Kwanini daladala nyingi za Dar ni mbovu? Tatizo ni nini hasa madereva au wamiliki wa magari hayo?

Abdul mndili

Senior Member
Oct 15, 2016
192
137
Habari wakuu nikiwa natoka point A kwenda point B hili daladala nililopanda limekamatwa zaidi ya mara 5 na traffic njiani... na kila traficc akikagua anasema gari ni bovu...maana huku kusimamishwa safari ya lisaa limoja yamekuwa masaa mawili na nusu.
 
Habari wakuu nikiwa natoka point A kwenda point B hili daladala nililopanda limekamatwa zaidi ya mara 5 na traffic njiani... na kila traficc akikagua anasema gari ni bovu...maana huku kusimamishwa safari ya lisaa limoja yamekuwa masaa mawili na nusu.

Sheria mbovu, usimamizi mbovu unapelekea kuwa na magari mabovu barabarani.
 
Walioshindikana kitabia na kimaadili ndio waendesha magari haya. Wao don't care uzima wa gari wala abiria waliowabeba hivyo usitegemee kama watajali. Pia, kwa kuwa gharama za matengenezo ya magari normally hazitokani na kipato chao, so usitegemee watakuwa wanajali.
 
Umaskini...unaleta usimamizi mbovu....mwenye gari anatafuta hela ya kula, kondakta hela ya kula, dereva hela kula, bado trafik nae anataka hapo hapo... bado serikali na sumatra......gari linasahaulika kutunzwa...kama linawaka na kutembea basi lilende lirudi.

Mfano.. angalia bus za kilimanjaro express...bus zake ni namba A bado zinaonekana mpya ina maana anajali gari zake ..sio iende irudi..anarudisha asilimia ya mapato kutunza gari zinazomwingiza hayo mapato. Angalia magari ya UDA yote nyang'anyang'a sidhani kama alikuwa anarenga hela ya kuhudumia magari ukiacha kuhakikisha linawaka na kuweza kwenda na kurudi.

Madereva pia hawatunzi magari hawajali likiharibika atahamia gari nyingine.
 
Mengi yanakuwa yameshatupwa na wamiliki wa awali hivo wanayokuwa nayo wanakuwa wanagangaganga
 
Back
Top Bottom