Kwanini gharama za kusafirisha maiti huwa ni kubwa sana, vipi gharama za kusafirisha maiti kwenye ndege nazo ni kubwa sana?

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,277
6,673
Abiria wa kawaida anaweza kusafiri kwa 50,000 lakini umbali huo huo kwa maiti ikawa milioni moja mpaka mbili au zaidi kidogo.

Hata kama maiti haina mkao wa kawaida wa binadamu basi angalau ingezidi mara 2 au 3 kwanini gharama zinakuwa juu sana?

Kwa mliowahi kusafirisha maiti kwenye ndege vipi nako gaharama zinaweza kuwa mara 10 ya nauli ya kawaida?
 
Mara nyingi maiti husafirishwa mpk kijijini wakati abiria wa kawaida ataishia tu stendi Tena mjini.
Gari la maiti hutembea taratibu sana kwababu linakuwa limekodiwa tofauti na gari la abiria la kawaida linakuwa kwenye biashara zake za kawaida, kwa kifupi mnaposafirisha maiti mnakodi gari mkiwa wengi wkt unapisafiri unakuwa mwenyewe hamna mamlaka na gari.
 
Abiria wa kawaida anaweza kusafiri kwa 50,000 lakini umbali huo huo
kwa maiti ikawa milioni moja mpaka mbili au zaidi kidogo. Hata kama maiti
haina mkao wa kawaida wa binadamu basi angalau ingezidi mara 2 au 3
kwanini gharama zinakuwa juu sana?
Kwa mliowahi kusafirisha maiti kwenye ndege vipi nako gaharama zinaweza kuwa
mara 10 ya nauli ya kawaida?
Kwenye ndege wengi hatujui ila ukitusaidia tutajua andika wasia wako tukuzike wapi kisha katisha maisha yako na sisi tutachukua maiti yako mpaka eapoti ambako tutaambiwa nauli nasi tutakujibu gharama zake.
 
... Mkuu, unasafiri kutoka hapa kwenda Mbeya kwa mfano, unatoa nauli ya shs Alfu 50, lakini kumbuka kuwa ndani ya basis mpo abiria 55 hadi 60 mliyotoa nauli hiyo. Kwa maana kwamba mwenye basi lake ameishatengeza faida.
Sasa chukulia maiti mmoja na waombolezaji madhalani 25 wasafirishwe kwa nauli hiyo hiyo! Hapa lazima mfanyabiashara azibe like pengo LA kusafirisha abiria 25 kwa mapato ambayo yangepatikana kwa kusafirsha abiria 55!!
Unadhani hapo nani atabamizwa??
 
Maiti inarudi kama mzigo na mzigo kwenye ndege unalipwa kwa kg na kila kilo ni hadi dollar 5 wengine wana taratibu zao za kusafirisha ndio maana unakuta zinafika hadi 40mil
Kwa mfano maiti pamoja na jeneza zinaweza kuwa na kilo 120@$5=$600*Ths. 2300= Tshs. 1,380,000/= Mbona haifiki hzo 40mil?
 
Mkienda na maiti stendi halafu mkaweka jeneza kwenye buti na mkashushiwa stendi ya mnakoenda hakuna gharama.

Unapokodi coaster ianche kupiga routes zake siku nzima kwa ajili yako lazima uwape mapato ya siku kama wakikupiga zaidi jua ni tamaa zao tu.
 
Abiria wa kawaida anaweza kusafiri kwa 50,000 lakini umbali huo huo
kwa maiti ikawa milioni moja mpaka mbili au zaidi kidogo. Hata kama maiti
haina mkao wa kawaida wa binadamu basi angalau ingezidi mara 2 au 3
kwanini gharama zinakuwa juu sana?

Kwa mliowahi kusafirisha maiti kwenye ndege vipi nako gaharama zinaweza kuwa
mara 10 ya nauli ya kawaida?
Kwenye ndege wanapima kwa kilo na au dimensions then unapewa jumla.Kwa mfano kama uzito ni 100kg unaambiwa tu kila kio ni bei gani then unazidishiwa kwa rate ya kio moja ya mzigo
 
Usikariri fikiri kisayansi. Kwa maana tukianzia hizo 40mil/Tshs2300*$5= Kg 3478.26. Yaani jeneza na maiti vinakuwa na Kg 3478.26! Mhh nyinyi watu mbona mnataka kula vya watu bila aibu? Hebu kasome hesabu upya!!
Hayo ya Mil 40 sijasema mimi..!! Ila Maiti na jeneza kuwa na Kilo 120 ndo nimeshangaa.. Kwanza mtu akifa kilo zinaongezeka..pili jeneza kilo zikipunguza sana 100 labda kama Maiti ya mtoto na jeneza la mtoto sio mtu mzima.
 
Mheshimiwa bado tu mungu hajakupenda? Sisi huku bado tunafanya mahesabu hatujui jibu tutalipata lini, njia ya wosia ndiyo ilikuwa fupi na sahihi. Tukienda eapoti bila mzigo hatutapata jibu tutaambiwa tupeleke mzigo wakaupime kwani watu wanatofautiana uzito.
 
Hayo ya Mil 40 sijasema mimi..!! Ila Maiti na jeneza kuwa na Kilo 120 ndo nimeshangaa.. Kwanza mtu akifa kilo zinaongezeka..pili jeneza kilo zikipunguza sana 100 labda kama Maiti ya mtoto na jeneza la mtoto sio mtu mzima.

Bado jamaa hakukosea kiasi cha kumlinganisha na “WanaKolomije”, ametumia hizo figures kama ‘mfano’ tu.... nimejifunza kitu kupitia mfano wake.

Hapo kwenye ‘kilo kuongezeka’ hebu fafanua kidogo kwa FACTS.
 
Back
Top Bottom