neo1
JF-Expert Member
- Sep 1, 2013
- 577
- 838
Habari wana jamvi,
Kwanza nampa pole ndugu Tundu Lissu kwa majanga yaliyotokea kwake. Kitendo kilochofanyika kwake sio sawa na haikubaliki kwenye jamii ya kidemocrasia na jamii ya kistaarabu. Pia ni kuharibu image ya taifa.Tunapishana kwa hoja. Lazima tujenge jamii inayosema na isiyo na uoga lazima viongozi wakubali kukosolewa lazima kuwepo na uvumilivu wa kisiasa.
CHADEMA ni chama kikubwa na pia chama kinapata ruzuku toka serikalini zaidi ya 500M kwa mwezi> nikikosea naomba kusahihishwa.
Kutokana na tukio la Lissu naona wanatembeza bakuli la kuchangiwa kwa matibabu ya Lissu.
CHADEMA wakati wa vugu vugu la njaa nchini mlisema kama serikali haitatoa chakula kwa wananchi mlisema mtawapatia chakula cha msaada wahitaji wote nchi nzima, leo wananchi wale wale mnawaomba mchango wa matibabu, hapo bado sijaona logic!.
Kwa nini msingefanya fundrising na kuweka target ya hela mnayotaka kwa ajili ya matibabu ya mh Lissu kwenye chama kuna watu wakubwa kama Lowasa, Sumaye ambao wangealika marafiki wachache mngepata michango mizuri!
Leo bunge limetoa nusu ya posho kwa kila mbunge jumla imepatikana 45M.
Je hizi mmezihesabu kwenu au kwenye matibabu ya Lissu! Je hela ya matibabu ya matibabu ikizidi na gharama ikawa ndogo kuliko mlichokusanya,je hela itaingia kwenye mifuko ya chama? Atapewa mhanga(Lissu) au ndo itakuwa imetoka. Je mtakuwa tofauti na serikali kwa ilochofanya Bukoba?
Je kweli CHADEMA ni chama cha matukio? Sasa mnaamua kutembelea tukio la mh Lissu kupata huruma ya jamii? Je policy yenu ni CHADEMA mtafanyia nini jamii au ni jamii itawafanyia nini CHADEMA. Pamoja kuwa hamna dola je mnafanya nini kuinua afya, elimu, maji, chakula kwa kaya, kuitangaza nchi kimataifa! Zaidi ya kulalamika?.
Zaidi ya yoyote sikubaliani na ombi lenu la kuchangiwa kwa matibabu ya mh Lissu unless mnataka kuanzisha mfuko kwa ajili ya kuhudumia wananchi maskini wasio weza kujihudumia kwa afya!
Tunajenga nchi moja tukubaliane na kupingana kwa hoja!.
Neo