Kwanini Dingiswayo hapewi heshima anayopewa Shakazulu?

Kwanini Dingiswayo hapewi heshima anayopewa Shakazulu?

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
19,943
Reaction score
37,825
Ulisoma historia ya Africa vizuri utagundua kuwa Shaka Zulu alikuwa mentored na Dingiswayo.Mafanikio na umahiri aa Shaka Zulu katika.medani ya vita ulitokana na mafunzo aliyo yapata kutoka kwa Dingiswayo.However Dingiswayo hapewi kabisa heshima kama anayopewa Shaka Zulu. Sababu unaweza kuwa nini bandeko?
 
Dingiswayi alimfundisha Tshaka Zuli vita!?..Hebu ngoja nirudi darasani..
Cc: Malcom Lumumba zitto junior hearly Elungata
There his martial abilities brought him to the notice of the paramount chief, Jobe, and, after Jobe’s death in 1807, to that of his successor, Dingiswayo. For nine years Shaka served in Dingiswayo’s army as it subdued tribe after tribe (including the Zulu). It was during this period of almost ceaseless war that he devised the ruthless political and military philosophy that would transform the fortunes of his father’s clan- Zulu: The Heroism and Tragedy of the Zulu War of 1879 by Saul David

CC:
Consigliere you may want to read this brother.!
 

Attachments

Dingiswayi alimfundisha Tshaka Zuli vita!?..Hebu ngoja nirudi darasani..
Cc: Malcom Lumumba zitto junior hearly Elungata

Baada ya mama yake kumtandika rungu la kichwa moja ya wafanyakazi wa mume wake alitimuliwa na kurudishwa kwao.
Shaka akafukuzwa na kulelewa na chifu wa Mutethwa, huko ndiko alikutana na Dingswayo baada ya kuwa chifu wakaanza kuvamia vijiji na yeye alisaidia kabisa kwasababu Wazulu walimkataa kwa kusema amezaliwa nje ya ndoa kabla mama yake hajaolewa na chifu wa Wazulu. Hadithi ya huyu jamaa imekaa kama The Epic of Sundiata....!
 
Hata Daudi na Sauli walikuwa na bifu Kali kwa sababu Daudi aliwaua maadui wengi zaidi ya Sauli....cha kufurahisha ni kwamba mtoto wa Sauli Jonathan alimpa tafu kinoma jamaa Daudi wakati mdingi wake anamsaka...na akawa anamuibia na siri + mipango ya mshua kumhusu ye Daudi...hivyo haya mambo yapo tangu dahari... story ya Dingishwayo inapita humuhumu mwa wa Daudi na wa Sauli...
 
Mtoa mada in history we start with key figure tshaka anakumbukwa coz alileta effects zaidi ya dingshwayo huyooo soo hata kama alikuwa stident wa huyo mzee history ina mark mtu aliyeleta effect kubwa kumbuka NGUNI SPEAKING MIGRATION one of the factor ilikuwa shaka expansionism policy and his military strength and geniuness
 
Mtoa mada in history we start with key figure tshaka anakumbukwa coz alileta effects zaidi ya dingshwayo huyooo soo hata kama alikuwa stident wa huyo mzee history ina mark mtu aliyeleta effect kubwa kumbuka NGUNI SPEAKING MIGRATION one of the factor ilikuwa shaka expansionism policy and his military strength and geniuness
Nimekuelewa mkuu
 
Palantir
History haijawahi kuandika if shaka ali learn military technique za dingishwayoo laa hasha ila shaka alikuwa brave soja aliyepigana kwa weledi wa hali ya juu akiwa nomo soja. Ilaa tuna mwita genous due to fact that aliazisha new military technque kama scotch wisk, cow horn system , short stabbing spear zote hizi b4 never used among Nguni speaking pipo wajamen ukitaka maelezo for each npo masta wa history Tz. Keep in mind hakuna kitabu nliwahi kusoma eti shaka ali learn from someone his military geniuness. Over
 
Kwa maelezo hayo mtazamo wako unakubaliana kwamba Dingiswayo alimfundisha Tshaka vita ama walikuwa ally wakitegemeana!?..
Mhhhh Mkuu,
Tshaka kabla ya hapo alikuwa chini ya Chifu Jobe lakini hakuwa mwanajeshi mkubwa.
Aliajiriwa kama mwanajeshi kamili wa Mutetwa chini ya Godongwana (Dingiswayo) akiwa na miaka 23.
Hapa alikuwa hafahamiki na Godongwana na alifanya kazi kama mwanajeshi wake na akaja kupata Umaarufu sana alipopigana na Buthelezi ambapo wenzake walikaa nyuma ila yeye akaenda mbele kupambana na jeshi lote peke yake.
Hichi kitendo ndicho kilimfanya awe karibu na Dingiswayo ambapo baadae alimfanya awe kiongozi wa jeshi lake (Izisiwe) hapa wanasema ndipo alijiongeza sana na kutengeneza mbinu mbali mbali za kijeshi. Tshaka alikuwa ni mbunifu sana!

