Kwanini Dr Ndalichako asijiuzuru?

Kwanini Dr Ndalichako asijiuzuru?

Status
Not open for further replies.
Unajua kwa mtu anayefatilia isue za waislam atakubaliana na mimi kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakitoa malalamiko yao kwa njia za kidiplomasia lakini kila suala waliloliendea kwa njia za kidiplomasia serikali ilitia pamba masikioni sasa wamesha ona hizo njia hazina mpango nao kwahiyo wanaloamua walifanye watalifanya tu wala hakuna wakuzuwia. Pia kwa kipindi kirefun sana magazeti na TV ni vyombo ambavyo kupia wahariri na waandishi wa hivyo vyombe hupotosha habari za waislam, hilo waislam wote wanalijua kwa hiyo haliwashughulishi tena, narudia haliwashughulishi tena, tena mkiona namna gani vipi muache tu hata kureport habari zinazowahusu waislam.
NECTA ni kitengo cha parokia, wafanya kazi wote wa baraza ni waRC does it mean kwamba pale wengine hawana sifa ya kufanya kazi?

NDALICHAKO BORA UJIONDOA MWENYEWE USISUBIRI KUAIBISHWA ZAIDI KWANI MAANDAMANO YALIYOENDA KWA NCHIMBI YALIKUWA CHA MTOTO, NA HATUTOONDOKA MPAKA UMEFUNGASHA MAKABURASHA , ukawe katibu mkuu wa mitihani kanisani kwenu. Tumechoka kuonewa
 
Soma vizuri comment yangu "Wanatangazwa kuunga mkono CUF". Najua kuna propaganda za Udini lakini ni nani aliyekanusha wito wa Makamu mwenyekiti wa CUF pale jangwani wa kuwataka Waislamu wote wajiunge CUF? Sio Waislamu wenye wala Uongozi wa CUF uliokanusha, what does it imply?

hapo wanafanya makosa. lakini hata wala wachungaji wabunge wakati wa kampeni wajua walikuwa wana wahubiria nini waumini wao.....! mambo kama haya haya fai kwa ustawi wa demokrasia nchi hii. na kosa kidogo CCM inachukulia mtaji kukutoa kabisa kwenye ramani!!!
 
hii nssf nafikiri unaitazama kijuu kijuu.

Hebu fuatilia tokea kuanzishwa kwake 1967 utaona wapi umeilipo kupuruchuka.

Mimi nikiwa wizara ya fedha nakumbuka nilifana nao sana kazi hawa wakti huo ikiitwa npf (national provident fund) chini ya saguti na baadae oming'o na baadae mh mkullo.

Chunguza kwanza hilo kisha linganisha na baraza la mitihani tokea kuanzishwa kwake taza katibu mtendaji wake na manaibu katibu watendaji wake wote. Utaliona dhahir shahir.


Lakin vile vile kuna mifuko mingi siku hizi huko tz kama ppf, gpf , nssf etc. Kwanini dr dau tu?
Nina uhakika na nilichobainisha.

lengo lako ni nini? Kupata mapandikizi kila kona sio?
 
Nimejifunza kitu hapa! Lakini kwanini kuna kuwa na kauli tata toka kwa viongozi wenye Ilimu? Ushekhe unasomewa chuo kipi?
Kuhitilafiana ki rai hili ni jambo la kawaida sana, ila sijui ni utata upi unaomaanisha.

Ushekhe unasomewa chuo kipi?:
Ki asili Usheikh mtu huupata baada ya kukaa na Sheikh anayeeleweka na kusoma kwake kwa miaka, halafu huyu Sheikh akiridhika na mwanafunzi wake humuandikia Ijazah. Yaani huandikwa kama"huyu ana ijazah kutoka kwangu ya kufundisha somo fulani" inawezekana ikawa mtu ana ijazah kutoka kwenye fani ya Hadith, au Fiqh au Aqidah n.k

Lakini siku hizi si wengi wanaokaa na Masheikh miaka na miaka na kusoma kwao bali watu huenda katika vyuo vikuu vya Kiislamu, zile shahada zinazopatikana mule vyuoni huwa ndizo ijazah kwa wakati wetu huu. Sasa kama kuna mtu ana Doctorate kutoka Madinah University basi mtu huyo mimi nitamuita Sheikh.(Lakini si kigezo peke yake cha Usheikh).
 
