Kwanini Dar-es Salaam tu,tena Ubungo Bus terminal tu?

Kwanini Dar-es Salaam tu,tena Ubungo Bus terminal tu?

Nimekuwa nikijiuliza sana swali hili kuhusu dar-ubungo bus terminal,ni kwanini watu wanalipishwa pesa kuingia ndani ya stendi pindi wawasindikizapo ndugu ama jamaa zao na wakati mwingine hata wao wenyewe ikiwa hawakukata tiketi?
Mbona mtu anaweza msindikiza nduguye airport na asichajiwe pesa,au airport na ubungo, au ubungo ndio yenye thamani zaidi?
Mbona stendi zingine za mikoani hawatulipishi pesa kama hizo? Arusha,Mbeya,Mwanza na Tanga hakuna gharama kama hizo kwanini dar tu? Ni nani hasa mnufaikaji wa mradi huu ambao gharama zake hupanda kila siku? Kuvuka kigamboni ni sh.200 lakini kuingia ubungo tu ndani mule ambapo hakuna gharama yeyote ambayo halmashauri inaingia kwa wewe kumpeleka ndugu yako pale unalipia sh.300 kwa sasa,Serikali nayo imekuwa kinara wa kutuibia raia wake? Magufuli hulioni hili nalo kuwa kero kwa raia? Mradi huu hauna tija bali ni wizi ambao tumekuwa tukiibiwa kwa muda mrefu sana.
Tanzania ni nchi yetu sote jamani msitushike kila mahali.Kwanini ubungo,na pesa za hapo zinapelekwa wapi?
Ubungo mnatuibia sana aisee,maana katika stendi nyingi huwa vyombo vya usafiri ulipishwa na raia kutumia bure miundo mbinu iliyopo hapo,Kulikoni Ubungo bus terminal?
Kwa daraja la kigamboni mlisema kuwa sehemu nyingi duniani hilo ufanyika,naomba kujua kama kuna sehemu duniani wanalipisha raia wake kwa kuingia na kutoka katika stendi ya mabasi.
Kwa wenye majibu na maswali mengine zaidi huenda tukapata ukweli wa gharama hizi naomba tufahamishane wakuu.
Asante.
Halafu ni basi terminal yenye ingekuwa na hadhi kidogo au hata sehemu ambayo mtu anaweza kupumzika na kustarehe. Stendi ya jiji la kwanza kwa ukubwa nchini bado ni ya VUMBI halafu CHAFU na hata sehemu za kupumzikia mgogoro! Hii tozo ingewekwa stand ya Iringa mimi ningeridhika kabisa.
 
Wanajaribu kupunguza wasio na kazi na vibaka wasifanye pale ndio sehemu ya kwenda kufanya mipango yao ya uovu,japo hawajaweza kutimiza azma yao hiyo kwani vibaka ni wengi na wauza bangi na wasio na sehemu za kulala ni wengi sana mle ndani.
Kibaka na muhalifu yeyote yupo kazini, 200 haimshindi. Kama lengo ni hilo pesa zinazotozwa zinafanya kazi gani maana terminal bado ni ya ajabu mno kwanza ni CHAFU.
 
VIP Lounge iongezwe maana iliyopo ni ndogo sana yaani mkiingia watu 20 imejaa tayari
 
Back
Top Bottom