Kwanini baadhi ya ajira za mashirika ya umma michakato yake haipitii utumishi?

Sio lazima email, hata kwa njia ya simu, kwani hawana namba ya huduma kwa wateja? Au ofisini kwao, mbona kuna watu wanaappeal pale?
Sifahamu namba yao mkuu lakini hili Na mimi limeanza nipa mashaka japo nilikuwa Na matumaini makubwa sana Na pspr ila kwa hili wasipolitendea haki ntajua wazi wanamichezo michafu kama ambavyo mleta mada anasema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
May be and may be not..... Kuna kujitolea bure na kujitolea upate ya kujikimu.
Pia kuna suala la utunzaji Siri, kuna watu walufukuzwa kwa kulikisha taarifa yaani kila anachokiona full mitandao nk. Badala ya kufuatilia ni vijana wa tempo na WA field walihusika... From that point walisitisha tempo na field kwenye kitengo husika.
Wameomba msamahaa na wengine kukimbia ila ndo wamewafukuzisha wenzao kazi.
So rahisi kumwamini usiemjua na unaemjua ni muhimu kumwekea mashaka.
Sitetei ila nimejifunza mengi kwenye field na tempo works
Kujitolea free na bado watu hawataki,kuna jamaa humu ana degree ya Telcom,ana CCNA ,humu kuna thread yake kafungua zaidi ya mara mbili anaomba nafasi ya kujitolea free lkn zote hola,sasa hivi kijana wa watu ana shika chalk.Hapo bado hujaja kwa vijana wanaomba field ambao hawahitaji hela bali ujuzi,lakini bado hawapewe nafasi kwa TZ kama huna mtu utahangaika sana tena sana.

Mimi mwenyewe nilihangaika wewe ,mwisho wa siku kazi yangu ya kwanza ambayo nimejishikiza nimepigiwa pande.
 
Shida si degree shida utaratibu wa kazi husika, chanzo cha imani ni kuona /huwezi kuguarantee mtu usiemjua kwa undani.
Pia maisha yenu yana changamoto yaani yale ya sirini mnaweka hadharani na yale ya hadharani mnaweka sirini
Kuna kazi ilitoka na kigezo mwenye social network nyingi no za muda Mrefu.
Tasisi husika ikaingia kwenye page zao kuona matumizi ya Miranda, just imagine kati ya 100.waliofanikiwa 15.nafasi zilizotoka ni 43
Kujitolea free na bado watu hawataki,kuna jamaa humu ana degree ya Telcom,ana CCNA ,humu kuna thread yake kafungua zaidi ya mara mbili anaomba nafasi ya kujitolea free lkn zote hola,sasa hivi kijana wa watu ana shika chalk.Hapo bado hujaja kwa vijana wanaomba field ambao hawahitaji hela bali ujuzi,lakini bado hawapewe nafasi kwa TZ kama huna mtu utahangaika sana tena sana.

Mimi mwenyewe nilihangaika wewe ,mwisho wa siku kazi yangu ya kwanza ambayo nimejishikiza nimepigiwa pande.
 
Nilishakuwa refarii.nikampa sifa kijana alichoenda kufanya mungu anajua na siku anaondoka hata mimi niliekubali kuwa mdhamin hakunitaafu
Kujitolea free na bado watu hawataki,kuna jamaa humu ana degree ya Telcom,ana CCNA ,humu kuna thread yake kafungua zaidi ya mara mbili anaomba nafasi ya kujitolea free lkn zote hola,sasa hivi kijana wa watu ana shika chalk.Hapo bado hujaja kwa vijana wanaomba field ambao hawahitaji hela bali ujuzi,lakini bado hawapewe nafasi kwa TZ kama huna mtu utahangaika sana tena sana.

Mimi mwenyewe nilihangaika wewe ,mwisho wa siku kazi yangu ya kwanza ambayo nimejishikiza nimepigiwa pande.
 
