Kwanini hatupendi kusoma vitabu?

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,278
6,671
Binafsi naamini hata yule msomaji mzuri wa Riwaya tu ana uwezo
mkubwa wa kufikiri kuliko watu wasiosoma kabisa vitabu, Naombeni
ufafanuzi kwanini Watanzania wamekuwa si wapenzi wa kusoma vitabu
kama siku za nyuma?

Binafsi siwezi kusafiri safari ndefu bila kuwa na kitabu cha kusoma,
watanzania wamekuwa mabingwa kwenye meza za magazeti kusoma
vichwa vya habari bila kununua, tena kuna mtu mmoja namfahamu ikifika
asubuhi tu lazima achukuwe miwani kwenda kusoma vichwa vya habari bila
kununua lakini akiona ile mikanda ya kina KIRIKOU lazima anunue, hivi kuna
tatizo gani linasababisha yote haya,

Maoni yangu: tanzania ifute ushuru kwa viwanda vyote vinavyohusika
na hatua yoyote ya uchapishaji wa vitabu, pengine unafuu utasaidia kuinua
hamasa ya watanzania kujisomea.

NB: hata post kama hii wengine hushindwa kusoma eti ni ndefu,
Wadau naomba mchango wenu na mapendekezo ya nini kifanyike.
 
Mkuu,GAZETI naamini katika hili swala lakujisomea tena bila kujali ninachokisoma kama kina manufaa kwa sasa au lah!
Nafikiri hata kwa wingi wa machapisho na unafuu wa bei haitasaidia kama mtu hana kiu ya kujiongezea maarifa. Hii lazima iwe tabia ya mtu binafsi, alafu tabia ndio ishawishike na mazingira ya nje.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom