Kwanini gharama za DSTV zinapanda maradufu?

Kwanini gharama za DSTV zinapanda maradufu?

Hawa jamaa wa DSTV ni kimeo dawa ni kuwakomesha tu watu wengi kuondoka kwa maramaoja then wajiulize kulikoni. Ni wizi mtupu, mimi mkuu nilishaachana nao dish lipo juu kama ulembo tu. na hao TCRA ni maboya tu hawawasaidii wa TZ sidhani hata kama wanafanya huo utafiti wa kulinganisha bei.
 
Wanabodi,

Naomba kwa mwenye taarifa, kwa nini gharama za ulipiaji wa DSTV zimepanda ghafla tena kwa gharama kubwa?Kifurushi kilichokuwa 17,000 kwa sasa ni 23,500, kilichokuwa 34,000 kwa sasa ni 51,000 na kilichokuwa 56000 kwa sasa ni 84000 hadi 147000 ukiongeza Supersport 3 na 7. Tatizo ni nini? Wameleta mitambo mipya?

Mwenye taarifa, naombeni nijue.

Achana nao, mie nimehamia Azam mwezi wa tatu sasa, bei zao za vifurushi ni nafuu sana. DStv decoder na dish sivitumii tena, anayehitaji ani-pm, bei maelewano.
 
Ni kweli mkuu wangu DStv ni shida na janga kwa waTanzania wengi hasa wenye kipato cha kati 219,000/=
 
Mnaotumia azam mngeweka bei za vifurushi ili watu wafanye maamuzi magumu. Na mnaotumia digitek mngethibitisha kama kweli hakuna malipo ya mwezi muone kama watu hawatasema Suu. Raha ya dstv kifurushi kiwe premium sasa kwa jinsi thamani ya shilingi ilivyo dola 100 kwa decorder sio wengi watakaoweza
 
Ambazo kama rand 14 ni sawa na US dollar 1, ina maana huku Tz twatakiwa tulipe Tshs.55000 kama 1US dollar ni Tshs 2200.Wanatuibia sana kama kura za.........

Ukiongezea na VAT 18% bado hatufiki bei ya kifurushi cha premium
 
Wenye mamlaka watueleze hili? Hiki chama cha haki za binadamu na wanaoshughulikia katiba, hawaoni kuwa tunanyimwa haki yetu ya msingi kabisa hapa kwa kubania vyombo vya kupatia taarifa. Wanasema taarifa ni haki ya mtu, sasa vipi hapa? Au wanasubiri CHADEMA na CCM ndo wakurupuke kutetea vyama na siyo wananchi?
 
Tujiulize pia.who is behind multichoice tanzania. Ndio maana ni untouchable
 
Mkuu mbona na wao rand haipo stable kwa dollar ilikua rand 7 kwa dollar moja ss ni rand 14 kwa dollar moja iyo rate ya leo..inakuaje South Africa malipo ni kidogo sana na ni nchi ambayo watu wanajiweza huku kwa masikini malipo mpaka laki na themanini kwa mwezi ? Na pia channel south zipo nyingi zaid kuriko huku tunakolipa ghali zaidi..huku imekua ni starehe wakati jozi sio starehe kwa kuwa wengi wanamudu kulipa dstv..
Mkuu sasa hiv DSTV premium unalipia 219,000, kutoka 199,000, 168,000, 147,000... Hizo gharama zilipanda ndani ya mwaka mmoja.. Kwa kweli Serikali iingilie kati.... hapa naona kuna watu wachache wanafaidi hela za watanzania...hasa wale top management...but hawa wachin wanalipwa kama matella wa bank...
 
Be careful, unaweza ukajisahau ukamaliza kodi ya nyumba na hela ya matumizi mengine ya hapo kwako...
#FanyaMaamuziMagumu Tafuta kisimbuzi cha bei nafuu mfano digitek au Azam tv...
 
Mkuu sasa hiv DSTV premium unalipia 219,000, kutoka 199,000, 168,000, 147,000... Hizo gharama zilipanda ndani ya mwaka mmoja.. Kwa kweli Serikali iingilie kati.... hapa naona kuna watu wachache wanafaidi hela za watanzania...hasa wale top management...but hawa wachin wanalipwa kama matella wa bank...
Katili mkapa anatuumiza pale.
 
Mnaotumia azam mngeweka bei za vifurushi ili watu wafanye maamuzi magumu. Na mnaotumia digitek mngethibitisha kama kweli hakuna malipo ya mwezi muone kama watu hawatasema Suu. Raha ya dstv kifurushi kiwe premium sasa kwa jinsi thamani ya shilingi ilivyo dola 100 kwa decorder sio wengi watakaoweza

Azam TV wako poa sana. Vifurushi vyao ni Azam Pure 24+ channels 12,000/= @ mwezi;, Azam Pure 50+ channels 20,000/- @ mwezi; Azam Play 80+ channels 25,000/- @ mwezi, na unaweza kuongezea Azam Sports channel 4: [1] Azam Sports HD, [2] Manchester United TV, [3] Liverpool FC TV na [4] Real Madrid TV) 15,000/-. Kama huja renew kifurushi, local channels utaendelea kuangalia free of charge!!

Samahani kama nimekosea naomba Azam au wanaojua zaidi wanisahihishe!
 
Asante sana mkuu. Natumai utakuwa umesaidia wengi sana ili nao wafanye maamuzi
 
Back
Top Bottom