Kwanini CCM na Magufuli wataondoka madarakani 2020

Kwanini CCM na Magufuli wataondoka madarakani 2020

Dunia sio mstatili, ni duara kwa maana inazunguka na Tanzania hivyo hivyo. Makubaliana na wewe kuwa Tanzania upinzani ni kama haupo tofauti na nchi kama Kenya. Lakini matendo yanayoendekea yatachochea upinzani wa ukweli. Kwa mfano Mheshimiwa Rais alipoingia madarakani ni kama aliteka nyoyo za watanzania wote hadi waliopigia kura upinzani wakawa wanajuta kwanini walipigia upinzani.

Sasa hivi hali tofauti, kauli na hali halisi ilivyo imewabadilisha mpaka wale waliompigia yeye kujuta kumpigia. Na kwa kuwa kujuta kwao ni kutokana na hali zao taabani za kiuchumi na kauli kali za Mkuu; hatutarajii hali hii ya watu kubadilika ndani ya miaka minne ijayo.

Sote tunajua hakuna nchi iliyojenga viwanda kwa miaka mitano, ila iliweka msingi imara usioyumba ndani ya miaka hiyo. Hata hivyo Mkuu yeye anaonyesha anataka kuwa na viwanda (firmly established) katika miaka hiyo, hili ni gumu. Akija kutahamaki 2020 hiyo hapo, ndio uchaguzi wa kipolisi sasa utakaoshika kasi. Na mind kwamba, kwa kutumia nguvu, bila shaka utashinda lakini uongozi wako utakuwa kama upepo, huna ulifanyalo na miaka hukatika kama moto wa mabua.

Hakuna chama cha upinzani chenye lengo la kwenda ikulu tanzania. Vyama haviandai wagombea urais miaka yote wanakurupuka tu. Mpaka mtu akatwe ccm ndiyo umsimamishe kugombea!! Usiote ndoto mchana kaka maana kwa hali ilivyo labda 2055!
 
Omba uzima. Kuna mwanafalsafa mmoja jina nimelisahau aliwahi kusema "ukiwa mwingi wa ahadi basi pia uwe mwingi wa uongo". Mwisho wa kunukuu.
 
Rais Akiwa Pemba alisema Mtu kuota Usiku ni Kawaida, ila Ukiona mtu anaota Mchana.........
 
Walisema 2015 sahizi eti 2020. Nadhani ikifika 2020 kwa mwendo huu wataingia kwenye makumbusho ya Taifa.

Mwenyekiti CCM JF
Inaelekea Ndugu Zetu hawa wana Dira yao ya Kufikirika kila Uchaguzi Mkuu ufikapo.
 
Mlipoteza Credibility Kwa Watanzania Pale tu mlipoamua kwa Makusudi kumbadili yule mlietuaminisha kwa Kipindi kirefu kuwa Fisadi, kutoka kwenye kashfa mliyompa mpaka Mgombea wa Chama Chenu akibeba kijiti cha kuwapeleka Ikulu.....
 
Mimi siyo mwanasiasa lakini kama nilivyotabiri uchaguzi uliopita ninatabiri tena kuwa kama mambo yataendelea kama yanavyoendelea sasa, JPM atapita vibaya sana na watakaomchagua ni wananchi hao hao ambao mnadhani nyinyi wa mjini ndiyo wasemaji wao!

Wewe siyo mtabiri.....kama ni mtabiri ebu tutabirie tamko litakalotolewa na...........kesho kutwa
 
Mleta Thread umenena kweli,ila utawaona stomach THINKERS & SEEKERS watakavyoruka na wewe na kutoa mapovu bila kujibu hoja kwa hoja.
Ni ukweli usiyopinga kwa wenye maono wataelewa bila kutumia mahaba,kwani serikali hii imezidiwa no missions,visions,plans and ojectives.
Utasikia kesho huyo katoa tamko lake mara mkuu wa kaya tamko lake mara mara hili mara lile kabla lile halijakamilika,yaani mambo ni mchananyiko kama uji wa nyama vile ambao hata haupo.
Anyway yangu macho na masikio na tuombe uzima na afya tele hadi mwisho wa Season iliyojaa Series of Movies.
 