Binafsi sioni sababu ya yeye kubakia hapo. Kwano kosa kama hilo la kiutendaji ni kubwa sana kwa jamii hasa ukizingatia kuwa limefungamana na mambo ya kiimani. Ikumbukwe ni siku nyingi sana waislam hao hao wa Tanganyika wamekuwa ma msururu wa malalamiko ya kudhurumiwa haki zao na Serikali yao.

Lakin ni funzo sana kwa Serikali ya JMTz kujifunza zaidi ikiwemo pamoja na kulifanya Baraza hilo la Mitihani kuwa na SURA YA MUUNGANO. Kwa kuamua kama Katibu mtendaji atatoka upande mmoja wa muungano basi naibu wake atoke upande wa pili wa Muungano kama ilivyo kwenye taasisi na wizara zote zenye sura ya Muungano kama BOT etc.

Lakin vile vile ikumbukwe tokea kuanzishwa kwa baraza hilo viongozi wake wakuu kama katibu mtendaji mkuu na naibu wake wote wamekuwa wakristo. Hakuna muislam hata mmoja na hapo ndipo panapozidisha mashaka kwa chombo hicho.

lakin mwisho za mwizi arobaini. sasa ukweli umedhihiri. Laazima Katibu mtendaji mkuu wa Baraza hilo lazima awajibike kwa kujiuzuru ikiwemo pamoja na kuwafikisha mahakamani kutokana na kuwa athri watoto hao kisaikologia na kuwapotezea muda wao.

Nadhani sasa ifike mahali Waislamu wanatakiwa kujitathmini kuhusu nini wanataka katika nchi hii. Kwa kifupi mimi binafsi naona kama hakuna jambo wanalolianzisha wakalimaliza na kupata matokeo wanayoyahitaji. Sisiti kutamka kuwa wengi wao wanatumika tu kama ngazi ya kuwafikisha mahali fulani "Waislamu" wenzao ambao ni werevu na wenye ajenda za siri kwa mgongo wa imani ya Kiislam. Kwa uchache ni kwamba waislamu walitaka Mahakama ya Kadhi, hata kabla ya kupatikana mahakama hiyo tayari wameanza kuzurugana wao kwa wao. Wanataka kupewa nafasi za upendeleo katika uongozi wa nchi, eti kuwe na uwiano wa madaraka katika taasisi za umma. Aidha wanataka wapewe nafasi za ukuu wa taasisi zote zile ambazo kutoka zilipo asisiwa hazijawahi kushikwa na Waislamu. Hayo ni mawazo yao, je wanasemaje kuhusu safu za uongozi katika serikali zetu mbili ( Muungano na SMZ)? Je, nao wa upande wa pili wapige kelele? Juzi kuna wananchi wenzetu wametenda kosa la jinai kwa kugomea kuhesabiwa "Waislam" wameandama hadi makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani na kushinikiza kuachiwa kwa "Waislam" wenzao waliokamatwa kwa kuvunja sheria? Muitikio wa serikali katika hilo sote tunaufahamu, sasa wanataka kulazimisha Dr. Ndalichako ang'olewe hivi "Waislam" sasa wamekuwa ni "pressure group" au ni "Wanaharakati"? Kama ndivyo kwanini basi wanachagua matukio? Pale Morogoro Kuna "Muislam" alipigwa na "kitu kizito" kilichorushwa na "wenye nchi" akafa mbona sikuona "Waislam" kuishinikiza serikali ifanye uchunguzi wa kilichoondoa uhai wa Marehemu pale Morogoro au yule bwana hakuwa "Muislam"?
 
Huyo ni Binti wa Mfalme, amewasaidia vigogo wengi wa CCM na watoto wao kupita mitihani inayosimamiwa na NECTA.
 
na hyo ndo alitakiwa awe wa kwanza kisha wengine wafuate, bado ameng'ang'ana kuwepo hapo, na hao wanaodai ndalichako wao hwamuoni mwenzao ndo kawasaliti, shukuru kwanza ndo tuende kwingineko.

