Kwanini bei ya sukari ipande kama petrol | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini bei ya sukari ipande kama petrol

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Novatus, Jul 29, 2009.

 1. Novatus

  Novatus JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2009
  Joined: Jul 28, 2007
  Messages: 331
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  I??

  Kwa wiki kadhaa sasa bei ya sukari imepanda siku hadi siku. sina huhakika na na mikoa mingine ila nina uhakika na hapa Mwanza. ni jambo la kusikitisha kuona sukari inayotegemewa na karibu kila mwananchi toka mtoto hadi mzee, toka mgonjwa hadi wenye afya, tajiri na maskini!!

  Viwanda vyetu vinafanya kazi kwani sukari inayoonekana madukani inatoka viwanda vya hapa nchini. Jamani mwenye kuelewa ni kwanini atueleze.

  WABUNGE pamoja na shughuli nzito za kutetea hoja mbalimabali fuatilia hili linagusa jamii mnayoiwakilisha.
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kwanza viwanda vyote vilibinafsishwa na viongozi ni share holders.
  Lakini walipokuja na sera ya kulinda viwanda vya ndani, na kwa kuwa hakuna mtetezi wa mlaji kwa hii wanaita free market, wajanja hawa wachache wametumia jukwaa hilo kuibia wananji.

  Ndivyo ilifanyika hata katika mafuta hadi EWULA walipoamka usingizini
   
 3. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Naungana na wewe kabisa, nchi za wenzetu kuna "professional lobyists" katika kuhakikisha maslahi ya wafanya biashara yanalindwa na watunga sheria na sera za nchi.
  Tanzania wanasiasa wengi wanakuwa wafanyabiashara na kila maamuzi wanayofanya wanafikiria kwanza wao watanufaika vipi, kwenye biashara zao na hata rushwa walizopokea toka kwa wafanyabiashara ili wawakandamize wananchi ambao hawana hela za kuwahonga viongozi ili matatizo yao yapewe kipaumbele
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwani Kagera shuga imekuwaje? Nilidhani wao ndio wanasambaza huko kanda ya ziwa?
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Property of fisadis are all over the country!Price r the same every where.
  Uwezi kuamini.
  Hakuna hata haja ya kuwa na kiwanda kule Kagera. It makes no difference!:(

  Tunao sasa beparis from our own people voted by us:(
   
Loading...