Kwa experience yangu.
Kila mtu anakuwa na turn offs au deal breakers zake. Tunaweza ziita "Vunja Mkataba" zake. Wanaume wengi naona tunazo common kadhaa ila nyengine tunapishana kama ilivyo tabia, hatufanani.
Unakuta mtu unamkubali vzur, lakini unakuja kupata deal breaker, inakulazmu ujitoe.
Unakuta,
- Mdada analazimisha ndoa wakati wewe bado hujapitisha TBS vizuri, au tu kama mwanaume unaona conditions bado haziko sawa, ila mwenzio anakupa timeline na kuforce sana. Unajikuta unaamua acha usiwe kikwazo kwenye maisha yake. Unajitoa.
- Unagundua mwenzio ana mindset flan unaona kabisa hii itakua shida mbeleni.
- Unagundua si muaminifu, ni mwizi, mshirikina, au ana tamaa sana ya mali na maisha, au ushindani usio wa maana. Unaona isiwe kesi, unajitoa.
- Labda kuna tabia haikupendezi na kila unavyojaribu habadiliki. Hapa wengine unaskia wakisema "Me ndo nilivyo hata wengine wameshanizoea hivi." kimoyo moyo unasema sawa. Ila mimi si wengine. Unajitoa.
Wengine waongezee deal breaker zao.
Mfano mimi kuna tabia naweza kukuvumilia maana najua binadamu hatuja kamilika. Ila ukini cheat, aisee hilo Nimejigundua siwezag kusamehe. Nitajitoa!
Ongezea za kwako...
Sent using
Jamii Forums mobile app