Ngoja niwape Siri,chakula Cha msibani kinapikwa na wataalamu wengi(wananzengo) Kila mmoja ana ufundi wake ndio maana wamama wapishi wanatoa kitu kikali,tofauti na mama junia nyumbani anapika pilau kama anapika kandešš, lakini pia nyenzo/vifaa vya upishi mara nyingi ni natural yaani ni Kuni au mkaa,na chakula cha kwenye mkaa/Kuni ni tofauti na kwenye gesi au umeme ambapo wengi huwa tunatumia majumbani.Tuheshimu asili Mimi huwa naenda kwa mama yangu ananipikia mboga ya kwenye chungu na ladha inakuwa tamu tofauti na inayopikwa kwenye sufuria au rice cooker na wife nyumbani.Yaani kiufupi tu teknolojia imesababisha tunakosa ladha ya chakula iliyotukuza kwenye makuzi yetu