Naona mnajadili sana PSRS mana ni wanazingua. Vip kuhusu kampuni binafsi mfano TBL, CEMENT,ALAF, SBL, KSCL,kuna kampuni hapo nafasi ya field tu wanataka ufahamiane na mtu, kuna jamaa anasema alienda kuomba dili TBL Mby akaambiwa kazi ipo ila tatizo jina alitoki ukanda wa mrefu mlima enzi izo Hr akiwa Te... mana kubebana wao kwanza ilikuwa ndo slogan yao enzi izo. Mapokezi tu unaenda unamkuta mdada analafudhi ya ukanda wa mlima utamweleza shida zako atakwambia mwaka huu iyo program haipo labda mwakani. Iyo kauli anaitoa kila mwaka uendapo , Tuendelee kutoalist ya kampuni zingine zinazozingua.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Habari zenu wanajamvi,
Naungana nanyi wote mlioko Tanzania kwa msiba wa kijana mwenzetu Ruge..! Hakika kazi yake ya hapa duniani ameimaliza na mungu ailaze roho yake mahali pema peponi,

Pia naona kwenye mitandao ya kijamii habari za kurudi nyumbani kwa mzee EL poleni pia mlioguswa kwa namna yeyote na huu uamuzi wake
Kama taarifa zitakuwa ni sahihi.

Niliahidi wiki ijayo siku ya alhamisi nitaleta humu uzi wa kuelezea fursa mbalimbali zilizoko nje ya nchi kwa wale watafutaji wanaoingia kihalali hili mpaka mda huu uzi ushakamilika unasubiri siku tu urushwe humu.

Leo naomba kuzungumzia ubovu uliopo kwenye michakato ya ajira unaowapa ugumu watoto wa maskini katika baadhi ya taasisi na mashirika ya umma na jinsi wakuu Hawa ambao michakato ya ajira ya taasisi zao haipitii utumishi wanavyopeana ajira kwa kujuana, ninayozungumza nina uhakika nayo kwa asilimia zaidi ya 100 maana nimefanya kazi serikalini kabla ya kuacha na kwenda nje ya nchi na nilipata kujenga connection na taasisi nyingi za serikali kwa nature ya kazi niliyokuwa nafanya hivyo Siri nyingi nilizijua.

Tangu psrs ( Sekretariati ya ajira) ianze kuratibu michakato ya ajira kwa taasisi na mashirika ya umma,. Urasimu na udanganyifu umepungua kwa kiasi kikubwa ( sio kwamba psrs haupo urasimu upo, huu urasimu nitauzungumzia siku moja), Leo nazungumzia hizi taasisi ambazo ajira zake hazipitii utumishi.

Kuna mashirika na taasisi ambazo ajira zake hazipitii utumishi Kama TANROAD, TANAPA, HIFADHI YA NGORONGORO, TANESCO, TPDC,WCF, NSSF, na hayo mashirika yaliyounganishwa kuunda (PSSSF) pia Kuna BOT, EWURA, TAKUKURU ziko nyingi Mimi nazungumzia hizi nilizo na uzoefu nazo.

Hawa BOT Kama hauna connection pale ya kukufanya ujulikane Basi hata wakikushortlist utaenda kukamilisha ratiba tu, nafasi zikitoka pale wanaanza kuulizana wao Kama Kuna mtu ana ndgu anakidhi vigezo then wanakuscreen kwa vimemo kwa watu wote wanaohusika na huo usaili ushahidi ninao sihitaji kuuweka wazi kwa watu walioingia hapo BOT kwa mlango huu, inaweza fanya wakanijua mapema maana wengi ni watu wangu wa karibu.

