Kwanini Arusha imekuwa ni ngome ya CHADEMA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Arusha imekuwa ni ngome ya CHADEMA?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kasimba G, Apr 10, 2012.

 1. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Ukiongelea ngome za CDM majiji yote kasoro Tanga, Yaani mbeya, Dar, Mwanza na Arusha, lakini arusha wana special case, ndio maana tathmini ya watu wanasema hata CDM ikisimamisha jiwe watashinda, hivi wanajf wenzangu mmeisha wahi tafakari sababu ni nini?

  Kwa jiji la Arusha, viongozi wengi saana wa serikali na chama i.e. CCM kwa kutumia kigezo cha jiji la kitalii, wamawekeza saana huko, sasa raia wa kawaida wanaona mambo hayo kwa macho yao, hivi unafikiri wenyewe wanafikiri viongozi hao wanatoa wapi mabilioni ya kuwekeza Arusha kama sio kuiba! Ndio msingi haswa unaosababisha CCM isieleweke arusha.

  Kwa sehemu nyingine za nchi hawajui source ni nini, ndio maana hata wanaCCM wanaokaa arusha only a few wanaweza ku VOTE kwa CCM, wanaona madudu hayo!

  Nawasilisha!
   
 2. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Alafu pitia takwimu za wizara ya elimu arusha kuna shule nyingi za sekondary hata kabla ya shule za kata so watu wanajua haki zao.
   
 3. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,770
  Likes Received: 6,098
  Trophy Points: 280
  Inaonekana Arusha ni mji (sipendi kuita jiji nikikumbuka majiji kama Tokyo, Dubai, Beijing, NY, Cairo, n.k.) wa kiharakati zaidi.

  Watu wa Arusha wengi wao maisha yao wanaishi kiharakati kulinganisha na miji mingine na kwa kuwa CDM (hata Mh. Pinda aliwahi kutamka hivyo) mambo yao wanafanya kiharakati then Arusha na CDM ni kama mapacha. Hayo ni mawazo yangu.
   
 4. E

  EGPTIAN Member

  #4
  Apr 10, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aah! Arusha walamba kisusio ni wengi sana! Mbegeni wanahamasishana CDM kuchukua nchi.
   
 5. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #5
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Wajinga wajinga wamepungua Arusha waliobaki ni fighters ambao wamegundua kuchelewa kwao kimaisha moja ya sababu ni ccm, ndio maana Arusha ukisimamisha jiwe na jk ,jiwe litashinda ilmradi liwe na bendera ya Chadema!chadema kama chama kinapendwa Arusha ccm ni sehemu ya matatizo ya Arusha
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Apr 10, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Wajinga wametoweka kwa kiwango kikubwa Arusha. Mtaji wa ccm siku zote ni wajinga! Hata rais aliyetangazwa mshindi na NEC anajua ccm haina chake Arusha, kwasababu watu wa Arusha wamepata elimu ya democrasia, ndiyo maana tokea atangazwe mshindi hajawahi kukanyaga Arusha kwa kufanya Mkutano.
   
 7. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #7
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Kule Arusha watu wana uelewa sana kuhusu haya majambazi ccm but so kama kule tanga kwani wao hawajui chochote kile kwao kazi ni midundiko, vigodoro usiku kucha mpaka asubuhi zas y mi huwa nasema sehemu ambazo zimekaliwa na waarabu watu wake wengi huwa ni vilaza wa elimu ya uraia.
   
 8. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #8
  Apr 10, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Ukiona sehemu kuna wanaopenda cdm wengi basi ujue kuna wenye akili wengi zaid!!!!!
   
 9. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #9
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Of last alipokuja aLIIngia usiku wa saa 1.30, akalala sehemu ya maficho, na asubuhi kafungua mkutano wa Takukunguru AICC, na by saa 4 akachapa lapa kurudi Dar, chini ya ulinzi mkali ajabu!

  Arusha ni jeshi kubwa sana linaloendelea kukua...kizazi cha sasa chote, tuseme Primary na Secondary schools hakuna mwanafunzi yeyote anayeweza kutamka, acha kushabikia ccm, walishapita enzi hizo, wako ng'ambo ya pili!...kuna picha ilibandikwa humu wakati wa kampeni Arumeru, watoto wa Nursery wamepiga full-kombati(aka magwanda), sasa fikiria watoto kama wale utaanzia wapi kuwabadili fikra zao kichwani waipende ccm, maana akili yao ishajua ccm=mafisadi!

  Kizazi cha ccm cha akina Mzee Mrema(aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini)kinapukutika kwa haraka, na hata leo hii ukifanyika uchaguzi wa Mbunge Arusha, zile kura
  36,000 alizopata Buriani hazitaweza kupatikana tena, sanasana wataishia na nusu yake, au chini ya hapo.

  Imagine leo watu walikuwa wanazima moto uliokuwa unateketeza vibanda eneo la 'Chini ya Mti', huku wakiimba Peoples Power!...Sasa fikiria kazi ya kuzima moto ni ya kijamii, na wala haihusiani na siasa kabisa, lakini zoezi zima lilitiwa hamasa na slogan ya chadema!

