Kwanini CCM wanatuita SACCOS?

Kwanini CCM wanatuita SACCOS?

Pamoja na kuwa ukweli ni mchungu ni lazima usemwe.

Ukweli huogofya na ndiyo maana wale wanaosubiri matunda bila ya kutaka kuwa sehemu ya kuyatafuta, hao ruksa kuingia mitini na hata kutoa povu kabisa.

Ukweli ni mchungu ndiyo maana walio waoga na wasio tayari kuzilipa gharama chungu za ukombozi, ni sahihi kuwahimiza kwa bidii kabisa, kukaa pembeni kwani kwa hakika hata mawazo yao hayahitajiki.

Ni heri kuwa na watu wachache waliodhamiria, kuliko kuwa na watu wengi mizigo.

Tafakari za kina za tulikotoka, tulipo na tunakokwenda haziwezi kuepukwa katika kufikia malengo ya wazi yaliyopo.

Kuna hili la kuitwa SACCOS. Hili si la kufumbia macho. Kuona kukosolewa kwake kwa marefu na mapana yake kunaweza kutuvusha.

Chama kinachopigania katiba ya wananchi kama agenda yake kuu ya sasa, hakiwezi kuwa baridi namna hii tangia Mbowe kushikiliwa.

Chama kinachopigania haki, uhuru na usawa hakiwezi kuwa baina ya vyama ambavyo havijatoa kauli yoyote hadharani ya mshikamano na askofu Mwingira.

Chama kinachopigania haki, uhuru, usawa na demokrasia hakiwezi kuwa hakijatoa kauli yoyote rasmi na hadharani ya mshikamano na mzee wa upako, askofu Shoo na hata Polepole.

Mbowe akiwa kizuizini na Lissu akiwa nje ya nchi ni wazi sasa kuwa kwa mustakabala wa harakati kuendelea, chama kinabidi kujitathmini kwa kina.

Siasa za ukombozi zina tija zaidi "on the ground" kuliko mitandaoni.

Wako wapi kina Heche, Kigaila, na kina Lwaitama?

Wako wapi kina Mdude?

Ziko wapi busara za kina Bagonza, Ulimwengu, Niwemugizi, Ponda, Mwamakula na wenzao?

Ifahamike, ukombozi hauwezi kuwa wito kwa kila mtu. Yaani hata J4?

__________
Uanaharakati ndiyo njia pekee ya kuipata katiba ya wananchi
Sikubaliani na mwelekeo wako wa kukiri kwamba ccm wana hoja pale wanapodai CHADEMA ni saccos ya Mbowe. Kinachotokea ndani ya CHADEMA sasa ni kama ilivyokuwa kwa ccm na Nyerere enzi hizo.
Unapokuwa na mmoja anayejitolea sana kwa chama, kukitumikia kwa nguvu zote, kutojitafutia mafanikio au faida binafsi, anabaki kama nyota inayong'ara.

Lakini ccm hawana nia njema wanapodai CHADEMA ni "saccos ya Mbowe". Wanajenga picha kwamba Mbowe anafaidika kifedha na CHADEMA, ilhali ni kinyume chake. Mbowe anafilisika ili CHADEMA isitawi. Pia, Serikali ya ccm inamfilisi na kumkwamisha Mbowe ili asiwe na uwezo wa kuitumikia CHADEMA, wakati wakieneza propaganda kwamba Mbowe ananufaika kutoka CHADEMA.
Nadhani mada yako umeijengea pasipostahili.

Kuhusu CHADEMA kusinzia au la, mimi nadhani iko vizuri tu.
Agenda ya Katiba mpya inakwenda vizuri, ukizingatia tumefikia mahali serikali imekuja na "mkakati" wa "katiba" unaoshorikisha "Baraza la vyama vya siasa". Hii sasa inatoa fursa kwa wananchi kupitia forum mbalimbali, kuanzisha michakato yao, ili kuuchallenge mkakati wa serikali, kama ilivyotokeaga huko Kenya. Haya ni mafanikio makubwa.
Kumbuka kazi kubwa inayofanywa na CHADEMA hivi sasa ni kuelimisha jamii, ili kuimarisha nguvu ya umma. Hili ni eneo muhimu sana. Kuongeza political literacy ya watanzania. Sehemu kubwa ya hii inafanyika mitandaoni, ni kweli. Lakini unawezaje kuwalaumu CHADEMA kwa hili, ilhali mkakati wao wa mwanzo ulizimwa kwa nguvu kubwa, na ndio sababu ya Mbowe kuwa gerezani sasa? Japo mahakama sasa imekuwa uwanja wa siasa.
Lakini usibeze nguvu ya mitandao mkuu. Inafuatiliwa na wanabchi kwa karibu sana.
Tunachohitaji kufanya, badala ya kulaumu viongozi, ambao hata hivyo wanaendelea kujitolea, kila mmoja ajiulize anaisaidiaje CHADEMA? Unauliza Heche yuko wapi, wakati mwenzio mdogo wake aliuwawa na polisi, ili kumkomoa. Heche hata hivyo anaendeleza mapambano, tunamwona Startv, mitandaoni.
Wote sisi ni jukumu letu
 
