Kwanini CHADEMA inachangisha hela ya matibabu ya Lissu?

Kwanini CHADEMA inachangisha hela ya matibabu ya Lissu?

nionavyo mimi viongozi wetu wa CDM wamelazimisha Lissu apelekwe nairobi kwa matibabu ili wapate michango wapige deal. kwani mpaka sasa ishapatikana zaid ya mil 70. wametumia vizuri ule msemo wa kiswahili unaosema 'pafiwapo ndio paliwapo'

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaaani wewe ni zaidi ya KILAZA maana hata picha Huelewi
"Sababu za kiusalama ndio zimemuamisha hapa"
 
Kwan umelazimishwa kuchanga? Ccm roho zinawauma Kuona watu wakichanga.
 
Madaktari wa Tanzania ndo waliokoa maisha ya Lissu...dakika chache baadae, chadema inatoa tamko kuwa madaktari wa Tanzania ni feki na hawaaminiki...hii sio haki kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona unaongea kama umetoka usingizini! Ulimsikiliza vizuri mbowe? Alisema hivi kilichowasukuma kwenda Nairobi sio kufuata ubora wa wataalamu hapana bali usalama na hofu ya watesi wao, kwakuwa tukio lenyewe limewaogopesha sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa post akili zako unazijua mwenyewe nawasiwas umelala hatahivyo ukiamka na akili zako zikirudi utagundua kuwa ulichoandika ni ujinga kwan hela zinazotolewa kwa moyo na wenye mapenzi na mtu wao zinakuumaje hebu watazania ifike muda tuwe waelewa na wamoja si

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tusiwe na mawazo hasi sababu ya tofauti za kisiasa. Kama CCM mnataka kufanya siasa na tukio la Lissu, basi mnajiweka pabaya zaidi maana watu wengi wanahisi kuna mkono wa serikali mnayoiongoza.

Lissu haumwi kama Ndugai, Mnyika, na Mbatia, bali kapigwa risasi na watu wasiojulikana na kwa Usalama wake, matibabu yake hayajafuata utaratibu wa hospital ya mkoa, hospital ya rufaa, Muhimbili na baadae rufaa ya nje ya nchi. Ndo sababu hakukuwa na nafasi ya bima ya Bunge. Haijulikan matibabu yatagharimu shiling ngap na Lissu atapona lini.

Wakati huu tujikite kwenye maswali ya msingi kama: je wauaji wamekamatwa? Gari iliyohusika(Nissan nyeupe) imekamatwa? Uhai wa Lissu utakuwa salama hata akipona?
 
View attachment 584536

Wadau, amani iwe kwenu

Kwanza kabisa natoa pole kwa majanga yaliyomkuta Tundu Lissu. Ni wakati sasa kwa Watanzania kushkamana bila kujali itikadi zetu ili kumuombea Lissu apone. Pia tuwe na moyo wa subira ili tuviachie vyombo vya dola vitimize majukumu yake kuwasaka waliohusika na tukio hilo.

Pamoja na hayo, Nimesikitishwa sana na hii tabia iliyoanza kujengeka kwa viongozi wa CHADEMA pindi majanga ama matukio mabaya yanapotokea. Ilianza kidogo kidogo na sasa imekomaa na kuota mizizi.

Alipofariki Mzee Ndesamburo, CHADEMA walichangisha fedha kutoka kwa wanachama, wafuasi na marafiki wa chama hicho. Hadi leo hii hakuna hata senti iliyofika kwa familia ya mzee Ndesamburo.

Leo wameanzisha mchango wa kumsaidia Tundu Lissu ila hawajaainisha wanahitaji kiasi gani na kwa malengo yepi. Wanajua kuwa kiwango cha huruma ya watu kwa Tundu Lissu kwa sasa ipo juu na kwa vyovyote wakianzisha mchango wa kumsaidia watapata fedha nyingi.

Tukumbuke kuwa Tundu Lissu ni kiongozi wa CHADEMA ambacho kinawajibika kumsaidia pindi anapopata majanga kama wafanyavyo kwa viongozi wengine hasa wanaotoka Kaskazini. Kwa wasiojua, John Mnyika alipopatwa na ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu mwishoni mwa mwaka 2016, CHADEMA walimpeleka nchini Ujerumani kwa matibabu na hakuna mtu aliyechangishwa.

Lisu pia ni Rais wa TLS na miongoni mwa incentives za kuwa kiongozi wa chama hicho ni kupata matibabu bure.

Lissu pia ana bima ya afya ambayo inawajibika kulipa gharama za matibabu pindi anapopatwa na ugonjwa.

Vilevile Tundu Lissu ni Mbunge. Mtambue kuwa miongoni mwa taasisi zinazojali sana watu wake ni Bunge. Spika Job Ndugai amekaa siku nyingi India akipata matibabu kwa fedha za Bunge. James Mbatia naye katibiwa India kwa fedha za Bunge. Wapo wabunge wengi waliohudumiwa ipasavyo na bunge ambapo wengine wametangukia mbele ya haki.

Si kila kitu chadema inaweza kuchangisha. Hivi ile michango ya kumsaidia Precious Mawazo imefikia wapi? Mmepata kiasi gani na je zimefika kwa mlengwa?

Niwaombe wafuasi wa CHADEMA, kabla hamjaanza kumchangia Lissu, waulizeni kwanza mnachanga kwa madhumuni gani. Msiwe bendera fuata upepo
Mnajaribu kuhamasisha watu wasichangie kwataarifa yenu tutachanga tu hata zikiliwa sio tatizo na wala haituumi tumeamua kuchanga wenyewe kwa hiari yetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lissu haumwi kama Ndugai, Mnyika, na Mbatia, bali kapigwa risasi na watu wasiojulikana na kwa Usalama wake, matibabu yake hayajafuata utaratibu wa hospital ya mkoa, hospital ya rufaa, Muhimbili na baadae rufaa ya nje ya nchi. Ndo sababu hakukuwa na nafasi ya bima ya Bunge

Kina Lizaboni walitaka mlolongo huu ufuatwe na in the process muda muhimu upotee na lengo kuu la wapiga risasi probably litimie. Kuchangia ni suala binafsi mno ambalo halihitaji mtu ashauriwe au azuiwe na mwingine.
 
Walimsema Mkuu kala rambirambi za kagera,,
Wao Mapemaaaaa!!wamemfanya ATM[emoji1321]
 
Buku Saba FC mmefunguliwa kuja kufanya propaganda kwenye shambulio la Lissu. Umasikini kitu kibaya, badala ya kuhoji kuhusu pesa, sisi werevu na tusio masikini tunahofia uhai wake baada ya kutoka hospitalini maana wabaya wake hawajakamatwa na huenda wasikamatwe kama kwa Roma, Bensaa8, Mwaikusa,n.k.
 
Rambi rambi za Kagera umekula za watoto Arusha umekula hizi nazo unataka wapokee mawazo yako ili uzile. Chama Cha Marambirambi
 
Back
Top Bottom