  Arusha iko Next Level!
   
 10. Ba Martha

  Ba Martha JF-Expert Member

  #10
  Apr 10, 2012
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  A twn mji wa wajanja...na watu wanajitambua...i wish watu wa Tanzania nzima wangekuwa kama pipo za A twn..coz hata watoto wadogo huwaambii kitu kuhusu CDM. Pita kila kona ya mji, gereji, sokoni, n.k....ni chama kubwa CDM.
   
 11. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #11
  Apr 10, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  mi nadhani ni kutokana na shughuli kuu mbili.....madini na utalii.....watu walio wengi kama hafanyi kazi zinazohusiana na utalii basi ni mfanyabiashara wa mawe.....sasa ukiangalia sekta hizi mbili zimefisadiwa sana na wahanga walio wengi ni vijana....hivyo wakazi wa mji huu wanajaribu kutetea kama sio kurudisha hadhi ya mji wao....enzi za tanzanite Arusha ilikuwa mji wa asali na maziwa....
   
 12. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #12
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Arusha ni kitovu cha mabadiliko makuu ya kisiasa na mustakabali wa taifa hili,
  hii ni tokea zama zile za awamu ya kwanza.
  Ushahidi unaoishi ni Azimio la Arusha ambalo wasomi wa bara la afrika wanasema lilisimika dola la kiafrika na kuasisi fikra za kimapinduzi katika namna ya mtu mweusi anavyoweza kujiongoza na kusimamia rasilimali zake.
  Damu ya "Azimio la Arusha" ndio kiini cha wakazi wa Arusha kuchukia utawala ulioua AZIMIO hilo na hvyo umma huo kugeukia kwa upande unaonekana kusimamia harakati zilizohimizwa na Azimio la Arusha,.....
  KUJITEGEMEA!
   
 13. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #13
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mkuu,
  Ulipotaja gereji umenikumbusha sehemu moja hapa A-Town inaitwa SIDO(kuelekea Unga-Ltd), kuna magereji mengi sana, actually wengi tunatengenezea huko mikweche yetu, maana services hazina tofauti na magereji makubwa, lakini bei ni ya kizalendo sana!

  Eneo hilo lilitekwa na ccm, wanalifanya ni lao kabisa!...Sasa balaa ya eneo hilo hakuna mtu hata mmoja wa ccm katika population inayozidi watu 2000 wa hapo. Lakini kwa vile eneo ni la ccm, wote wamebaNDIKA picha za Kikwete na bendera za ccm zinapepea vibaya mno, mioyoni ni watu wa level nyingine kabisa wote ni cdm damu!
  Wanasema hawana jinsi ya kuishi hapo kinyume na kuonyesha unaipenda ccm, maana utafukuzwa na kuporwa eneo.

  Peopleeees Power!
   
 14. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #14
  Apr 10, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  kumbe jombaa na wewe ni chama la kule kwa wakereketwa....
   
 15. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #15
  Apr 10, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  sehemu yenye watu walioelimika hawawezi kuipenda ccm/ mfano Arusha, moshi, mwanza, mbeya, hata shinyanga wako vizuri sana. Kigoma nako wakali kweli kweli.
   
 16. s

  sverige JF-Expert Member

  #16
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 361
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  nakumbuka ile fujo ya ngaramtoni duh inataka moyo naile nyomi iliyokuwepo
   
 17. Skp2ole

  Skp2ole Senior Member

  #17
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nashukuru kwa kuukubali mji/jiji letu kwa mabadiliko ya kisiasa na kijamii na hakika Arusha ndo italeta mapinduzi ya kisiasa nchi hii. Kwa msisitizo peoplessssssssssss powerrrrrrrr ndo tunataka kufanya salamu yetu na baadaye iwe ya kitaifa wakuu
   
 18. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #18
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kule kwa maukweli besti!...Ngoma inapigwa service kwa 40K wakati ukienda pale Captain Sakina unalambwa 100K!
   
 19. H

  Hemed Maronda Senior Member

  #19
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Acha matusi Arusha ni kama sehemu nyingine yoyote katika Tanzania sema UBINAFSI UDINI NA UKANDA ndo umewajaa sana na watu wengi wa Arusha wanaona Chadema ndo mali yao kwakuwa kina Mwenyekiti ambae ametokea Hai na ni mkwe wa muasisi wa Chadema pia Katibu Mkuu ni kutoka Mbulu hivyo kutokana na ubinafsi walokuwa nao wanaona hawana Chama cha kushabikia zaidi ya Chadema na ajenda yenu ya kutaka kuwatumia Watanzania wengine kwa kuwadanganya kuwa Chadema itawaletea ukombozi watu washagutuka na hiyo ajenda ya SIRI!
   
 20. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #20
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Mia ya mia chali R huku ccm hainaga kitu aaarifu ni sawa na inapiga sarakasi huku imefaa taulo tu.
   
Loading...