Chadema ya Dr Slaa ilikuwa moto...hii ni mitusi na mipasho kwenda mbele.
NB: Maendeleo hayana chama
 
Utakuwa umenisoma vibaya mkuu. Hakuna niliposema Chadema ni "Saccos ya Mbowe" wala hata kuwa na mwelekeo wa kukiri hayo.

Tambua Chadema imepoa sana baada ya Mbowe kukamatwa. Chadema haijatoa hata matamko ya mshikamano na kina Mwingira, Mzee wa Upako au hata Shoo.

Kwa maana ya kuwa kwa kujua au kutokujua, tumejipanga na mtesi wetu.

Ubaridi huu ndiyo unaogomba. Chama cha harakati ni chama cha mapambano. Ndipo ilipo tofauti yake na Saccos niliyoiongelea.

Zingatia tofauti ya "Saccos" na "Saccos ya Mbowe." Mawili hayo hayatangamani.

Katika mapambano sote hatuwezi kuwa sawa. Hapa ndipo tunapaswa kutambua nani anaweza kufanya vizuri zaidi wapi baina yetu. Mbowe angekuwa nje hali ya uwanja ingekuwa tofauti kabisa leo.

Kumbuka:

Uanaharakati ndiyo njia pekee ya kuipata katiba ya wananchi

Kuwaulizia Heche, Kigaila na Lwaitama si kuwa hakuna la maana wanalofanya, bali ni katika kutambua katika hali ya sasa (Mbowe akiwa kizuizini) damu kama hizo haziwezi kuwa mbali na hatamu za chama.

Kazi lazima iendelee na kwa hali hata iliyoboreshwa zaidi.

Ninajua Heche kuuliwa mdogo wake na ninasikitika naye. Ila tambua damu hizo ni muhimu kuhakikisha chama cha harakati za ukombozi hakipoi na hasa kama hawajaomba wenyewe kupumzika.

Kujitathmini kwa dhati kabisa katika mapambano hakuwezi kuepukwa. Muhimu sana kujua:

1. Minyukano ndani ya CCM haitusaidii kwenye madai yetu ya katiba mpya.
2. Mwendazake hayupo tena, makando kando yake tuhangaike nayo kwenye "haki na maridhiano" baada ya katiba mpya.
3. Agenda zetu ni za kudumu si marafiki.

Kwamba unazungumzia kulaumu viongozi? Hilo nalo ni dalili za kuto kunisoma vyema. Hakuna anapolaumiwa mtu zaidi ya kuwa huu ni wito kufanya vizuri zaidi.

Kama mdau kushirikiana kuona jahazi letu linafika salama ni wajibu.

Harakati ardhini zitatupatia ufumbuzi wa tunayoyataka. Harakati mitandaoni peke yake haziwezi kutufikisha.

Zingatia:

Mbowe: Kwanini atashikiliwa kwa Muda Mrefu
 
Waliichukia sana awamu ya tano

Mpaka wamebakia irrelevant.
 
Chadema ya Dr Slaa ilikuwa moto...hii ni mitusi na mipasho kwenda mbele.
NB: Maendeleo hayana chama

Chadema hakijawahi kuwa cha mtu:

1. Minyukano ndani ya CCM haitusaidii kwenye madai yetu ya katiba mpya.
2. Mwendazake hayupo tena, makando kando yake tuhangaike nayo kwenye "haki na maridhiano" baada ya katiba mpya.
3. Agenda zetu ni za kudumu si marafiki.

Ila nakubaliana nawe kuwa chama cha ukombozi hakiwezi kujitenga na harakati. Na huo ndiyo ulio msingi wa hoja.
 