Siku za nyuma tungeweza kushauri ili chama kiendelee kukubalika zaidi ila kwa sasa tunaogopa.
Yote tunamwachia Mungu .
 
Wananchi vijijini ndio wanaolalamika kwa kiasi kikubwa!
Wanadai kua walidanganywa kua bidhaa za ujenzi kama mabati, sement, mondo,misumari, mbao nk kua vitashuka bei baada ya kuichagua CCM, Wanalia tabu ya maji ni shida tupu hakuna unafuu hata kidogo, sukari bei iko juu pamoja na pesa kua ngumu kiasi hicho.

Wanasema kua sasa imetosha kudanganywa hata kama atashuka YESU agombee Urais kupitia CCM hawatakaa warudie makosa kuipigia kura mgombea kupitia CCM.

Haya ni malalamiko ambayo nimeyasikia kwa wananchi wengi mfululizo huku wilaya ya Magu maeneo ya kisesa mkoani Mwanza.

Kwa hali hii hata kama katiba ya wananchi bado ni kizungumkuti CCM watatobolea wapi! Kama watatoboa lakini wasi wasi wangu ni kura za bao la mkono.Vinginevyo kusubiria uvujwaji wa wazi wazi wa katiba iliyopo wakati wa uchaguzi ujao, maana naona uhai wa mwisho wa CCM ulikua kwa Rais aliyepo sasa ila kama ndio wananchi wanachoka mapema tu hivi ndani ya miezi 9 ya uwala huu mimi sina neno zaidi.
 
Haitoboi wakati kura hampigi. Kwa taarifa yako hao hao wanakijiji ndio wanaokipigia na kukirudisha madarakani coz CCM inawafikia kila kona. Mbuni mikakati ya kuwafikia wapiga kura kule walipo na sio maonesho ya chopa na mafuriko feki mijini halafu malalamiko ya kuibiwa hayaishi. Mtu anakuchagua vipi kule Mpitimbi wakati kura hujamuomba na hujawahi kusimamisha hata mgombea wa kitongoji?
 
Watu wa vijijini ni Lumpen proletariat. Kofia, kanga, leso, T shirt can turn the scale in a different direction overnight
 
Vijiji kama vya huko Domya ni sheeda yaani!!
Huko wanataabika mbaya, lakini ......
 
Mwaka 2015 Ccm ilishindwa sema figisu za Makamba ndio zilirudisha madarakani. Mimi naona waongeze watu watu wasiofungamana na upande wowote kwenye kujumlisha matokeo ili kupata uwazi
 
Waache tu wahangaike maana wakati wa kampeni wakipewa pipa la pombe ya kienyeji na kuchinjiwa ng'ombe basi wanasahau tabu zote kwa masaa
 
Mzaa mzaa huzaa usaha....

1. Hakuna kufanya siasa hadi 2020
2. Hakuna kufanya mikutano ya kisiasa ya ndani
3. Loading.....

Hakuna ucha... i mean hakuna uchambuzi 2020!!!
 
Haitoboi wakati kura hampigi. Kwa taarifa yako hao hao wanakijiji ndio wanaokipigia na kukirudisha madarakani coz CCM inawafikia kila kona. Mbuni mikakati ya kuwafikia wapiga kura kule walipo na sio maonesho ya chopa na mafuriko feki mijini halafu malalamiko ya kuibiwa hayaishi. Mtu anakuchagua vipi kule Mpitimbi wakati kura hujamuomba na hujawahi kusimamisha hata mgombea wa kitongoji?
Wanavijiji hali zao mahututi sasa hivi.
 
Back
Top Bottom