Kwanini gharama za DSTV zinapanda maradufu?

LINCOLINMTZA

JF-Expert Member
Mar 15, 2011
1,639
516
Wanabodi,

Naomba kwa mwenye taarifa, kwa nini gharama za ulipiaji wa DSTV zimepanda ghafla tena kwa gharama kubwa?Kifurushi kilichokuwa 17,000 kwa sasa ni 23,500, kilichokuwa 34,000 kwa sasa ni 51,000 na kilichokuwa 56000 kwa sasa ni 84000 hadi 147000 ukiongeza Supersport 3 na 7. Tatizo ni nini? Wameleta mitambo mipya?

Mwenye taarifa, naombeni nijue.
 
tatizo la azam chanel za kihindi ni nyingi sna utafikiri wote wahindi sijui wanapata bure

hakuna chanel za wanyama. leguer 1tu ya spain ndio huonesha
 
tatizo la azam chanel za kihindi ni nyingi sna utafikiri wote wahindi sijui wanapata bure

hakuna chanel za wanyama. leguer 1tu ya spain ndio huonesha

Noted mkuu? Tatizo langu ni hawa DSTV! Sasa hivi wanapromosheni ya kuuza Dish, na decoder kwa Shilingi 79000. Sijui hili punguzo ndo wamelifidia kwa wateja wa zamani? Kwa nini washushe bei ya kununulia decoder na dish halafu wapandishe gharama za ulipiaji? Mimi nilikuwa najua kwamba gharama ya ununuaji vifurushi zingeshuka kadiri siku zinavosonga mbele kama mitambo ya simu.
 
hicho king'amuzi kimekuwa bei juu sana kwakweli
 
Hawa jamaa wanatumia udhaifu wetu ukienda Durban,harare,lilongwe na lusaka hata abidjan bei yao iko chini sana sijui tatizo liko wapi. TCRA wameshindwa kuwa control hawa watu wasipandishe bei hovyohovyo. Na jinsi tunavyokwenda vingamuzi vyote vitakuwa na trend hiyohiyo wakati channel nyingi mfano za easy tv,azam wao wanazipata bure kwenye Fta. Nenda nchi kama misri,sudan hizi mbc ni bure kwenye madish ya upepo
 
Bei zao zinaenda sambamba na thamani ya sarafu yetu, wao gharama zao ni kwa dollar.

Mkuu mbona na wao rand haipo stable kwa dollar ilikua rand 7 kwa dollar moja ss ni rand 14 kwa dollar moja iyo rate ya leo..inakuaje South Africa malipo ni kidogo sana na ni nchi ambayo watu wanajiweza huku kwa masikini malipo mpaka laki na themanini kwa mwezi ? Na pia channel south zipo nyingi zaid kuriko huku tunakolipa ghali zaidi..huku imekua ni starehe wakati jozi sio starehe kwa kuwa wengi wanamudu kulipa dstv..
 
Mambo yote ni bain sport kwanza ipo inaonekana kria, supersport wanajidai ni HD ila muonekano wao wala sio bora, na mabei yao rukuki.
 
Mkuu apa south africa ukilipia dstv RAND 350 unaona channel zote
 
Mkuu apa south africa ukilipia dstv RAND 350 unaona channel zote
Ambazo kama rand 14 ni sawa na US dollar 1, ina maana huku Tz twatakiwa tulipe Tshs.55000 kama 1US dollar ni Tshs 2200.Wanatuibia sana kama kura za.........
 
Wanabodi,

Naomba kwa mwenye taarifa, kwa nini gharama za ulipiaji wa DSTV zimepanda ghafla tena kwa gharama kubwa?Kifurushi kilichokuwa 17,000 kwa sasa ni 23,500, kilichokuwa 34,000 kwa sasa ni 51,000 na kilichokuwa 56000 kwa sasa ni 84000 hadi 147000 ukiongeza Supersport 3 na 7. Tatizo ni nini? Wameleta mitambo mipya?

Mwenye taarifa, naombeni nijue.

Premium 219,000/=
 
Back
Top Bottom