Wananchi wanaingiaje front kuwapa ugali watu ambao nao wamejificha wanaogopa kuumia?

Ndiyo maana ya maoni ya reorganization.

Mbowe akiwa kizuizini na Lissu akiwa nje ya nchi, watu aina ya Heche, Kigaila na Lwaitama hatupaswi kuwa mbali na hatamu za uongozi wa chama.

Majina hayo yanawakilisha wote tulio tayari kufa kwenye mapambano kuliko kwa Malaria.
 
Sijaelewa mantik ya hoja yako ila naona nikama unalaumu chama wakati huo huo utaki kuona hali ilivyo.unajua harakati za kulikomboa taifa kupitia fikra mbadala ni jukumu la kila mtu mwenye akili timamu na uchungu na nchi kwahiyo sio swala lakuviachia vyama pinzani vyenyewe.Hao unaotaka chadema itoe tamko kuunga kauli zao sidhani kama ni jambo lenye tija,kwasababu mambo mengine ni hoja binafsi za watu japo kwa njia tofauti na lengo laweza kufanana na la chama ila hiyo sio njia sahihi za cdm kufanya siasa zake.huu sio wakati wa chama kushikana na kauli za watu ambao hatujui wanazitoa kwa nia gani,huu sio muda wakudandia visa vya watu ata kama vinagusa manufaa ya kile chama inachokipigania.Chama kama chama kazi yake ni kuadress matatizo ya nchi kupitia njia za chama ila kama kuna wanaojitokeza pembeni kuunga hizo jitihada wanakaribishwa,ila sio chama kiunge jitihada binafsi za watu zilizotolewa kwa namna ya uhasama au ugomvi.Swala la katiba mpya na mambo mengine bado ni agenda kuu ya chama ila baada ya kesi ya mbowe kujitokeza lazima chama kijipange namna nyingine ya kupush hiyo agenda bila kuathiri kesi ya mwenyekiti.sasa haya ni mambo yanayohitaji busara kubwa kuyatekeleza.Na lazima ukumbuke nchi hii bado hatujafika hatua ya siasa za jino kwa jino ndo maana wadau baada yakuona mambo mengi hayajakaa sawa kwa upande wao na wakipush zaidi hizo agenda mambo yatakua magumu zaidi watu wameamua kutumia mitandao ya jamii kuelimisha na kutoa hoja zitakazoendeleza harakati zile zile kwa njia salama.Usiwe na kiu ya haraka ya mabadiliko kabla muda haujafika.
Nb:Kichwa chako cha mada na mada yenyewe havijawiana kiasi chakutoa jibu sahihi nikwanini chadema iliitwa Saccos na wapinzani wake.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Shida CHADEMA inaongozwa zaidi na mtu binafsi badala ya taasisi.

Laiti ingekuwa ni taasisi hata in absence ya Mbowe na Lissu bado chama kingeongoza harakati ya kudai katiba mpya kwa ari ileile.

Na ndio maana Mbowe hataki kuachia Uenyekiti, maana the moment anaachia uongozi... That will mark the beginning of the end for CHADEMA.

