Kwanini Graduate huwezi kutajirika kwa kukimbilia kijijini. Ni kujizika

Kwanini Graduate huwezi kutajirika kwa kukimbilia kijijini. Ni kujizika

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
9,462
Reaction score
23,246
Utajiri ni watu. Ni rahisi kutajirika ukiwa kwenye watu wengi kuliko ukiwa mwenye porini eti unatafuta maisha.

Vijijini ni kwenda kuchukua mali ili uzitele kwa watu wengi utajirike.

Ukiwa msomi graduate halafu ukakata network na kukimbilia kijijini porini eti kutafuta maisha na utajiri unajipoteza.

Umiza kichwa katikati ya hao watu unaweza kufanya nini ukatoboa.

Kurudi vijijini au mahali pasipo na watu wengi ni kujirudisha zama za mawe za kale.

Kumbuka kukaa vijijini ni adhabu, ndio maana Mungu alimpa adhabu Kaini kwa kumuweka NOD ( Mahala pasipo watu).

Ni hilo tu.
 
Utajiri ni watu. Ni rahisi kutajirika ukiwa kwenye watu wengi kuliko ukiwa mwenye porini eti unatafuta maisha.

Vijijini ni kwenda kuchukua mali ili uzitele kwa watu wengi utajirike...
Endeleeni kujazana hapo nyumbani Dasalam.

Joto liwe lenu , jua liwachome , mvua ikinyesha mshindie chai ya mia mbili na kashata sisi wenye mji tuko huku vijijini kwenu tunazikusanya pesa tunakuja kuzitumia hapo huku tukiwadanganya kuwa sisi ni mafreemasons
 
Mali iko shamba,matajiri wa dunia wako matakoni mwa nchi yako wanasaka ngawira ww umejificha kwenye kijiji kikubwa unajiona mjanja.
 
Katika kitu nimejifunza, maisha hayana formula hasa haya ya kwetu. Unaweza kufanikiwa popote (iwe mjini / kijijini).

Apply yourself to whatever you're genius at, and you can do anything in the world.
 
Back
Top Bottom