Siyo kweli kuwa CCM wote ni mazuzu, akitoka mtu CCM akija CDM uzuzu utakwisha? Ni imani yangu saizi watu wamechoka CCM hivyo wanatafuta unafuu na unafuu huo umeindokea CDM baada ya kuonyesha inaweza. Mbona Mpendazoe alipoanzisha CCJ alionekana mtu asiye na uelekeo lakini alipojiunga CDM anaonekana mtu makini. Achana na huyo yupo yule mwanamashairi Shibuda mbunge wa CDM msukuma pekee mwenye tambo na mbwembwe nyingi mbunge wa Shinyanga ni zuzu japo yupo CDM? Alikiponda chama chake pale bungeni kama amepata wazimu, mbona hamsemi. Tuache ku generalize hoja very likely conclusion ikawa mbovu. Ni mtazamo tu.