Sasa ikumbukwe kitu kimoja cha Muhimu,
Tshaka alikuwa ni mwanajeshi mbunifu (Military Genius) lakini mambo yote ya Siasa, Utawala na Biashara alijifunza kutoka kwa Dingiswayo kwasababu jamaa alikuwa anafanya Bishara hadi na Wareno huko Deloga Bay. Kama kujengwa Tshaka alijengwa wakati ni kiongozi wa kijeshi wa Mutetwa, ndiyo maana hata Baba yake Tshaka alivyokufa aliyeruhusu Tshaka arudi kule akachukue kiti alikuwa ni Dingiswayo. Alifahamu ukweli kwamba Baba yake Tshaka miaka ya nyuma baada ya kuambiwa kuhusu uwezo wa mtoto wake aliwatuma watu wamrudishe lakini akakataa, basi Dingiswayo alichukua huu mwanya ili kujijenga kisiasa. Wanahistoria wanasema alivyorudi kuwa Chifu bado alikuwa anajihisi kama yuko chini ya Mutetwa na ndiyo maana Dingiswayo alivyokuwa anauwawa Tshaka hakusaidia kwasababu alikuwa anataka awe huru.

Dr Donald Morris in The Washing of Spears anasema hivi:
"As a further result Shaka came to the direct attention of Dingiswayo, who at once recognized his qualities of leadership. He saw more in Shaka than a mere soldier: he saw a potential chieftain for the Zulus, who were far upcountry on the fringes of the Mtetwa hegemony, where they might someday serve as a buffer to more powerful clans to the north. Under his tutelage Shaka rose to command of the iziCwe and participated in the councils where the Mtetwa policy was hammered out".....(Page 29) -Hapo penye nyekundu ndipo pana mwangaza!

NB: Ndiyo Tshaka amefundishwa na Chifu Godongwana (Dingiswayo) kuanzia Diplomasia, Utawala, Jeshi, Siasa na Biashara. Na alifanya hivi akitegemea kwamba siku atampandikiza Tshaka awe kiongozi wa Wazulu na yeye atanue himaya yake (exposure yote ya Tshaka aliipatia kutoka Mutetwa sema yeye akajiongeza kama kiongozi)

CC: LIKUD
 
Palantir
History haijawahi kuandika if shaka ali learn military technique za dingishwayoo laa hasha ila shaka alikuwa brave soja aliyepigana kwa weledi wa hali ya juu akiwa nomo soja. Ilaa tuna mwita genous due to fact that aliazisha new military technque kama scotch wisk, cow horn system , short stabbing spear zote hizi b4 never used among Nguni speaking pipo wajamen ukitaka maelezo for each npo masta wa history Tz. Keep in mind hakuna kitabu nliwahi kusoma eti shaka ali learn from someone his military geniuness. Over

Mfalme Tshaka Zulu aliweza kufanya yale aliyoyafanya kwasababu mengi alijifunza kutoka kwa Dingwisayo.
Sema yeye kama mwanajeshi alijiongeza sana na kuleta mbinu mpya ambazo zilimfanya Dingwisayo ampandishe cheo kwenye vikosi vyake. Mengi aliyojifunza Tshaka kutoka kipindi hiki ndiyo yalimfanya ajenge utawala imara sana aliporuhusiwa na Dingwisayo kwenda kuwa Chifu wa Wazulu. Ni sawa na kusema kwamba Mfalme Alexander Mkuu wa Makedonia (Alexander the Great of Macedonia) asingefanya yale aliyoyafanya kama Baba yake Mfalme Philipo asingemwajiri mwanafalsafa mkubwa kwa wakati huo Aristotle amfundishe.

