Kwanini baadhi ya watu wako hivi?

Kwanini baadhi ya watu wako hivi?

Mkuu si huko kwenye sehemu za kukutana kwa mara moja, yaani unafanya kazi au unasoma na mtu wa namna hiyo.

Kutoa siri na habari zako kwa watu sio vizuri mana binadamu hawatabiriki bora kuwa kimya sasa kuwaambia watu mambo yako ili iweje
 
Wapo hao na mimi nlikua na tabia hiyo lakini nilipofika chuo nikajikuta hiyo tabia nimeiyacha bila ya kukusudia
 
Yani me napenda mtu asiyeropoka, awe mkimya kidogo but asiwe mkimya mazima. Kuna mtu utakaa naye dk 3 lakini utamjua majina, kazi yake, assets alizonazo, his/her future plans, elimu yake n.k. Watu wa hivi usitegemee kama itatokea tena mimi kukaa na wewe, they are so irritating khaa. Afu unakuta anayoyaongea mengi ya uongo, kupenda tu sifa za kindezi
 
Yani me napenda mtu asiyeropoka, awe mkimya kidogo but asiwe mkimya mazima. Kuna mtu utakaa naye dk 3 lakini utamjua majina, kazi yake, assets alizonazo, his/her future plans, elimu yake n.k. Watu wa hivi usitegemee kama itatokea tena mimi kukaa na wewe, they are so irritating khaa. Afu unakuta anayoyaongea mengi ya uongo, kupenda tu sifa za kindezi

people express their variety so as one day you can expose his life when he/she is dead
 
ndivyo haswa wote tunatakiwa kuwa hivyo sio unapanda daladala by the time unashuka kila mtu anajua majina yako matatu na wapi unafanya kazi na mkeo alikusaliti na unaumwa kisukari.....what for?

hahahahaha wengine wanajiongelesha kwa simu makusudi kabisa mambo yake binafsi
 
Wewe unataka kumjua mtu kwa undani kwa sababu gani hasa???? una mpango wa kumtafutia mchumba wa kumuoa/kuolewa?????
 
Hizo ni personality za watu...

Ila nakubali kuwa na mtu msiri awe rafiki au partner ni kazi sana...

Na watu wasiri ndio wanaoongoza kwa suicide...

kwa hiyo kuna faida na hasara zake...kwa both personality traits...ila msiri ni mbaya zaidi...

(ingawa nahisi mimi ni mmoja wao japo niko open zaidi humu JF kwa kuwa sina ninaye mjua...kama naongelea kwenye chungu vile...lol)
 
Hizo ni personalities. Ila kama kumbukumbu zangu ziko sahihi, kuna makundi 4 ya personality: Sanguine, Choleric, melancholy, na phlegmatic. Sanguine na choleric ni talkative na friendly, ila sio good friends yaani si wa kuwategemea kukusaidia wakati unawahitaji: melancholy na phlegmatic sio waongeaji sana ila true friends hupatikana toka kwao. Ila haimaanishi sanguine na choleric wote ni bad friends au melancholy na phlegmatic wote ni good friends. Personality zote zina faida na hasara na watu wote wana mchanganyiko wa personality, isipokuwa kuna moja ndiyo hujitokeza zaidi. Hivyo watu wako hivyo kutokana na personality zao, na nina uhakika umefaidika na zote.
 
people express their variety so as one day you can expose his life when he/she is dead

I don't entertain it, I think its kind of immaturity too. How on earth would u start blabbing about who u are or what u have to strangers? Is it a must for us to know about ur details, what for?
 
Kuna watu wanapenda privacy. Ni muhimu kuheshimu utashi wa kila mmoja. Kuna watu wako nosy, ukimuambia kitu kimoja anakuganda na maswali kama mia

ila kuna watu wanakera, siku ya kwanza mmekutana atajielezea wee maisha yake utafikiri umemuomba story urekodi movie.
 
Back
Top Bottom