BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,767
- 288,340
Mbona huyu anayechota pesa matrillions ya walipa kodi bila idhini ya Wabunge hujawahi kumkemea? Mbona hujawahi kumkemea kwa kutoa rushwa ya milioni 10 kwa kila mbunge pale Lumumba October 2016? Mbona hujamkemea alipokwapua rambi rambi za wahanga wa tetemeko kagera bilioni 16 na kuwaacha wakitabika!?
Tuliochangia na watakaochangia matibabu ya Lissu wanafanya hivyo kwa mapenzi yao kwa hiyo haikuhusu kitu na roho yako mbaya na wivu wa pesa ambazo hazikuhusu kitu.
Tuliochangia na watakaochangia matibabu ya Lissu wanafanya hivyo kwa mapenzi yao kwa hiyo haikuhusu kitu na roho yako mbaya na wivu wa pesa ambazo hazikuhusu kitu.
View attachment 584536
Wadau, amani iwe kwenu
Kwanza kabisa natoa pole kwa majanga yaliyomkuta Tundu Lissu. Ni wakati sasa kwa Watanzania kushkamana bila kujali itikadi zetu ili kumuombea Lissu apone. Pia tuwe na moyo wa subira ili tuviachie vyombo vya dola vitimize majukumu yake kuwasaka waliohusika na tukio hilo.
Pamoja na hayo, Nimesikitishwa sana na hii tabia iliyoanza kujengeka kwa viongozi wa CHADEMA pindi majanga ama matukio mabaya yanapotokea. Ilianza kidogo kidogo na sasa imekomaa na kuota mizizi.
Alipofariki Mzee Ndesamburo, CHADEMA walichangisha fedha kutoka kwa wanachama, wafuasi na marafiki wa chama hicho. Hadi leo hii hakuna hata senti iliyofika kwa familia ya mzee Ndesamburo.
Leo wameanzisha mchango wa kumsaidia Tundu Lissu ila hawajaainisha wanahitaji kiasi gani na kwa malengo yepi. Wanajua kuwa kiwango cha huruma ya watu kwa Tundu Lissu kwa sasa ipo juu na kwa vyovyote wakianzisha mchango wa kumsaidia watapata fedha nyingi.
Tukumbuke kuwa Tundu Lissu ni kiongozi wa CHADEMA ambacho kinawajibika kumsaidia pindi anapopata majanga kama wafanyavyo kwa viongozi wengine hasa wanaotoka Kaskazini. Kwa wasiojua, John Mnyika alipopatwa na ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu mwishoni mwa mwaka 2016, CHADEMA walimpeleka nchini Ujerumani kwa matibabu na hakuna mtu aliyechangishwa.
Lisu pia ni Rais wa TLS na miongoni mwa incentives za kuwa kiongozi wa chama hicho ni kupata matibabu bure.
Lissu pia ana bima ya afya ambayo inawajibika kulipa gharama za matibabu pindi anapopatwa na ugonjwa.
Vilevile Tundu Lissu ni Mbunge. Mtambue kuwa miongoni mwa taasisi zinazojali sana watu wake ni Bunge. Spika Job Ndugai amekaa siku nyingi India akipata matibabu kwa fedha za Bunge. James Mbatia naye katibiwa India kwa fedha za Bunge. Wapo wabunge wengi waliohudumiwa ipasavyo na bunge ambapo wengine wametangukia mbele ya haki.
Si kila kitu chadema inaweza kuchangisha. Hivi ile michango ya kumsaidia Precious Mawazo imefikia wapi? Mmepata kiasi gani na je zimefika kwa mlengwa?
Niwaombe wafuasi wa CHADEMA, kabla hamjaanza kumchangia Lissu, waulizeni kwanza mnachanga kwa madhumuni gani. Msiwe bendera fuata upepo