Kwa mtazamo wangu nchi yetu imeingia kwenye mgogoro mkubwa kabisa wa kikatiba ambao haujawahi kuikumba nchi hii tokea kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini mwaka 1992.
Kwa kuwa kitendo cha Rais kutangaza hadharani kuwa anapiga marufuku shughuli zozote za kisiasa hadi mwaka 2020, ni uvunjaji wa wazi wa Katiba ya nchi yetu Ibara ya 3.
Sasa pengine bila kujua impact yake, inawezekana Magu wakati anatangaza zuio hilo la shughuli za vyama vya siasa hadi mwaka 2020, pengine aliamini kuwa, ana mamlaka ya kiutawala ya kupiga marufuku shughuli za siasa za vyama vya upinzani na kuruhusu shughuli za siasa za chama chake cha CCM!
Sasa hapo ndipo ninapouona mgogoro mkubwa kabisa wa kikatiba utakapoibuka iwapo Rais wa nchi anayo mamlaka ya kupiga marufuku shughuli za kisiasa za vyama vya upinzani na hapo hapo kuruhusu shughuli za kisiasa ziendelee kwa chama chake cha CCM.....