Kuna Hawa TANROAD ( Hawa ni warasimu kwelikweli kwenye masuala ya ajira) kwa nature za ofisi zao hasa mikoani kote isipokuwa makao makuu Hawa ofisi zao zinakuwa jengo moja na ofisi za Temesa, TBA, TAPE na pia huwa zinapakana na GPSA na kwenye hayo magodauni ya GPSA utazikuta ofisi za MSD wamepanga humo kwa ukanda wa ofisi hizi wafanyakazi wa TANROAD na MSD ndo huonekana matawi ya juu kwa sababu wanalipwa vizuri, Safari nyingi wanapata ikiwa wafanyakazi wa ofisi zingine Kama TANROAD,TEMESA, na GPSA wako hoi bin taaban ( labda kwa mfanyakazi wa GPSA kituo Cha mafuta huyu Yuko njema), hivyo hii inawafanya wawe wababe kwenye ukanda wa ofisi hizi, Hawa huwachukua ndgu zao au watoto wa kike wazuri waliohitimu vyuo wanawafanya vimada wao then wanawaweka kwenye ofisi wakiwa kama wafanyakazi wanaojitolea then nafasi za kazi zikitoka TANROAD mkoa wowote ule wanaanza kuwafanyia connection Kama mkoa husika uliotangaza hakuna mtu aliye ndani anafiti vigezo, kasheshe linakuja Kama huna mtu wa kukushika mkono hata nafasi ya kujitolea hupati labda uwe msichana mrembo then wakwere wakuone ukikubali masharti Yao Basi hapo utaula, MSD na TRA zamani nao walikuwa na tabia hii baada ya michakato ya ajira yao kuhamishiwa Psrs urasimu kwenye taasisi hizi umepungua.
Ushahidi wa taasisi hizi ninao na kwa kifupi fuatilieni ajira zilizotoka mwaka Jana mikoa ya tanga, njombe na Kilimanjaro, kigoma na ruvuma na kwingineko
Hawa ni watu ninaowajua na jinsi walivyopata kazi najua kwa hiyo najua ninachokiongea kwa zaidi ya asilimia 100

TANESCO Hawa ndo walewale ukiona umepata nafasi ya kazi hapa basi ujue wamemtafta wa kumuweka wamekosa, Tena Hawa wameenda mbali mpka nafasi zao za kazi Mara nyingi huwa wanatoa Kama "INTERNAL ADVERTISEMENT" tabia hii walikuwa nayo pia TPA kabla ya michakato Yao kuhamishiwa psrs, ili kuwapa nafasi watu wao waliowaweka kujitolea, Yaani hapa utakuta baba meneja, mtoto dereva, mwipwa afisa ugavi, binamu mhasibu hawaachani na TANAPA, Hifadhi ya ngorongoro na WCF ( kwa Sasa Hawa ndo wanaolipa vizuri + malupulupu kwa taasisi za serikali) Wala NSSF.

Hizi tabia zinachangia kuwafilisi watoto wa maskini just Imagine haya mashirika yanatoa nafasi labda Kilimanjaro, mtu Yuko ruvuma Hana nauli anauza mifugo au anakopa kwenda usaili ambao wenye michakato ya ajira wanajua nani mshindi wa kazi husika.

Pia hivi vibali wanavyopewa mameneja wa taasisi kuajiri watumishi wa mikataba nashauri hapa kuwe na utaratibu mzuri. Nakumbuka ilishawahi kufanyika ofisini kwetu kulikuwa Kuna upungufu wa madereva, phone operator, mhasibu,mgavi na mhudumu wa ofisi kwa uhitaji wa watumishi Hawa tulipewa kibali tuajiri ajira za mikataba, mimi nilianda tangazo then likasambazwa kubandikwa kwenye ofisi za serikali ili watu waone waweze kuomba ilikuwa mwaka Jana na kweli watu waliomba wengi, tukaita wote usaili ukafanyika na meneja alikuwa sauti ya mwisho kwenye hizi ajira Cha kushangaza watu walioitwa kuanza kazi wote ni ule mkoa anaotoka boss, siku zilivyoenda tukaja kugundua kumbe ni jamaa zake, na hii iko karibia ofisi zote za umma kwenye hizi ajira za vibali maalumu wanawekana kwa undugu na ujamaa na hapa ndo MAUMIVU yanapokuja kwa mtoto wa mkulima na maskini ambaye kwenye familia anakuwa hana mtu wa kumuongoza.

Nini kifanyike:

Ajira zote za serikali na mashirika yake zipitie Sekretariati ya ajira katika utumishi wa umma watu washindanie huko, haina maana ya kuundwa chombo hiki halafu taasisi zingine ziendelee kuajiri zenyewe wakati zinatumia pesa za umma, maana kwa Sasa zile taasisi zinazolipa vizuri zinaajiri zenyewe na ambazo Zina Hali mbaya kimaslahi ndo ajira zake zinapitia utumishi that's why Hawa watoto wa kimaskini wakishapata ajira huko mawazo yao yanakuwa ni kuhama taasisi kwenda taasisi zinazolipa vizuri na sio kufanya kazi kwa ufanisi.