Aristotle alimfundisha Alexander kwa miaka kama sita hivi:
Mambo ya mwenendo wa nyota, Lugha (Kihebrania, kilatini, Lugha za Babeli, Kigiriki), Jiographia ya Upepo na Bahari, Mambo ya nyota, Kuumbwa kwa Ulimwengu na Sayansi ya vitu vya dunia, Siasa, Falsafa nk. Aristotle ndiye aliharibu hata mawazo ya Mfalme Alexander kuhusu wanawake, kwasababu yeye binafsi alikuwa anaamini wanawake ni binadamu nusu.
Hivyo akashauri Alexander ajitenge nao na ndiyo maana kuna baadhi ya wanahistoria wanasema alikuwa anafanya Ushoga na Binadamu (Well this is till debatable)..Lakini katika maisha ya Alexander bahati mbaya sana Aristotle huwa hata hakumbukwi na watu tunaamini tu kwamba alitokea akawa na akili ile (Hell No)

NB: Hoja hapa ni kwamba,
Haata kama utakuwa mbunifu kiasi gani, kuna sehemu lazima utafundishwa tu. Hasahasa linapokuja suala zima la Utawala na mambo ya vita..Ukisoma vizuri historia ya viongozi wakubwa wengi hapa duniani "Mentorship is one of the key ingredient in their Success", lakini bahati mbaya sana wale wanaotokea kuwafundisha huwa hawakumbukwi au hata kufahamika. Ukisoma sana vizuri historia utakuja gundua hata Yesu alikuwa ni msomi sana na alifundishwa kweli kweli na akafundishika tofauti na mambo ambayo tunayajua.

CC: LIKUD
 
Malcom lumumba
Swali ndo linakujaa if xo kwann dingishwayoo haandikwi kama shaka zulu
 
Malcom lumumba
Swali ndo linakujaa if xo kwann dingishwayoo haandikwi kama shaka zulu
Anaandikwa sana tu,
Hakuna kitabu ambacho utazungumzia maisha ya Mfalme Tshaka Zulu bila kumzungumzia Mfalme Godongwana au Dingiswayo (The Troubled one). Sema tu mitaala yetu ya Historia ina walakini mkubwa sana sana: Hebu jiulize kwanini Mzee Nyerere (Baba wa taifa) anaandikwa peke yake kama shujaa wa nchi na kudai Uhuru wakati kulikiwa na wazee wengine waliosaidia kudai Uhuru wa Tanganyika ??? Mkuu tusipojiongeza kusoma na kufundisha watoto wetu kuna vitu vingi vya msingi kuhusu Historia ya Afrika vitatupita. Hivi umewahi hata kuangalia Syllabus ya Historia ya O-Level na A-Level ??? Haiko vizuri kabisa kabiaaa na mambo ya msingi wameyatupa tu.....
 
Malcom lumumba
Naskia BON MWAITEGE alikuwa dancer wa JANGALASON leo ana mafanikio zaid ya boss wake wa kipindi hicho sasa in HISTORY n kipi kinaandkwa aliyefundsha au aliyefundshwa akafundshka kupita maelezo

Kuna kitabu cha kingeleza kimeandkwa king crossed ze river lkn mfalme so yeye ndo wa kwaza kuvuka mto kwann mwandsh aliandka king crossed ze river wakat watu weng b4 walivuka (hapa nmekumbuka juz kat kingwangala kavuka kamfereji ka maji ... Habar mitandaon WAZIRI AVUKA MTO KWENDA KUONA MIPAKA ILIYOSOGEZWA) soo jiulize n mda gan historia huaza kuandkwaa
 
Malcom lumumba
N kwel dingishwayooo kandkwa ila hajapewa uzto mkubwa km jbaba tshaka. Kuhusu mitaala n kwel tz tuna shda ilaaa history somehow imeazia in grassroot mr kutoka kusoma history of river queen in england to mkwawa of hehe. Mirambo. Etc
 
Malcom lumumba
N kwel dingishwayooo kandkwa ila hajapewa uzto mkubwa km jbaba tshaka. Kuhusu mitaala n kwel tz tuna shda ilaaa history somehow imeazia in grassroot mr kutoka kusoma history of river queen in england to mkwawa of hehe. Mirambo. Etc
Wewe ukiwasoma The Plantagenet wa The War of Roses au Henry The Great halafu ukaacha kuwafundisha watoto vizuri kuhusu wakina Tewodros The Great, Mirambo, Quuen Anna Nzinga, Ramesses na Mkwawa unategemea utajenga kizazi kinachofurahia Uafrika kweli ???

NB: Hivi nikikuuliza leo,
Kwamba unajua aliyepigana vita nyingi za Mtemi Mkwawa wa Uhehe dhidi ya Wamassai kule Morogoro hadi kupelekea Mkataba wa Amani alikuwa ni dada (Mwanamke) yake unaweza ukawa na Ufahamu kuhusu hili ??? Lakini jiulize tu kwanini huyajui haya na wala hujafundishwa darasani ??? (Yapo tu kwenye Maktaba za Waingereza yamekaa tu)
 
Yeboooosa, shaka nae mbwembwe zote bt aliishi miaka 40 tu
 
Malcom lumumba
Nmependa mwendo huu sasa tuambie kwann unazan some history or events hufichwaaa
 
Back
Top Bottom