Kwanini " Ametekwa" Isiwe " Amekamatwa na Polisi"

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,833
2,790
Kutekwa na Kukamatwa na Polisi

Maneno hayo mawili hapo juu yapo tofauti sana.
1. Kutekwa ni tukio linalompata mhanga bila taarifa. Kukamatwa na Polisi ni jambo linalokuja na kumpata mhanga kwa njia ambayo kila mwanajamii anakuwa na taarifa nalo.
2. Kutekwa silaha hutumika lakini Kukamatwa na Polisi silaha ni nadra sana kutumika inategemea ukubwa wa kosa na tabia ya mtuhumiwa.
3. Kutekwa hufanywa kwa kificho, inadaiwa na kuondoshwa mara moja, lakini kukamatwa na Polisi ni jambo linalofanyika taratibu zake zikianzia kwa mjumbe kisha kwa mhanga mwenyewe.
4. Kutekwa hakuelekezi mhanga anapelekwa wapi, Kukamatwa na Polisi huahinisha mhanga anapelekwa kituo gani.
5. Kutekwa nguvu hutumika ikiwa ni pamoja na kumkamata mhanga kumuingiza kwenye gari na kuondoka mara moja, Kukamatwa na Polisi taratibu kufuatwa na mhanga huingia mwenyewe kwenye gari la Polisi.
6. Kutekwa (Kidnap) Kukamatwa na Polisi (Arrest)
7. Watekaji hawavai sare Polisi wakamataji mara nyingi wana vaa sare zao.
8. Aliyetekwa hana matumaini ya kurudi salama, aliyekamatwa na Polisi huwa na moyo uliotukuka kurudi salama.
9. Aliyetekwa hana dhamana kwani huwa hajulikani aliko, aliyekamatwa na Polisi nyuma yake kufuatwa na watu wanaotaka kumdhamini.
10. Wengi wa waliotekwa hawana la kusema ikiwa wataachiwa kwani hupata vitisho, wote waliokamatwa na Polisi mashitaka yao huwa wazi kila mtu hujuma.
11. Watekaji kamwe hawaonyeshi vitambulisho, Polisi wakamataji huonyesha vitambulisho ikiwa mhanga atataka kuona vitambulisho.
12. Magari wanayotumia Watekaji ni TINTED Polisi Wakamataji hutumia gari ya WAZI PICK UP.
13. Watekaji kutenda utekaji wao popote alipo mhanga, Polisi Wakamataji humfuata mhanga mahali anapopatikana hasa nyumbani ili jamii itambue kuwa mhanga amekamatwa na polisi.
14. Watekaji hawajulikani ni akina nani, Polisi Wakamataji wanafahamika kuwa ni Polisi na hata majina hujulikana.

Tofauti hizi chache nilizoahinisha ndizo zinazosababisha wananchi kutamka kwamba fulani Katekwa na watu wasiojulikana kwasababu njia ya kumkamata mhanga siyo ya kawaida kama ulivyo Ukamataji wa Polisi.
 
Back
Top Bottom