mapema. Wanahistoria fanyeni kitu... Najua ni dozi chungu, lakini kwa hakika, mgonjwa anaihitaji ili apone.

Labda nirudie tena swali langu, Ni kwanini historia ya Mwafrika kabla ya biashara ya utumwa na ukoloni haipo popote. Inafichwa au haikuandikwa??
Kwani waafrika walianza lini kuandika ndipo History yetu ilipoanzia
 
Kunazo njia nyingi za kupitisha historia, naamini, kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Nitakupa mfano wa michoro labda! Sidhani kama kuandika ni kigezo kikubwa cha kusema historia ya mwafrika imepotea kwa sababu alikuwa haandiki tu!
 
Back
Top Bottom