Kwanini Diamond ni bora kuliko Kiba

Paul S.S

JF-Expert Member
Aug 27, 2009
6,402
3,242
Kama leo yakifanyika mashindano ya BSS au Tusker project fame na mengineyo kama hayo, na washindani wakabaki wawili Diamond na Kiba basi nahakika pasi na shaka Alikiba ataibuka mshindi kwa maana ya kujua kuimba vizuri na sauti tamu.

Lakini kwenye soko la ulimwengu wa muziki kujua kuimba vizuri na kuwa na sauti tamu pekee hakukufanyi ukafanikiwa kimuziki,
Siri ya muziki ni mwanamuziki kujua wapenzi wa muziki wanataka nini na uwafanyie nini ili wapende wanachokisikia na wanacho kiona kutoka kwa mwanamuziki.

Diamond anajua wapenzi wa muziki wanataka nini kutoka kwake, anajua awafanyie nini wamjue, anajua aimbe nini, anajua atengeneze video za vipi awakamate wapenzi wake, anajua aishi vipi kuwateka akili washabiki wa muziki.

Zaidi ya hayo anajua apanue vipi wigo wa muziki wake kwa kufanya nini.

Kiufupi Diamond ni bingwa wa mikakati endelevu. Anajua kutumia kila nafasi anayoipata kuhakikisha ina mboost kimuziki bila kujali anatumia gharama kiasi gani wala watu wanasema nini kuhusu yeye.

Una weza kudhani Diamond anafuja pesa kuwasambaza mameneja wake kila kona nje na ndani ya nchi kwenda kusambaza CDs zake za nana wakati unaweza kumrushia mtu hata aliyeko USA kwa whatsap na akaipata.

Unaweza ukamuona mjinga kwenda kwenye shows na msafara wa team yake yenye mameneja, camera man mlinzi nk nk ukadhani anachezea pesa.

Unaweza ukadhani ana date na watu maarufu bahati mbaya ina tokea tu.

Unaweza ukadhani anajikomba kwa wasanii wakubwa wa naijeria na Godfather SA kuwalipa pesa kufanya nao kolabo na videos
Unaweza ukadhani ana ringa kwakuwa haonekani viwanja na kujichanganya na "wenzake" sijui bilz mara escape one mara kule, yeye ni ndani tu, au kukataa kolabo na wasanii hovyo au kuhudhulia show mbuzi.

Unaweza ukamuona mjinga ku expose maisha yake kwa show off kibao za maisha yake

Kwa ufupi hii ndio inaitwa mikakati ya ushindi na mafanikio

Kuna watu wanaweza kudhani mameneja Fella na Babu tale ndio nguzo ya kuu kabisa ya mafanikio ya Diamond,.

Kimsingi huwezi kusema Fella na Tale hawahusiki, lakini ni mwanamuziki mwenyewe ndio msingi mkuu wa mafanikio yake.

Mwanamuziki akijitambua basi mameneja ni kama bonus tu kwenye mafanikio yake.

Niliyoyataja hapo juu ndio ambayo kimsingi Ali Kiba anayakosa.

Tofauti yao kubwa ni kwamba ALI KIBA ANACHOJUA YEYE NI KWAMBA ANAPENDWA TU NA WANAO MFAHAMU HATA IWEJE, WAKATI DIAMOND YEYE ANACHOKIJUA NI AFANYE NINI ILI APENDWE ZAIDI HADI NA WASIO MFAHAMU.

Ndio maana leo hii almost all over the continent Diamond ni jina kubwa kimuziki na Ali Kiba atabakia kupendwa kwenye Fiesta na East Afika kidogo.

Alikiba ni kama haoni wala hasikii vile sababu tayari anao mtaji mkubwa sana wa mashabiki wake Tz lakini sasa hana mikakati yoyote endelevu.

Mwana ni moja ya nyimbo nzuri sana, ailikosea kuitoa na video ikaja baadae sana na matokeo yake sote tunayajua.

The video was amazing lakini tatizo watu walisha tengeneza video zao vichwani kwa karibu miezi kadhaa wakati wana usikiliza na kuucheza, so inapotoka video wanakuta tofauti na badala kuifurahia wanaanza kuikosoa kulingana na maono yao.