Mungu ibariki Tanzania
ULIYOYASEMA NI UKWELI MTUPU. BAADHI YA MASHIRIKA YA UMMA KAZI ZA MIKATABA YA MUDA MAALUM HAZITANGAZWI POPOTE. NDUGU WA WAOMBA KAZI WANAENDA OFFICE YA HR WANAPEWA MIKATABA YA MUDA. HIYO MIKATABA YA MUDA HAIISHI MPAKA WANAPEWA MIKATABA YA KUDUMU. HAKUNA USAILI WOWOTE.
ILI KUIZUGA JAMII WANATANGAZA INTERNAL ADVERT LAKINI UKWELI NAFASI HIZO HUWA TAYARI ZIMEJAA. KIBAYA ZAIDI WANAOLETWA KWA MTINDO HUO HUWA NI VILAZA WA KUTUPWA.
 
Mkuu ni hatari mno kwa taifa
 
Naona mnajadili sana PSRS mana ni wanazingua. Vip kuhusu kampuni binafsi mfano TBL, CEMENT,ALAF, SBL, KSCL,kuna kampuni hapo nafasi ya field tu wanataka ufahamiane na mtu, kuna jamaa anasema alienda kuomba dili TBL Mby akaambiwa kazi ipo ila tatizo jina alitoki ukanda wa mrefu mlima enzi izo Hr akiwa Te... mana kubebana wao kwanza ilikuwa ndo slogan yao enzi izo. Mapokezi tu unaenda unamkuta mdada analafudhi ya ukanda wa mlima utamweleza shida zako atakwambia mwaka huu iyo program haipo labda mwakani. Iyo kauli anaitoa kila mwaka uendapo , Tuendelee kutoalist ya kampuni zingine zinazozingua.
Ushasema kampuni binafsi...hapa hata wewe

Ushasema kampuni binafsi, hata wewe unaweza anzisha yako na ukamuweka mkeo awe meneja.
Hiyo sio Mali ya umma
 
Kuna Mazingira lazima uanze internal advert km mtu kajiendeleza kwa nn asipate?.hii hupunguza internal conflicts na ukute aliejiendeleza anajua mengi, kuliko mpya.. Pia km mtu kajitolea miaka 3 kazi imetoka lazima umrekomend ikiwa tu ana vigezo. Lakini km ni wale ambao wanajitolea, hajakabidhiwa anakiburi dharau nk huyo ni kuto mrekomend. Kuna faida kumrekomend mtu aliejitolea maana anajua Mazingira ya kazi kuliko mtu mgeni anaefuata green pastures tu
Mkuu nakupinga kwa asilimia zote, nafasi za kuingilia unatangaza Kama " Internal Advertisement" hii ni kuhalalisha loop ya urasimu katika ajira
 
Mkuu nakupinga kwa asilimia zote, nafasi za kuingilia unatangaza Kama " Internal Advertisement" hii ni kuhalalisha loop ya urasimu katika ajira
1980s kulikuwa na mradi chakula bora kulikuwa na kitu km hicho nikamuuliza kwa nini huo mradi ukawa hivyo nikajibiwa kuku unaemfuga haitaji kamba mguuni wala manati.maana anajua utaratibu wa nyumbani kwao,kulikuwa na watu wamejiendeleza ila waliajiriwa kwa sifa za awali na masharti lazima wapewe intavyuu ili waweze kupewa maslahi stahiki na sifa zao mpya,just zawadi kwa utumishi wao.
hakuna kisicho na madhara,kutofautiana ndo maendeleo,kuna uhusiano mkubwa na uzoefu ktk nyanja tofauti,mahali pakazi ni km ndoa ila mtu ana uzoefu wake kwa hiyo sikupingi,watu wengi husema shilingi inapande mbili mm naamin inapande tatu.
 
Back
Top Bottom