Kwanini biashara yako ya kwanza ilikufa? Sema nasi tujifunze

Sokoro waito

JF-Expert Member
Nov 21, 2014
2,201
2,587
Hamjambo wadau na watafutaji wa pesa,

Mimi binafsi nilifungua biashara yangu ya kwanza nilipokuwa mwanafunzi wa sekondari ambayo ilikuwa ya duka dogo la rejareja ila biashara hii ilikufa kwasababu ya kukosa ulinzi wakati wa usiku, wezi waliniibia mara kadhaa hadi kupelekea kudhoofisha mtaji wangu na hatimaye nikafunga biashara. Baada ya hapo nilijifunza kuwa biashara yoyote ile lazima iwekewe ulinzi thabiti.

Vipi kwa upande wako wewe, kwanini biashara yako ya kwanza ilikufa?

Huenda biashara yako ya kwanza haikufa ila ila ilikumbana na changamoto kedekede, basi share nasi kuhusu hizo changamoto.

Sema ili nasi tujifunze.
 
NI MARA CHACHE SANA BIASHARA AMBAYO HAUISIMAMII MWENYEWE KUSTAWI NA KULETA FAIDA!!!

USICHEZE MBALI NA BIASHARA YAKO-

UPIGWAJI NI NJE_NJE!!!
 
Hamjambo wadau na watafutaji wa pesa,

Mimi binafsi nilifungua biashara yangu ya kwanza nilipokuwa mwanafunzi wa sekondari ambayo ilikuwa ya duka dogo la rejareja ila biashara hii ilikufa kwasababu ya kukosa ulinzi wakati wa usiku, wezi waliniibia mara kadhaa hadi kupelekea kudhoofisha mtaji wangu na hatimaye nikafunga biashara. Baada ya hapo nilijifunza kuwa biashara yoyote ile lazima iwekewe ulinzi thabiti.

Vipi kwa upande wako wewe, kwanini biashara yako ya kwanza ilikufa?

Huenda biashara yako ya kwanza haikufa ila ila ilikumbana na changamoto kedekede, basi share nasi kuhusu hizo changamoto.

Sema ili nasi tujifunze.
Sababu ilikuwa ulinzi pia nlikuwa nauza kuni mtaji Milion Ila ulinzi haukuwa mzur niliibiwa kidgkidg mpka mtaji ukafa
 
Back
Top Bottom