4 7mbatizaji
JF-Expert Member
- Dec 8, 2019
- 11,303
- 12,954
Propaganda zao mfu zilishakwama, hawana jipya, CCM sio level ya Chadema tena ,wanalazimisha yaende lakini wapi,Pamoja na kuwa ukweli ni mchungu ni lazima usemwe.
Ukweli huogofya na ndiyo maana wale wanaosubiri matunda bila ya kutaka kuwa sehemu ya kuyatafuta, hao ruksa kuingia mitini na hata kutoa povu kabisa.
Ukweli ni mchungu ndiyo maana walio waoga na wasio tayari kuzilipa gharama chungu za ukombozi, ni sahihi kuwahimiza kwa bidii kabisa, kukaa pembeni kwani kwa hakika hata mawazo yao hayahitajiki.
Ni heri kuwa na watu wachache waliodhamiria, kuliko kuwa na watu wengi mizigo.
Tafakari za kina za tulikotoka, tulipo na tunakokwenda haziwezi kuepukwa katika kufikia malengo ya wazi yaliyopo.
Kuna hili la kuitwa SACCOS. Hili si la kufumbia macho. Kuona kukosolewa kwake kwa marefu na mapana yake kunaweza kutuvusha.
Chama kinachopigania katiba ya wananchi kama agenda yake kuu ya sasa, hakiwezi kuwa baridi namna hii tangia Mbowe kushikiliwa.
Chama kinachopigania haki, uhuru na usawa hakiwezi kuwa baina ya vyama ambavyo havijatoa kauli yoyote hadharani ya mshikamano na askofu Mwingira.
Chama kinachopigania haki, uhuru, usawa na demokrasia hakiwezi kuwa hakijatoa kauli yoyote rasmi na hadharani ya mshikamano na mzee wa upako, askofu Shoo na hata Polepole.
Mbowe akiwa kizuizini na Lissu akiwa nje ya nchi ni wazi sasa kuwa kwa mustakabala wa harakati kuendelea, chama kinabidi kujitathmini kwa kina.
Siasa za ukombozi zina tija zaidi "on the ground" kuliko mitandaoni.
Wako wapi kina Heche, Kigaila, na kina Lwaitama?
Wako wapi kina Mdude?
Ziko wapi busara za kina Bagonza, Ulimwengu, Niwemugizi, Ponda, Mwamakula na wenzao?
Ifahamike, ukombozi hauwezi kuwa wito kwa kila mtu. Yaani hata J4?
__________
Uanaharakati ndiyo njia pekee ya kuipata katiba ya wananchi
CCM Chama magawio, Chama GANI mpaka mkuta mwanaume mzima,anakunishwa nazi, Sasa hao vijana na wanakokolo watafanya nini?
