Kwanini CHADEMA mmetunga na mnasambaza uzushi wa ukabila wa Hayati Magufuli?

Nimekuwa nikisikia hizi maneno ama uzushi wa maneno kua Hayati Magufuli ni mkabila, ana upendeleo wa Wasukuma, mara hili mara lile.

Uzushi huu umekuwa ukipigiwa chapuo na watu wa kanda moja lakini pia uzushi huu umebebwa na Chadema kama mojawapo ya tuhuma dhidi ya Magufuli.

Leo kwenye press, mwenyekiti wa Chadema Bw. Mbowe amesisitiza kwenye mabaya ya Hayati Magufuli kua alikua na upendeleo wa kindugu(neportism). Kwa maana kwamba Magufuli alijaza ndugu zake na jamaa zake kweye taasisi za serikali na vyombo vya dola kwa upendeleo wa undugu na ukabila.

Kwa Dunia hii ya teknolojia, nilitegemea Chadema na wenzake walete ushahidi wa numbers, mfano, Wakurugenzi wa Halmashauri wako 250, Wasukuma wako 80, ama wakurugenzi wa mashirika ya umma wako 200, wasukuma wako 100, ama wakuu wa vyuo vya serikali wako 50, wasukuma ama ndugu zake na Magufuli wako 20.

Ama nilitegemea Chadema waje na takwimu za mawaziri wako labda 30, wasukuma 12, labda majaji nchi nzima wako 100, wasukuma wako 40.

Wangekua na hizo statistics hapo unaweza kufanya analysis na ukasema kweli kuna ukabila na upendeleo ama kweli Magufuli alikua mkabila na mwenye upendeleo wa kindugu kwenye kutoa nafasi.

Nashindwa kuwaelewa Chadema, hoja ya ukabila na upendeleo wa Magufuli uko kwenye kitu gani? Kwa nini chama kama Chadema waamue kutunga uzushi kama huu usio na ushahidi wowote na waupigie debe hadi kwenye vyombo vya habari?

Kwa nini Chama mjikite kwenye kutunga na kusambaza uzushi kama huu?

CHADEMA, msisahau tunajua ukabila mlionao kwenye CHama, kuanzia mwenyekiti, katibu mkuu, mkurugenzi wa fedha, mkurugenzi wa itikadi na wakurugenzi wote kua wa kabila moja.
Yaani mbowe hata aibu hana. Ukabila uko chadema maana sio uchaga tu hadi ni upendeleo wa wamachame. Kuhusu wasukuma kwanza hawa watu ni karibu 1/3 ya raia. Kwa hiyo ukiwaona kila mahali kwa wingi ujue wapo kwenye space ya nchi yao tanzania.
 
Ushahidi upo , mfano mmoja wapo ni zile ajira za mwaka Jana za ualimu, Nina Jamaa yangu ni sukuma, tumesoma kozi moja, kuapply nilimtangulia ,kumaliza shule nilimtangulia , gpa nilimshinda , ila yeye akapata ajira Mimi nikakosea ajira, Sasa kigezo kilichotumika mpaka yeye kapata mi nikakosa si ni ukabila ,yeye ni sukuma Mimi ni nyaki😀😀😀 ushahidi huo
Acha uongo some time kuna mapungufu pia kwenye application na ujue kuna vigezo tofauti na gpa pia.
 
Back
Top Bottom