Kuna kila dalili kuwa CCM itaanguka vibaya sana 2020.
Sababu kuu juu ya anguko hilo ni,
1.Wananchi kuchoshwa na udikteta wa rais.Ni hulka ya binadamu kutaka kuwa huru,yeye na ndugu zake hata kama utampa kila kitu.
2.Kutokutekelezwa kwa ahadi na kutokutatuliwa matatizo ya wananchi.Serikali inaonekana haitoweza kutatua kero za wananchi kama walivyotarajia.
Mambo kama kuhamisha Makao Makuu sio kipaumbele cha maskini walio wengi,kuzuia safari haleti credit sana kwa wananchi.
3.Kutunza amani,udugu na mshikamano.Kauli za wakuu wa sasa zinajaza watu hofu,wanatishwa! Wakipata mtu wa kuwapa moyo,wataachana na kauli za kibaguzi kwa kutoichagua CCM.
4.Kuimarika kwa ushirikiano wa vyama Vya upinzani.CUF na CHADEMA,vyama vikuu vinahisi kunyanyaswa na serikali ya CCM,hivyo vitaungana tena na Labda kuunda chama kimoja! Hiki chama au huu muungano utakuwa na nguvu sana.
5.Kudorora kwa kuaminiana ndani ya CCM.Wale jamaa watahujumiana na ndio maana wananyukana kimyakimya.Mf.nyuzi za ndg Lizaboni wa JF wakati wa mchakato wa kumtawaza Dr.Magufuli uenyekiti wa CCM.
Chamsingi ni upinzani kuwa imara.