Hurting truth.
Mawazo yako sio sahihi.sijui kama unajua kwanini mbowe yuko magereza,na hii sio mara ya kwanza mbowe kukaa magereza,mbona kipindi alichokua magereza uko nyuma bado chadema iliendelea na harakati zake.Nikwasababu chadema inaamini kua kesi ya mbowe ya sasa inauhusiano wa moja kwa moja na harakati za chama.sasa kwa hali hiyo lazima kuwe na njia tofauti zakuendeleza hizo harakati.Wakienda kichwa kichwa kama chama watajikuta kwenye mtego utakaowasumbua.Usifiki kufanya siasa za upinzani afrika ni jambo rahis rahis.Inahitaji akili maarifa na uvumilivu mkubwa.Kwahiyo tatizo ni nyakati wala sio mbowe au chama.na naamini chadema itashinda huo mtihani ulio mbele yake.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Katiba Mpya, Uongozi wa Kitasisi na Demokrasia ya kweli inapaswa kuanzia ndani ya CDM kabla ya kuhangaika na nchi.
Nchi ni kubwa kuliko chama.vyama vinaanzishwa na watu na vinakufa ila nchi itaendelea kuwepo.Na swala la katiba mpya ya nchi nilakila mwananchi ndani ya nchi,hao chadema ni wahamasishaji tu.Kwa tafsiri nyingine nikwamba katiba mpya inaweza kupatikana bila kuhusisha vyama vya siasa endapo itakua ni agenda ya wananchi wote.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Sijaelewa mantik ya hoja yako ila naona nikama unalaumu chama wakati huo huo utaki kuona hali ilivyo.unajua harakati za kulikomboa taifa kupitia fikra mbadala ni jukumu la kila mtu mwenye akili timamu na uchungu na nchi kwahiyo sio swala lakuviachia vyama pinzani vyenyewe.Hao unaotaka chadema itoe tamko kuunga kauli zao sidhani kama ni jambo lenye tija,kwasababu mambo mengine ni hoja binafsi za watu japo kwa njia tofauti na lengo laweza kufanana na la chama ila hiyo sio njia sahihi za cdm kufanya siasa zake.huu sio wakati wa chama kushikana na kauli za watu ambao hatujui wanazitoa kwa nia gani,huu sio muda wakudandia visa vya watu ata kama vinagusa manufaa ya kile chama inachokipigania.Chama kama chama kazi yake ni kuadress matatizo ya nchi kupitia njia za chama ila kama kuna wanaojitokeza pembeni kuunga hizo jitihada wanakaribishwa,ila sio chama kiunge jitihada binafsi za watu zilizotolewa kwa namna ya uhasama au ugomvi.Swala la katiba mpya na mambo mengine bado ni agenda kuu ya chama ila baada ya kesi ya mbowe kujitokeza lazima chama kijipange namna nyingine ya kupush hiyo agenda bila kuathiri kesi ya mwenyekiti.sasa haya ni mambo yanayohitaji busara kubwa kuyatekeleza.Na lazima ukumbuke nchi hii bado hatujafika hatua ya siasa za jino kwa jino ndo maana wadau baada yakuona mambo mengi hayajakaa sawa kwa upande wao na wakipush zaidi hizo agenda mambo yatakua magumu zaidi watu wameamua kutumia mitandao ya jamii kuelimisha na kutoa hoja zitakazoendeleza harakati zile zile kwa njia salama.Usiwe na kiu ya haraka ya mabadiliko kabla muda haujafika.
Nb:Kichwa chako cha mada na mada yenyewe havijawiana kiasi chakutoa jibu sahihi nikwanini chadema iliitwa Saccos na wapinzani wake.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app

Kwa hakika hukuelewa mada wala mahusiano yake na kichwa cha habari. Hilo ni jambo la kawaida na hakuna geni hapo.

Hata hivyo nisiache kukushauri kutulia kusoma na ku digest vikiwamo viambata vyote kama nia ni kuelewa.

Kumbuka umechagua kichwa cha habari na kukomaa na mfano (matamko ya mshikamano) wa wanaodhulumiwa kama sisi, peke yake.

Umeshindwa kuona kuwa chama cha ukombozi ni chama cha harakati. Kwamba kupoa kiasi cha kutojihusisha na dhuluma za wengine ndipo u congregational wa kawaida (Saccos) unapoingia. Kutokutoa matamko ni mfano tu wa kujitenga na uchama wa ukombozi.

Ni muhimu kuwa na progressive mind badala ya kuwa na mawazo mgando. Hata kwa mifano au majina tusiyoyapenda kama itatusaidia kujipanga vizuri zaidi, why not?

Tusipende kusikia yale tu tunayopenda kuyasikia:

Tutambuane, nani ni nani katika kudai Katiba mpya

Kwamba tuliamua kwa makusudi kutokutoa hata matamko rasmi ya mshikamano na kina Mwingira, mzee wa upako au hata Shoo? Nukuu hizi hapa zinatuhusu:

IMG_20211221_163114_082.jpg

IMG_20211226_103449_257.jpg

Kama hatuungi mkono shughuli za wengine waziwazi, vipi tutegemee wao kuyafanya hayo kwetu?

Kumbuka kesi ya Mh Mbowe ni kesi ya kisiasa. Hakuna inachoweza kufanya Chadema kuathiri lolote kwa kujaribu kunyenyekea. Zaidi sana kwa kuongeza ari ya kudai katiba mpya ingesaidia kesi hii hata kumalizwa. Ndiyo maana hata Mwingira yawezekana asitikiswe kabisa.