Kana kwamba hajui alikosea Kiba karudia yale yale, katoa hit kali cheketua lakini tunaenda mwezi wangapi sijui huu bado video ni kitendawili......... He is not serious

Sijawahi ona mwanamuziki anapendwa namna hii kama Kiba hadi wapenzi wake eti wanampigia magoti awafanyie nini.

Ali kiba is so predictable, yaani hivi sasa unajua kabisa anahangaikia video ya cheketua, mara nimeibiwa mara soth africa machafuko........ Comon guyz.

Nani alijiu nana inakuja? Nasema nawe je? Lini unajua ft p squre ipo tayari au vp?

Kiba hajui hata kucheza na akili za mashabiki wake kabisa.

Nenda page ya insta au fb au tweeter uwone Diamond anavyo wakatisha viuno followers wake all over the world, hadi utapenda isee
Nenda kwa Kiba sasa, daah.

Akipost picha wapenzi wanamuomba tafadhali tutolee kichupa cha cheketua king.

Imefikia eti video ya mwana ikichezwa tv kubwa leo wapenzi wako wanafungua na thread kabisa!!!!!! Unawatesa sana washabiki wako kiba

Alikiba ana niboa sana sababu najua anakitu kikubwa anaweza fanya lakini habebeki.

Nilicho kuja kugundua pengine washabiki wake wanamlemaza.

Naamini akiona wapenzi wake wote wanamkazia na kumwambia ukweli atashtuka kuliko kukalia kumsifia ujinga eti unaweza

Mwisho Kiba kumbuka huu mpambano uliuanzisha mwenyewe ulipozindua Mwana dsm kwa kudai umekuja kuchukua ufalme wako.

Lakini kama ufalme wenyewe ndio huu basi kuna haja kubwa sana ya kuacha kabisa kumlinganisha na kuwapambanisha kiba na mondi maana utakuwa sio mpambano fair.

Cc; aione kiba mwenyewe au mameneja wake
 
Ngoja niagize kitu ya bariiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiidi niwe nasoma kometi za watu wanavyotoka mapovu
 
Tofauti yao kubwa ni kwamba ALI KIBA ANACHOJUA YEYE NI KWAMBA ANAPENDWA TU NA WANAO MFAHAMU HATA IWEJE, WAKATI DIAMOND YEYE ANACHOKIJUA NI AFANYE NINI ILI APENDWE ZAIDI HADI NA WASIO MFAHAMU
Ndio maana leo hii almost all over the continent Diamond ni jina kubwa kimuziki na Ali Kiba atabakia kupendwa kwenye Fiesta
na East Afika kidogo

+Ally ni mvivu mno kutanua Fan base yake yeye anaridhika mapema sana na die hard fans alionao.

+pia kwenye kujitangaza yupo nyuma sana. Music umebadilika sana siku hizi umekua biashara, abadilike!
 
King Kiba ndo habari ya mjini kama hutaki endelea kucheza cheketua.
 
Kiba mpuuzi sana aisee huyu jamaa, tatizo ni kama hajitambui sababu tu kuna watu wanampenda hata asipotoa wimbo kiaka 10 watamsifia ndio king

Yaani cheketua huu mwezi wa 3 sijui bado hajatoa video yake?
Kuimba anajua sijui anataka nini sasa, anaboa kichizi

Jana alikua na show usa page zake kwenye social media kimyaaaaaaa
Watu wanapigana vikumbo kumuomba awapostie show ilikuaje ya kakalia anakula baga tu
 
hahahaha huyu kiba huyu, hiyo video ikitoka tutashuhudia thread zisizo na idada humu
 
Achana na Nassib Abdul, wenye chuki binafsi watazidi kuumia jamaa anajua.
 
Achana na Nassib Abdul, wenye chuki binafsi watazidi kuumia jamaa anajua.

Yaani mimi tangia video ya Nana itoke basi tena!!nimefatilia sana jinsi mameneja wake wanavyopeleka video nchi mbalimbali Africa,jinsi video ilivyopokelewa na mataifa mbalimbali kwenye vituo vyao vya tv na mitandao ya kijamii

Nimetafakari kwa umakini sana,NASSIB kumfananisha na Msanii mwingine nitakuwa nimemdhalilisha sana diamond kwa hapa bongo hana mpinzani,nasema Notounfaircompetition!!!
 
Back
Top Bottom