Kwanini DSTV ni ghali sana?

Mara mia DSTV kuliko hivi ving'amuzi mbuzi
 
Kwanini usijilazimishe kupenda LIGI YA bongo?! acha kuwa mtumwa!

Viongozi wenyewe ndo hawa akina Aveva.. Kaburu.. Manji.. Sanga ndo ulazimishe watu wapende mpira..? Mpira wa bongo ni pasua kichwa..! Yaani viongozi wa simba na yanga wanaungana kuiba mapato ya milangoni na kugawana halafu unilazimishe nipende mpira mie..! Hawa ambao wanatakiwa kuwa wabunifu na kujenga timu zenye uwezo na kujitegemea leo ndo wasaka tonge wakubwa..

Acha tujinogeshe na ligi za ulaya zinazoendeshwa kiushindani wa hali ya juu..
 
Nafikiri huu uzi sijauelewa!!
Kuna promo au!

Huyo naye amekurupuka tu!! Bila kujua kwa sasa startimes wameleta kifurushi kipya unalipia tsh.4000 kwa mwezi unapata channel za ziada kama nne hivi.iman tv, cctv 9, swahili na nyingine kama mbili hivi.ndio tangazo lao la sasa na sio bei ya decoder.
 
DSTV wana ving'amuz vya ofa kwa sasa vinauzwa tsh 99000 na unalipia tsh 17000 kwa mwez! Hilo ndo tangazo lao lililopo hewani!
 
Huyo naye amekurupuka tu!! Bila kujua kwa sasa startimes wameleta kifurushi kipya unalipia tsh.4000 kwa mwezi unapata channel za ziada kama nne hivi.iman tv, cctv 9, swahili na nyingine kama mbili hivi.ndio tangazo lao la sasa na sio bei ya decoder.
Wewe ndio umekurupuka.., wanauza decoder iliyounganishwa kwa shs.4,000/=!
 
Kwanini usijilazimishe kupenda LIGI YA bongo?! acha kuwa mtumwa!

Ligi ya Bongo naangalia kwenye Azam Tv. Kwa ufinyu wa akili zako unadhani kuangalia ligi za nje ni utumwa. Vingapi Tanzania tunatumia vya nje?
Internet inayokuwezesha ku post humu JF si ya Bongo. Huo sio utumwa?
 
Mkuu, achana na mpuuzi huyo. Azam Tv yenyewe anaangalia vibandani.
 
Hizo ndio hoja za maana.
 
Dawa ya DSTV iko jikoni karibia inaiva ,inaitwa AZAM TV
 
Dawa ya DSTV iko jikoni karibia inaiva ,inaitwa AZAM TV

Azam TV atanionyesha Discovery HD,Crime &Investigation, BBC knowledge? Siku wakiwa na hizo channels na mimi nitawatelekeza DSTV,sio leo wala kesho.Multchoice wako mbali sana kulinganisha na hivi ving'amuzi vya Star times
 
hao wote kuwa na vitu hivi bado sana, mwenye uwezo aangalie DSTV kwa raha zake asiye na uwezo abakie na hivi videcoder vya kibongobongo maana biashara huria hata nguo kariakoo inatofautiana na inavyouzwa posta hata kama quality ni ileile, ukiuliza utaambiwa kodi ni tofauti. ndio inavyokuwa kwa hawa DSTV ila pamoja na hayo si kitu cha lazima saaana kivile kwa hiyo mtu kama ha-afford anaweza kupotezea kiaina
Azam TV atanionyesha Discovery HD,Crime &Investigation, BBC knowledge? Siku wakiwa na hizo channels na mimi nitawatelekeza DSTV,sio leo wala kesho.Multchoice wako mbali sana kulinganisha na hivi ving'amuzi vya Star times
 
Dawa ya DSTV iko jikoni karibia inaiva ,inaitwa AZAM TV
Naona DSTV sasa wanaanza kuuza visimbuzi vyao mpaka barabarani..
Na bado mtufate majumbani mgonge milango na kutuuliza kama tunataka huduma zenu...

Wekeni bei zinazoendana na hali halisi ya kimaisha muone kama hamjapata wateja wengi.
 
Mbina kwa sasa imedikia 69000 wwe unataka ifike bei ya bure??
 
AZAM TV tusaidie tuondokane na utumwa wa DSTV, kwa kweli ni ghali sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…