Kwanini Dereva wa Lissu akimbizwe Nairobi?

Kwanini Dereva wa Lissu akimbizwe Nairobi?

Kwa mwendo huu wa kukimbiza mashahidi inatia wasiwasi hata kama ni kweli Lissu amepigwa risasi.
 
nijuavyo mimi dereva wa lissu ndio first suspect. yaani ndio angekuwa mtu wa kwanza kuhojiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
lakini wakamuacha bila kumuhojii....sio tatizo lake polisi walishindwa kutumia akili kwanini wasingemuhoji yeye wa kwanza nani aliliona gari lilikuwa linamfuata?kwanini wakati wapo hospital wasingemchukua na mwenyekiti au mwanasheria wa chama na kwenda kumuhoji na kuanza kufuatilia...haya maelezo ya ilikuwa Nissan hatujui hata nani kasema,sijui walilaza kiti,sijui alimwambia asishuke kwenye gari hatuna uhakika nani alisema....inaweza kuwa kama ya Roma alitekwa na NOAH mwishoni mwenye tukio anakwambia sio NOAH ni SURF
 
Kwanini Lumumba mnamtaka dereva? mnataka kumuua? na kwanini muumize kichwa namna hii?

Kila mtu anajua mikono yenu imejaa damu, ngojeni warudi wamwage data Tundu Lissu sio Roma wa kuandaliwa press na Zamaradi Kawawa ataandaa mwenyewe na kusema kila kitu hata kama Bashite alionekana kwenye Nissan au alikuwepo Dodoma siku hiyo itajulikana.
 
Kuna mambo mengi yapo nyuma ya pazia ya hili suala.dereva kapelekwa kenya?asee,me sijui ila mengi yatafunuka.awamu ya magufuli.ofisi ya raisi imekuwa na nguvu hakuna mtandao wowote unaomtingisha magufuli.lakini pamoja na hayo bado suala la usalama malizeni uchunguzi haraka mseme ukweli wote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mmewakamata hao wadunguaji,au kuropoka ropoka tuu?
 
Hata hivyo, licha ya Jeshi la Polisi kufanya jitihada kubwa za kumtafuta dereva huyo, viongozi wa CHADEMA wanafanya juhudi kubwa ili dereva huyo asihojiwe kabla ya Lissu hajaruhusiwa kutoka hospitali.
"Kama jambo haulijui, haujalishiriki bora unyamaze. Kutunga uongo au kuandika sana ili uonekane unajua kufikiri dhidi ya uhalisia hakutasaidia upelelezi wala haki kuonekana ikitokea. Tuwe watulivu katika kipindi hiki ili haki itendeke",
 
Kwa mwendo huu wa kukimbiza mashahidi inatia wasiwasi hata kama ni kweli Lissu amepigwa risasi.
wana mkimbiza kwa sababu watu waliowakamata mwanzo walikuwa usalama wa Taifa unadhani wakimuacha si watampa kesi tu,,,,,,labda waliompiga risasi ni walewale aliowataja Lissu mwanzoni
 
We mtoa post pia unahaha kuona mbinu zenu kila kukicha mnafeli
 
lakini wakamuacha bila kumuhojii....sio tatizo lake polisi walishindwa kutumia akili kwanini wasingemuhoji yeye wa kwanza nani aliliona gari lilikuwa linamfuata?kwanini wakati wapo hospital wasingemchukua na mwenyekiti au mwanasheria wa chama na kwenda kumuhoji na kuanza kufuatilia...haya maelezo ya ilikuwa Nissan hatujui hata nani kasema,sijui walilaza kiti,sijui alimwambia asishuke kwenye gari hatuna uhakika nani alisema....inaweza kuwa kama ya Roma alitekwa na NOAH mwishoni mwenye tukio anakwambia sio NOAH ni SURF

Rejea hotuba ya polisi hawajamuona huyu mtu wanamsikia kwenye magazeti.
 
Tuwaze kama ni watu wenye akili,
Lissu kabla ya tukio hili alilalamika kuna gari inamfuata na akatoa namba kabisa,Je police walifanyia kazi?
kama kweli tupo siriasi tuanze na hawa police kwanini hawakuchukua jukumu la kufuatilia ni akina nani wanamfuatilia lissu kabla hatujaja kwa dereva,dereva awe wa afuate baada ya kupata majibu toka kwa police kilichowafanya wasichukue hatua hadi lissu anapigwa,

kama tuna akili lakini ndo tijiulize hayo maswali ila kama sie ni mazwazwa basi tuanze na dereva maana akili zetu zipo makalioni
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Dereva wa Tundu Lissu ni suspect number one kutokana na jinsi alivyojichanganya wakati akieleza jinsi Lissu alivyopigwa risasi. Maelezo yake yanatia shaka hali inayofanya hata wasio na kiwango cha phd kuweza kubaini nini kimetokea.

Hata hivyo, licha ya Jeshi la Polisi kufanya jitihada kubwa za kumtafuta dereva huyo, viongozi wa CHADEMA wanafanya juhudi kubwa ili dereva huyo asihojiwe kabla ya Lissu hajaruhusiwa kutoka hospitali. Baadhi ya viongozi wa CHADEMA nilioongea nao wana maoni kuwa, kumrelease mapema dereva huyo kwa vyombo vya dola kunaweza kubadili mwelekeo wa sakata hilo.

Ikumbukwe kuwa dereva huyo ana Miezi miwili tu tangu apewe jukumu la kumuendesha Lissu anbapo kabla ya hapo alikuwa dereva wa Makao Makuu ya CHADEMA Kitengo cha Ulinzi wa Viongozi wa chama hicho. Dereva huyo alipewa kumuendesha Lissu ikiwa ni jitihada za chama hicho "kuimarisha ulinzi" wa kiongozi huyo kwa kuwa mlinzi huyo amepewa mafunzo ya Ngazi za juu katika ulinzi wa viongozi, mafunzo aliyopata nchini Israel.
MMetaka kumuuwa Lisu na mmeshindwa.Yule dogo ni ndugu yake lissu .na amekuwa akimwendesha Lissu mika zaidi ya saba..Sasa sijui propaganda zenu zinasaidia nini
LISSU hatakufa na atarudi kuwaumbua zaidi
kwa hili CCM mnalo..
 
Back
Top Bottom