Kwanini bei ya mazao ya chakula na biashara iko chini kwa miaka hii mitano?

chotera

JF-Expert Member
May 19, 2016
6,305
15,034
Wakuu.

Najiuliza kwa nini Bei ya mazao kipindi cha JK ilikua juu kuanzia mazao ya chakula na biashara?

Ajabu kwa mfano ufuta mwaka huu mbeya umefika hadi 1300 kwa kilo.

Kwenye mchele ndio majanga, soya kuna balaa huko mimi nadhani Serikali kwa kuwa hawatoi ruzuku kwa mkulima waachie uhuru wa ununuaji na uuzaji wa mazao ili mkulima afanye kitu ambacho kitakuwa msaada kwake.

Hivi vyama vya ushirika havina maana hivi fikiria mnunuzi anakuja kununua na mifuko yake lakini kwenye korosho eti mkulima anauziwa gunia na chama hii sio sawa.
 
Mkulima amesahaulika sana kwa miaka mitano. Kulima bila pembejeo na wakati wa mavuno masoko hakuna.
 
Mnunuzi mmoja mazao mengi kwanini asiringe.

Demand & Supply.

Ukitaka uza, usipotaka kaa nayo. Mnunuzi ndio huyo.
 
Mnunuzi mmoja mazao mengi kwanini asiringe.

Demand & Supply.

Ukitaka uza, usipotaka kaa nayo. Mnunuzi ndio huyo.

Hata kwa mnunuzi hali ni mbaya, mpunga kwa mfano muda huu ulikua unakobolewa kilo moja kwa 1300 lakini sasa maeneo ya kanda ya ziwa ni 900 kwa kilo na wanunuzi hakuna
 
Mkuu, unajua swala la bei ya vyakula kila mtu ana mawazo na fikra zake!!

Ambao si wakulima hufurahishwa zaidi na bei kuwa chini, ila wakulima ndio wanalia!!
 
Hata kwa mnunuzi hali ni mbaya, mpunga kwa mfano muda huu ulikua unakobolewa kilo moja kwa 1300 lakini sasa maeneo ya kanda ya ziwa ni 900 kwa kilo na wanunuzi hakuna
Soko kubwa la mchele wetu Ni Kenya Uganda na Rwanda wamefunga mipaka Lisa corona.
 
Mbegu bora, upatikanaji wa pembejeo, watu wengi kukimbilia kulima, soko la nje kuwa gumu kutokana na changamoto ya corona hiyo nimezungumzia kwa mazao ya chakula ila kwa mazao ya biashara ni kutokana na serikali kuzuia wanunuzi binafsi na yenyewe kutaka kufanya biashara mfano korosho
 
Wanunuzi binafsi waruhusiwe asee maana usawa katika soko la mazao kwa sasa ni changamoto
 
Soko kubwa la mchele wetu Ni Kenya Uganda na Rwanda wamefunga mipaka Lisa corona.
Mh. alisema acheni hao jamaa waji-lockdown then hawatafanya kazi ya kulima kwa hio watakuja kununua chakula huku kwetu so tuwauzie kwa bei kubwa sana,sasa mbona hao jamaa hawaji hata kununua hio michele/vyakula aisee au ndo wamesusa?
 
Back
Top Bottom