Kwanini bei za nyumba za kulala Zanzibar ziko juu sana

mkadiriajimajenzi

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
549
608
Hivi majuzi nilipata wasaa wa kutembelea visiwa vya zanzibar nilistaajabu kuona bei za nyumba za kulala wageni ziko juu sana kulinganisha na huku kwetu bara yaani chumba ambacho huku bara unaweza kulala kwa Tsh. 5000 wao wanatoza 20K.Tatizo ni mji wa kitalii ama, mbona Arusha na miji mingine ya kitalii bei hazipo hivyo?
cb0080d4ca82bb162cdf90e8b7d880c5.jpg
9f9eb1d11b469d86fc1d16cf19d53acd.jpg
93f24af59bc797132cf9f6ca59ecc639.jpg
 
Hicho ni 20k (sio self)sehemu nyingine ni 40k-60k sehemu za kawaida kabisa
Inategemea lakini na ulichokwenda kufanya huko.kama umekwenda kutafuta maisha sawa.ila kama ukienda kula good time basi inabidi uende na hela ya kutosha.mji wa kitalii huo.
 
Zanzibar ni noma..
Nilienda Seminar moja huko chuma cha Elf 50 ni kibovu hatari..
Sabuni ya kipande..
No A/C
No Water heater..
Mashuka machafu.
Vyumba vina giza balaa..
Wakati Dar au Arusha kwa hela hiyo unapata chumba ambacho ni very quality
From there Seminar yeyote inayofanyika zanzibar siendi....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zanzibar ni noma..
Nilienda Seminar moja huko chuma cha Elf 50 ni kibovu hatari..
Sabuni ya kipande..
No A/C
No Water heater..
Mashuka machafu.
Vyumba vina giza balaa..
Wakati Dar au Arusha kwa hela hiyo unapata chumba ambacho ni very quality
From there Seminar yeyote inayofanyika zanzibar siendi....

Sent using Jamii Forums mobile app
next time tenga kama 200k hivi, utapata chumba kizuri tu na ufurahie muda wako huko. Zanzibar, the future of tourism.
 
Jamani tambueni kuwa Zanzibar wana shida kubwa ya mchanga wa kujengea hivyo lazima gharama za malazi ktk nyumba za wageni ziwe juu.
 
Zanzibar kuna ujinga mwingi sana, na ukilala mjini utaishia kulipishwa hela kubwa then unalazwa kwenye magofu...mi nilienda mpka Fuoni nikapata chumba cha kawaida kabisa kwa 40k, ambacho kwa Dar ni 15k au 20k!
 
Tuache kulalama, tutafute pesa, kuna Lodge pale Lushoto, chumba cha chini ni 150,000ths na cha juu 295,000ths,nilipokwenda kutembea tu sio kulala pale, Ile Lodge ilikua full booked!!,tusilalame ,tafuta pesa
 
kama huna hela bora ukae huko huko kwenu, Znz lazima uwe uko vizuri lasivyo utaenda kulala na wamasai.
 
Zanzibar kuna ujinga mwingi sana, na ukilala mjini utaishia kulipishwa hela kubwa then unalazwa kwenye magofu...mi nilienda mpka Fuoni nikapata chumba cha kawaida kabisa kwa 40k, ambacho kwa Dar ni 15k au 20k!
Zanzibar uwekeza bado upo Chini, Nyumba siyo nyingi bado Kuna uswahili sana Kule, utakuta mwananchi mwenye kipato kikubwa kwa siku ana ingiza million mbili lakini ukiona anapoishi utashangaa yani anaishi na mtu wa Kipato cha elf kumi kwa siku.
 
Back
Top Bottom