Kwanini Chato?

Nahisi akishaondoka, miundo mbinu ya huko inaweza kususiwa kwa chuki za roho hizi, na kwa kuwa imezungukwa na wanyonge masikini wasioweza hata kukata tiketi ya ndege watapasusia yawe magofu.
Na inawezekana ajaye akainyang'anya hadhi na kurudisha serengeti wanyama waliohamishwa.
Najifunza kitu hapa, kujenga chuki ni rahisi sana kuliko kujenga mapenzi na watu
 
Safi sana, kila siku wazungu wanaenda kaskazini/Manyara/Serengeti Mbona hatusemi bwana.. Peleka Simba, Tembo, Chui, twiga, sungura, Koboko, nyumbu, nungunungu na Serengeti yote tunahamisha.

Wazungu watatua Chato Airport straight from USA/LONDON/SPAIN/ISRAEL Kuja pale Chato National park wakimaliza hao wanakwea dream liner letu Air Tanzania..CDM wanapata taabu na ndugu zao ACT hahahhaha
 
 
Hifadhi inayoitwa Chato haipo na haijawahi kutajwa kwenye gazeti la Serikali!.. Mapori yaliyopandishwa hadhi ni matano ambayo ni > Biharamuro, Burigi,Kimisi, Ibanda na Rumanyika....kuwa Hifadhi za Taifa!... Hakuna hifadhi inayoitwa Chato!!! 😳 😳
 
mnasumbuka na vitu vidogovidogo na vya kijinga sana,vitu ambavyo hata vikiwepo havina athari kwa taifa kiuchumi,kisiasa,kijamii,kitamaduni wala kiusalama,mkoa wa simiyu ulipewa jina hilo kutokana na sababu zipi???kwann hauhoji pori la hifadhi linaloitwa maswa kuwepo meatu wakati hizi ni wilaya mbili tofauti???kwani hiyo hifadhi inhepewa jina la shangazi yako kama taifa tungekuwa na cha kuongeza au kupunguza????yaani nyie watu mnakera makusudi siku zingine,haya basi ww ukitaka kurefer jina la hiyo hifadhi tumia la baba yako ili usikereke
 
Chattle International Airport na ile ya bwagamoyo inaamia pale; mbuga mpya za wanyama zimeanzishwa baada ya kujenga airport, subiri mkoa wa Chattle kama hupendi, na kadhalika.
 
Sasa unaambiwa Hifadhi itaiwa Burigi/Chato. Lengo iitwe Chato, labda kaoa aibu kidogo.
Inatumika kuhalalisha ujenzi wa Chato International Airport.
 
Sisi sote ni watanzana haijalishi iitwa Chato au laah, mbona Tanzanite inachimbwa Manyara lakini soko lipo Arusha? Hifadhi ya Tarangire na Manyara zipo mkoa wa Manyara lakini ofisi zote za kitalii zipo Arusha na sio Babati ambaye ndio makao makuu ya mkoa wa Manyara.
 
SHANGAAA!
Serengeti National Park kwa asilimia kubwa inapatikana mkoa wa Mara lakini mapato kwa asilimia kubwa ni Arusha.
Arusha kumekaa kitalii maana lile ni jiji tofauti na Mara ambayo imekaa kikijiji kijiji hakuna sehemu ya kula bata na sehemu za kurefresh. Arusha kinachoipaisha ni wakazi wake ni ma hasla wanajituma kwenye utalii mfano magari, curio, tents, baloon, hotels etc sasa hawa Harooo wamelala wao ni kukatana mapanga
 
Hivi unaelewa ulichoandika kutokana na mada au umekurupuka...!! Ukitaka habari za mapanga hazisha mada ya wameru, wamasai, wakulya, wangoreme nk...
 
Hivi unaelewa ulichoandika kutokana na mada au umekurupuka...!!
Hivi hushangai mpaka naniliu hataki kwao Singida anatakaa Arusha yule aliyekuwa waziri

Anyway nina bia kichwani sasa hivi zinapanda taratibu tusameane tyuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…