Kumbuka kwa kupoa huku baada ya Mbowe kukamatwa wana incentives gani za kumwachia:

Mbowe: Kwanini atashikiliwa kwa Muda Mrefu

Zingatia:

Uanaharakati ndiyo njia pekee ya kuipata katiba ya wananchi

Haipo njia nyingine.
___________
Aungwe Mkono Askofu Mwingira kukemea Maovu
 
Chadema hakijawahi kuwa cha mtu:

1. Minyukano ndani ya CCM haitusaidii kwenye madai yetu ya katiba mpya.
2. Mwendazake hayupo tena, makando kando yake tuhangaike nayo kwenye "haki na maridhiano" baada ya katiba mpya.
3. Agenda zetu ni za kudumu si marafiki.

Ila nakubaliana nawe kuwa chama cha ukombozi hakiwezi kujitenga na harakati. Na huo ndiyo ulio msingi wa hoja.
Tujiulize, nani wanaofanya Chadema kionekane chama cha kiharakati?

Ni CCM. Kwasababu wao wanajiita "chama dola" na wanasaidiwa na dola kukaa madarakani, watu wanapigwa wakidai haki zao, kura zinaibwa vituoni kwa nguvu, CDM wakijitetea wanaitwa wanaharakati.

Wao CCM wanataka CDM wawe makondoo wanaonyamaza kwa kila baya watalofanyiwa, na kujibu mapigo kwa CDM ni kwa kufuata sheria za nchi, vitu kama maandamano ni haki yao, ili kupaza sauti zao kwa ukatili wanaofanyiwa na polisi na CCM.

Lakini bado watanyimwa vibali, wataambiwa intelijensia ya polisi imeona patakuwepo na vurugu kwenye maandamano, kama polisi wameinusa vurugu kwanini wasipeleke ulinzi? hawapeleki sababu wao na CCM ni timu moja.

Siku CCM wakiacha uhuni wao wa kutegemea jeshi la polisi, wakafanya kama chama cha siasa, basi siku hiyo hiyo na Chadema hakitaitwa chama cha kiharakati, uanaharakati wa CDM unalazimishwa na matendo ya CCM.
 
Neno harakati si neno baya. Maneno harakati na ukombozi ni maneno yaliyo karibu.

Halikubaliwi jambo bila kupambana, na hiyo ndiyo harakati.

Chama cha harakati ni kile kinachotaka mabadiliko dhidi ya mtawala asiyetaka kuridhia.

Chama cha kudai ukombozi wa aina yoyote ikiwamo katiba mpya ni chama cha harakati.

Bila harakati hakuna mabadiliko.

Harakati ni kwa mujibu wa sheria. Hakuna kosa kisheria la kuwa mwanaharakati.
 
Neno harakati si neno baya. Maneno harakati na ukombozi ni maneno yaliyo karibu.

Halikataliwi jambo bila kupambana, na hiyo ndiyo harakati.

Chama cha harakati ni kile kinachotaka mabadiliko dhidi ya mtawala asiyetaka kuridhia.

Chama cha kudai ukombozi wa aina yoyote ikiwamo katiba mpya ni chama cha harakati.

Bila harakati hakuna mabadiliko.

Harakati ni kwa mujibu wa sheria. Hakuna kosa kisheria la kuwa mwanaharakati.
Tatizo kwao ni tafsiri ya neno "harakati" kwao harakati ni vurugu ndio maana CDM wakitaka kuandamana watasema intelijensia yao imewaonesha patakuwa na vurugu.

Hata hawa wapiga kelele wengi humu ndani nao wanachukulia harakati kama vurugu ndio maana wanalazimisha CDM kiachane na harakati. Sasa CDM kikiachana na harakati kama maandamano, mikutano ya siasa, na nyingine kitakuwa chama cha siasa cha aina gani?
 
CDM ikiachana na "harakati" itakuwa "Saccos." Yaani mkusanyiko wa watu usiokuwa na mbele wala nyuma.

Hakuna mabadiliko bila harakati. Ndipo tunapoona harakati zinaelekea kupoa hivi, ni muhimu kupiga kelele.

Kazi (ya ukombozi) lazima iendelee.
 
Ndiyo maana ya maoni ya reorganization.

Mbowe akiwa kizuizini na Lissu akiwa nje ya nchi, watu aina ya Heche, Kigaila na Lwaitama hatupaswi kuwa mbali na hatamu za uongozi wa chama.

Majina hayo yanawakilisha wote tulio tayari kufa kwenye mapambano kuliko kwa Malaria.
Hivi sasahivi nani anapambana?
 
Back
Top Bottom