asiyetabirika
Member
- Oct 14, 2019
- 46
- 55
Nakumbuka ilikuwa ni mara ya kwanza kwenda kuandikishwa shule, nilipelekwa na mshua ila kwenye process za kuniandikisha kuna sehemu aliniacha nje ya ofisi ya mkuu wa shule kwenye bench, wakati nimekaa kwenye lile benchi nje kwenye ofisi ya mkuu wa shule baba akiwa ameingia ndani kumilisha baadhi ya taratibu ili nianze masomo yangu ya darasa la kwanza kuna mwanafunzi wa hiyo shule alikuja kukaa pembeni yangu akaanza kujitapa kuwa yeye yupo darasa la pili na kuna masomo magumu huku akinitisha na ugumu wa hesabu uliopo huko nilitishika kidogo kwa sababu mimi ilikuwa nikihesabu mwisho wangu ulikuwa ni mpaka kumi kwa ufasaha ila mwisho wangu kabisa ilikuwa ni mpaka 20 kwa mbinde.
Baada ya majigambo kadhaa ya yule mwanafunzi wakati anainuka kwenye lile bench tulilokaa wote akalisukuma makusudi kwa nyuma ili nidondokee nyuma kiukweli isingekuwa umahiri wangu ningeshuka chini, nilipatwa na hasira nika mfuata dogo nilimpa vichwa yaani nilipiga vichwa yule dogo alifurukuta kwa kurusha vingumi vyake lakini havikifua dafu nilitandika vichwa yaan hata sikujua ule ujasiri ulitoka wapi na ugumu wa bichwa langu ndio niliupima pale yaani nilitia ndosi, tia vichwa hadi mshua na mwalimu aliyekuwa nae ndani akatoka kuja kutuachanisha nikatia bichwa la mwisho kwa yule mwanafunzi akapiga magoti chini huku kamasi na jasho likimtoka mwilini na kwikwi za kulia.
Baada ya kuachanishwa yule mwalimu alinifokea sana huku akilitolea macho bichwa langu nadhani alishangazwa na ugumu wake akanitishia kunichapa mzee nae alionyesha kukasirika juu ya tukio lile, baada ya muda tukaruhusiwa turudi nyumbani huku yule mwanafunzi tukimuacha kapigishwa magoti akisubiri adhabu yake, mimi niliambiwa nikaanze shule juma tatu kwa sababu siku ile ilikuwa ijumaa.
Sasa cha kushangaza tukiwa njian mzee alionyesha kufurahishwa na uhodari wangu hasa kwa ule ujasiri wa kumtia vichwa mwanafunzi kwa siku ya kwanza tu na ukizingatia nilikuwa bado mgeni kabisa. Mshua aliniambia "safi sana mwanangu yaani usikubali kuonewa,hata mimi baba yako sikuwahi onewa kizembe shule, yaani yule ungetia ngumi na mateke kabisa" mzee alinipa kichwa yaan hata nilipoanza shule sikuwahi kuonewa hadi namaliza shule.
Sasa kwanini imekuwa wazazi wakifurahia badhi ya hizi tabia mbaya kwa watoto wao wa kiume? Taja pia tabia mbaya iliyowahi ifanya halafu ukapongezwa na mzazi kinyume na matarajio yako kuwa ungegombezwa.