Kwanini bei ya vifurushi vya simu na ving'amuzi zinakuwa ghali tofauti na zamani?

Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
2,102
3,615
Miaka ya 2010 walisema kuwa, mkonga wa taifa mawasiliano ukikamilika bei ya vifurushi itapungua, lakini siku zinavyozidi kwenda bei ya vifurushi inazidi kupaa.

Swali dogo tu! Miaka ya nyuma (2000), bei ya vifurushi vya simu ilikuwa chini ingawa wateja walikuwa ni wachache, lakini leo vifurushi vya simu bei juu na wateja ni wengi! Je, kati ya zamani na sasa, zama zipi makampuni yanatengeneza faida kubwa kati ya kipindi cha wateja wachache na wateja wengi?

Hivyo hivyo, kwenye makampuni ya ving'amuzi, miaka ya nyuma vifurushi vilikuwa bei chini ingawa wateja walikuwa wachache, lakini leo bei ni juu na wateja ni wengi!

Mimi nilidhani zama hizi bei ya vifurushi ilipaswa ishuke chini kwa sababu makampuni yana wateja wengi ukilinganisha na zamani!

Kwenu wataalamu wa uchumi!
 
Zama zinabadilika mkuu Sasa tupo 2022 ukiwa unawaza upo 2020 utakuwa na shida kichwani sio bure.

Lipa Kodi kwa maendeleo ya taifa pasipo na Kodi Hakuna maendeleo au Kama una njia tofauti ya kuishauri serikali kuleta maendeleo pasi kulipa Kodi iseme?
 
Sijabisha kulipa kodi. Naunga mkono kulipa kodi.

Nachotaka kufahamu, ni kanuni gani za kiuchumi zimetumika, kwamba, kipindi cha wateja wachache bei ya vifurushi ipo chini, na kipindi cha wateja wengi bei ya vifurushi ipo juu!

Kwani, kwenye wateja wengi si ndiyo bei inatakiwa iwe chini pamoja na kulipa kodi, au? Nyie wataalamu wa uchumi mtusaidie sasa!
 
Kadiri watumiaji wanavyo ongezeka ndivyo gharama za utoaji hudum zinavyo ongozeka ,

Kumbuka na makampuni lazima yalipe cha kaisali..lazima wakuminye wewe ili na wao wapate Chao
 
Issue ni inflation...mfumuko wa bei. Running costs za makampuni zinaongezeka na kuathiri bei za vifurushi.

mfano, minara huwa ina standby generators. Mafuta yanayo run zile generator yakipanda bei itaongeza gharama za uendeshaji. Magari ya haya makampuni yanatumia mafuta haya haya yaliyopanda bei.

So wao pia wanamtwisha mtumiaji wa mwisho hilo ongezeko la gharama ili ku maintain profit margin.
 
Back
Top Bottom