Madai yetu kuhusu NECTA ni ya muda mrefu hata kabla ya huyo shukuru. Na yeye asipokuwa makini tunamng'oa. Sisi hatuangalii nani yuko pale tunataka haki itendeke. Ndalichako ndio mtendaji wa baraza. Kule Nishati alianzwa katibu kisha Ngereja alifata baadae. madai yetu ya miaka kumi Je 10years back Shukuru alikuwepo pale?
 
Wizara ya ...

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu Waziri wa Elimu...
.


Wewe Barubaru!
Hii issue HAIKUHUU!

WEWE SIO MTANZANIA. RUDI KWENU OMAN UKASHUGHULIKIE "NECTA" YA KULE.
 
hoja sio nani ni nani au nani ameolewa au kumuoa nani, hoja ni awajibikaji kwa kila mmoja bila kujali dini, jinsia au rangi.
Necta wanatakiwa wajichunguze kwani haya yasingetokea kama si waislamu kushinikiza.
Mwanzoni necta walikataa na wakapinga kuwa si kweli kabla hata hawajafanya uchunguzi, leo imethibitika.
 
Barubaru, kuna waziri aliyekuwa akiingoza hii wizara naye vipi? amefaurisha wanafunzi zaidi ya 5,000 hawajui kusoma na kuandika, mi napendekeza Dr. Shukuru Kawambwa nae angejiuzuru, kwasababu kama zaidi ya madenti 5000 wamefauru while hawajui kusoma wala kuandika sasa hao waliofeli hawajui nini?

Acha kuhamisha magoli.Aliesahihisha hiyo mitihani ni nani kama si NECTA?Pale kuna matatizo makubwa zaidi ya huo mtihani wa kiislamu
 
Hiyo siyo siasa,ndalichako yuko pale kama mtaaluma,hatuwez kuweka mtu yeyote tu eti kwa sababu ni muislam afu akatuharibie kazi.she has proved to be hard working with strong standings all her time there.binafsi siungi mkono kujiuzulu Dr.Ndalichako
 
Unajua kwa mtu anayefatilia isue za waislam atakubaliana na mimi kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakitoa malalamiko yao kwa njia za kidiplomasia lakini kila suala waliloliendea kwa njia za kidiplomasia serikali ilitia pamba masikioni sasa wamesha ona hizo njia hazina mpango nao kwahiyo wanaloamua walifanye watalifanya tu wala hakuna wakuzuwia. Pia kwa kipindi kirefun sana magazeti na TV ni vyombo ambavyo kupia wahariri na waandishi wa hivyo vyombe hupotosha habari za waislam, hilo waislam wote wanalijua kwa hiyo haliwashughulishi tena, narudia haliwashughulishi tena, tena mkiona namna gani vipi muache tu hata kureport habari zinazowahusu waislam.
NECTA ni kitengo cha parokia, wafanya kazi wote wa baraza ni waRC does it mean kwamba pale wengine hawana sifa ya kufanya kazi?

NDALICHAKO BORA UJIONDOA MWENYEWE USISUBIRI KUAIBISHWA ZAIDI KWANI MAANDAMANO YALIYOENDA KWA NCHIMBI YALIKUWA CHA MTOTO, NA HATUTOONDOKA MPAKA UMEFUNGASHA MAKABURASHA , ukawe katibu mkuu wa mitihani kanisani kwenu. Tumechoka kuonewa
Mark unafurahisha!kwelikweli! mtu akisoma hii post yako atafahamu tu kuwa kuna tatizo katika kufikiri kwako. Mtu mzima lazima utoe hoja, na hoja iwe na mshiko. Haiwezekeni wafanyakazi wa Baraza wote wawe RC. Hivi katibu mkuu wa baraza kesho akiwa muislamu na watu wa chini yake wakifanya makosa tunamtoa na kumweka mkristo! au tunamtoa kwa sababu ya dini yake?
 
Wakati Dr.Ndalichako aliposhika madaraka pale NECTA alimteua naibu wake ambaye alikuwa Muislam jina lake Ahmed Ally lakini aliacha kazi kwa hiari yake mweyewe na kurudi UDSM kufundisha.
 
