mchovu wa fikra
JF-Expert Member
- Jul 16, 2016
- 335
- 393
Nimekuwa nikijiuliza sana swali hili kuhusu dar-ubungo bus terminal,ni kwanini watu wanalipishwa pesa kuingia ndani ya stendi pindi wawasindikizapo ndugu ama jamaa zao na wakati mwingine hata wao wenyewe ikiwa hawakukata tiketi?
Mbona mtu anaweza msindikiza nduguye airport na asichajiwe pesa,au airport na ubungo, au ubungo ndio yenye thamani zaidi?
Mbona stendi zingine za mikoani hawatulipishi pesa kama hizo? Arusha,Mbeya,Mwanza na Tanga hakuna gharama kama hizo kwanini dar tu?
Ni nani hasa mnufaikaji wa mradi huu ambao gharama zake hupanda kila siku? Kuvuka kigamboni ni sh.200 lakini kuingia ubungo tu ndani mule ambapo hakuna gharama yeyote ambayo halmashauri inaingia kwa wewe kumpeleka ndugu yako pale unalipia Sh.300 kwa sasa,
Serikali nayo imekuwa kinara wa kutuibia raia wake? Magufuli hulioni hili nalo kuwa kero kwa raia? Mradi huu hauna tija bali ni wizi ambao tumekuwa tukiibiwa kwa muda mrefu sana.
Tanzania ni nchi yetu sote jamani msitushike kila mahali.Kwanini ubungo,na pesa za hapo zinapelekwa wapi?
Ubungo mnatuibia sana aisee,maana katika stendi nyingi huwa vyombo vya usafiri ulipishwa na raia kutumia bure miundo mbinu iliyopo hapo,Kulikoni Ubungo bus terminal?
Kwa daraja la kigamboni mlisema kuwa sehemu nyingi duniani hilo ufanyika,naomba kujua kama kuna sehemu duniani wanalipisha raia wake kwa kuingia na kutoka katika stendi ya mabasi.
Kwa wenye majibu na maswali mengine zaidi huenda tukapata ukweli wa gharama hizi naomba tufahamishane wakuu.
Asante.