Kwanini hatuwezi kupata Channel zingine DStv kama Startimes..... kwanini niwe na Decoder mbili?

Kwanini hatuwezi kupata Channel zingine DStv kama Startimes..... kwanini niwe na Decoder mbili?

CottonEyeJoe

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2008
Posts
331
Reaction score
73
TCRA tunaomba mliangalie hili tuweze kupata our Free-to-Air channels on DStv, Zuku, etc Decoders. Kwa nini niwe na decoder mbili… Makamba angalia hili bana….
 
Mkuu inabd uweke mbili 2. Kama nilivyofanya otherwise itakula kwako ukisubiri mamlaka

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mods hii mada hii ni mwafaka, ukizingatia kwamba tuna masaa mchache kbla hatujazimiwa mitambo koko (analojia) nashauri ingeenda kule kwenye jukwaa la gadgets na tech issues. Nakala kwa Fang, Buchanan na Paw.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: Paw
Mbili tu! Ting (Agape Tv), Star Times (TBC), King"amuzi cha ITV/ Star Tv, ongezea Zuku na Dstv.
Usipoangalia utamiliki kituo cha kurusha na kupokea matangazo!
 
Mbili tu! Ting (Agape Tv), Star Times (TBC), King"amuzi cha ITV/ Star Tv, ongezea Zuku na Dstv.
Usipoangalia utamiliki kituo cha kurusha na kupokea matangazo!
Hapa lazima harmonisation ifanyike haraka iwezekanavyo!
 
Kimsingi kuna tatizo katika mfumo mzima wa Ving'amuzi. Kuna siasa na biashara za wazito kati kuhama kutoka analojia kwaenda kwenye digitali. Kama mwisho wa kuhama ni 2015 kwanini Tanzania ina kiherehere cha kuhama mapema? Kwanini ziko nyingi!
 
Ndio maana mimi mpaka leo sijawa na king'amuzi chochote nasubiri wazime ndipo nione kipi ni kipi ah"
 
Channel walizopeleka kwenye Ving'amuzi ni zile zitakazowafanyia kampeini na zile ambazo hawana uhakika nazo hazitakuwa na nafasi mfano TV Mlimani ndo kwaheri. Kabla ya hgapo ilikuwa kwenye King'amuzi cha StarTimes lkn ikaondolewa kinyemela kwasababu ya sera zake.
 
dawa ni kuwabana hawa dstv,wenze2 kenya mpaka jana wana local chanels tano kweny package za dstv,kwa nin isiwe sisi? Viongozi wetu ni majanga sana
 
Hapa lazima harmonisation ifanyike haraka iwezekanavyo!

hawajamaa waliwaambia watanzania wajiandae kumbe wao ndio hawaja jiandaa muda wote waliokuwa wanatanza nivizuri wangetujuza watanzania tujiandae kununnua vingamuzi zaidi ya vitatu ilituweze kupata local channel leo namsikia naibu waziri makamba baada ya kuzima mitambo anazungumzia negotioation zinaendelea kuongeza channel kwenye baadhi ya vingamuzi kwa nini hilo lisingefanyika kabla.
 
Nimemsikia naibu waziri wa sayansi na technolojia ndugu Makamba jioni hii akikiri kuwa kuna changamoto nyingi wamezipata baada ya kuzima mitambo ya analojia na kwamba hata Dar tu kuna sehemu huwezi pata signal za digitali.

Nimebaki na mshangao!! Iweje haraka yote hiyo kumbe hata miundo mbinu bado?

Pili TCRA iliahidi kuwa kwenye kila king'amuzi free-to-air channel za tanzania zenye leseni za kitaifa zingeonekana kwenye ving'amuzi vyote vyenye leseni hapa Tanzania lakini cha kushangaza mpaka sasa DStv wanaonesha TBC1 tu.

Mimi sioni umuhimu wa kila mtu kuwa na vitatu au vinne ili kuona angalau channel zote za Tanzania ambazo ni free.

Mh. Januari tulitegemea uwepo wako hapo kama kijana wa kisasa kungeleta fikra mpya ndani ya wizara, hebu waelekezeni hawa watoa huduma za ving'amuzi waoneshe channel za kibongo ili watanzania tuzidi kuhabarika.
 
TCRA tunaomba mliangalie hili tuweze kupata our Free-to-Air channels on DStv, Zuku, etc Decoders. Kwa nini niwe na decoder mbili… Makamba angalia hili bana….

Mkuu naipenda jf ninayo moja napata za dstv,bongo,kanal,mytv,nk jf ni mambo yote
 
ngoja sasa waingie mikoani kuzima hiyo mitambo yao itakuwa ni issue nzito, coz hawajatoa elimu ya kutosha hasa mikoani na hayo makampuni yanayohusika na uuzaji wa ving'amuzi na yenyewe hayafahamiki vya kutosha na jinsi wanavyoendasha hiyo biashara(utoaji huduma), afadhali mjini mnawaelewa(tcra) lakini huko mbwinde hata hawaelewi kinachoendelea, tumekurupuka kwenye hili
 
Mimi sioni kama mikoani kutakuwa na tatizo kubwa sana,maana walio wengi tunatumia madish tangu siku nyingi hata kabla hivyo ving'amuzi vyao kuingia.
 
Back
Top Bottom