Wengi wa wachangiaji wamesahau kuwa katika ile tume iliyoundwa kuchunguza matokeo ya Islamic Knowledge kulikuwa na Waislamu! unafikiri watashindwa kuwamwagia Waislamu wenzao madudu yote waliyoyaona kwa Ndalichako na NECTA yenyewe? waite professionals hivyo hawataweza kumwambia Shikh Ponda, Kundecha au Barhiyan lakini watoto wao je? ndugu zao wa karibu?...think great!
 
By Miganiko:
"...your
arguments is a mere verbal diarrhea."

Kama English yako ndio hii bora tu utumie Kiswahili.
 
Kwanini Nchimbi , IGP Mwema, Kamanda Kamuhanda hawajiuzulu kwa tukio la Iringa, hivi tukio na NECTA na Islamic knowldge lipi Ni baya na ambalo linahitaji watu wawajibike, Hivi nyie ndugu zetu (Waislam ) Baadhi yenu Vichwa vyenu vimejaa Madudu au Matope

HAWO uliowataja wanawajibika kujiuzulu kama itathibit police walihusika na walifanya hivyo kwa amri zao.
ima kama police wale walifanya kwa nafsi zao hawajuzu kujiuzulu,
Ndalichako sio suala la uislam, sula hapa anapasisha walio feli na kufelisha walio soma
NECTA miaka nenda miaka rudi inakabiliwa na kashfa za mitihani kuvuja , hili tatizo la kila mwaka na ndalichako ameshindwa kuliondoa, anajaribu kufuta mitihani ya baadhi ya shule lakini baadhi ya shulke ambazo nazo zinahusuka na udanganyifu anaziwachia zipete.
hili ni tatizo kubwa kuliko la hao police
kwani unapopata maafisa polisi walio kokotoa mitihani lakini hawana uwezo ndio sasa tuna polisi wasio tumia akili ila nguvu
kwa hio lazima Ndalichako ajiuzulu , amesababisha matatizo makubwa kutokana na kushindwa kufanya haki katika matokeo ya mitihani huu ni uhain ni uhaini ni uhaini..
japo kumekuwepo na malalamiko ya muda mrefu kuhusu upendelo lakini ameshindwa kutoa tamko
ama ameshindwa kubuni mbinu ambazo zitaondoa kabisa malalamiko mfano kuwapatia watahaniwa vitambulisho vya namba na kufanya mitihani kwa namba na matokeo kutolewa kwa namba
serikali lazima imuondoe....hafai
 
Mark unafurahisha!kwelikweli! mtu akisoma hii post yako atafahamu tu kuwa kuna tatizo katika kufikiri kwako. Mtu mzima lazima utoe hoja, na hoja iwe na mshiko. Haiwezekeni wafanyakazi wa Baraza wote wawe RC. Hivi katibu mkuu wa baraza kesho akiwa muislamu na watu wa chini yake wakifanya makosa tunamtoa na kumweka mkristo! au tunamtoa kwa sababu ya dini yake?

Kweli umenielewa kiasi fulani ila kuna mahala hujaelewa. Ndalichako hatumtoi eti kwa kuwa wafanyakazi wake wote ni RC, hapana yeye kama mtendaji anatakiwa awajibishwe hiyo ni moja pili ni kuwa tunataka baraza lote liundwe upya kwahiyo hao watendaji unaowazungumzia kuwa ni wa chini sehemu nyeti kama hiyo hawatakiwi wawe wa imani moja, ni rahisi mno hujuma kufanyiwa watu wa imani nyingine ambao hawapo pale. wala sisi hatuhitaji eti ni lazima katibu awe muislam bali tunahitaji awe mwingine na baraza liundwe upya na liwe huru kufanya kazi zake. Tunahitaji katibu aliyetenda kazi za baraza kwa hisia kubwa ya imani yake. Ndalicho bai bai
 
Kwa hiyo waislamu wasingehoji matokeo ingekuwa imetoka pasingejulikana kitu,nawasiwasi hata masomo mengine watakuwa wanachakachua tu kama wameweza kuchakachua somo letu wenyewe,na hii ni makusudi wala si bahati mbaya ngoja tufanye uchunguzi tutaona tu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom